Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Mgeni akifika Zanzibar, Watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Chupi inaitwa chupi (mitaani itaitwa KUFULI)
Hafu ni vazi la kizamani , Lipo kama sketi nyepesi hivi ,zamani wanawake wa kipwani walikuwa wakivaa hafu n'a sketi juu yake.
Round about inaitwa hivyo hivyo, ikipinda baada ya Kona. Sufuria ndogo Dishi ni sufuria kubwa, kisima kuna cha mashine na cha kamba (kutofautisha). Bomba la maji wanaita mfereji , shule wanaita skuli , chèpe pauro (sio Paulo).... Charles Hilary ana lafdhi ya kule, kalelewa na kukulia kule .... Mi naona wanaongea Sawa tu.... Au labda kwa kuwa ni mswahili wa kuzaliwa.... Ukienda Tanga / Mombasa wanalafudhi nyengineee, Mtwara / Lindi.... Kiswahili kikubwa (usisahau lahaja rasmi ya lugha ya Kiswahili ni Kiunguja mjini) Wasalimie Mchamba wima , Mwembe mchomeke .... Hongera kwa kufika Zanzibar. Kura mpe Serif na Lisu ....😁
 

Daah zenji siyo daah nilihisi Kama sipo Tanzania wale watu sijui wametokea wapi au waarabu walikusanya watu kutoka mataifa mbalimbali ya afrika maana si kwa lafudhi ile.
Nilienda maeneo ya kusini mwa unguja huko daah.
Kule ni makunduchi wana lugha tofauti kabisa wazanzibar wengine huwezi elewa Kama c mmakunduchi
 
Hahahahaha eti nini!?
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
 
Inasikitisha na kuudhi sana kusema kweli. Wavifute tu vyama vya upinzani tujue moja tu kuliko haya maafa ya kutisha.
Most probably maana sidhani kama wana sababu nyingine ya msingi 😏😏
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
Uwongo!
 
Inasikitisha na kuudhi sana kusema kweli. Wavifute tu vyama vya upinzani tujue moja tu kuliko haya maafa ya kutisha.
Hii nchi ni pasua kichwa sana 🤨🤨🤨
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Zenji basi yaajabu sana akati huku daladal ni yutong wao canter mitsubish.!
Kipind hicho Dar es salaam walikua wanapenda kkuita "BONGO.!"
Lkn zinaenda kupungua mkuu Kuna mi kosta yakutosha.. hizo mbavu za mbwa zitakuwa za kubeba mizigo, lakini hata hivyo zile gari zipo njema sio mbavu za mbwa tu bali ziitwe roho ya paka.
 
Neno li... znz.. nawatumii

na komeo inaitwa komeo ..li chacha...labda ni ki mrima hicho!
Wabongo watu wa ajabu sana, badala ya kuwashangaa Wasukuma na kiswahili chao cha ajabu ajabu(maana hata hawajui matumizi ya R na L) eti wanataka kusema Zanzibar hawajui kiwahili! Aguju!!! Kwa taarifa tu kule kiswahili ndio lugha mama. Kama mtu ataongea lugha nyingine basi hiyo ni yakujifunza
 
Back
Top Bottom