Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Ntafika one day vipi kuhusu sekta za serikali kuajiriwa inawezekana?
Au nako ubaguzi mwingi?
Naskia tu huko vijana wengi hawafatilii shule kabisa
Unafuu wa maisha uko vipi?
Kule maisha yana gharama kwa kiasi chake hasa mjini sehemu za kitalii na za kihistoria ila kwa shamba sidhani! Kuhusu ajira au biashara nadhani ni hadi uwe na kitambulisho!
 

Daah zenji siyo daah nilihisi Kama sipo Tanzania wale watu sijui wametokea wapi au waarabu walikusanya watu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika maana si kwa lafudhi ile. Nilienda maeneo ya kusini mwa Unguja huko daah.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Eti n'tie dole hapo.
[emoji23][emoji23] Ni vituko vitupu

Siku hiyo nilikuwa Forodhani nauliza eti maeneo haya huwa wanapika vyakula kama wali au pilau! Yule dereva wa bodaboda aliyenipakia akaniambia huku sana sana wanapika bites na seafoods hasa mida ya jioni ila ukitaka vyakula kama wali harage (hapo kwenye harage nilicheka) au sembe (ugali wanaita sembe) labda utafute maeneo mengine!

Nikawaza kwani angesema tu wali maharage angekufa? Ukiwa mgeni kama haujawazoea unaweza hisi wanafanya makusudi!
 
kwa kauli hii ya ntie dole nmeamini hakuna right and wrong lakn inategemeana na jamii husika ina define vp jambo husika.
Yes kwa nchi nyingi sana kuna maneno yanaingiliana ila tu yanakuwa na maana tofauti unakuta neno fulani kwa lugha fulani lina maana nzuri kwa lugha nyingine lina maana mbaya! Mfano South Africa neno "mkundu" (ashakum si matusi) ni jina la mtu na lina maana nzuri tu!
 
[emoji23][emoji23] ni vituko vitupu

Siku hiyo nilikuwa forodhani nauliza eti maeneo haya huwa wanapika vyakula kama wali au pilau! Yule dereva wa bodaboda aliyenipakia akaniambia huku sana sana wanapika bites na seafoods hasa mida ya jioni ila ukitaka vyakula kama wali harage (hapo kwenye harage nilicheka) au sembe (ugali wanaita sembe) labda utafute maeneo mengine!

Nikawaza kwani angesema tu wali maharage angekufa? Ukiwa mgeni kama haujawazoea unaweza hisi wanafanya makusudi!
Eti "wali harage"[emoji3][emoji3] hawa watu bhana na hiyo lafudhi yao sasa ni balaa.

Kufundisha wanasema kusomesha!

Utasikia "mwl Zuberi asomesha skuli gani"? Hapo anauliza mwl Zuberi anafundisha shule gani.
 
Eti "wali harage"[emoji3][emoji3] hawa watu bhana na hiyo lafudhi yao sasa ni balaa.

Kufundisha wanasema kusomesha!

Utasikia "mwl Zuberi asomesha skuli gani"? Hapo anauliza mwl Zuberi anafundisha shule gani.
[emoji23][emoji23] [emoji1787][emoji1787]

Makazi (Nyumba) wanaita Makalio
Utasikia mafuriko yameharibu makalio ya watu zaidi ya 600

Kubisha wanaita Kudinda
Utasikia mie nilimuambia fanya hivi usifanye vile yeye akadinda

Majina ya maeneo sasa ndiyo utacheka uzimie sijui Mchamba wima mara Kibanda maiti! Kuna sehemu inaitwa sijui Banda la Karafuu kata ya Pita na Zako!
 
Kule Bububu kuna sehemu inaitwa bububu kwa nyanya yaani nilikua nacheka sana nikisikia hilo jina. Kingine umesahau nyanya maji wanaita Tungule.

Mti wanaita kijiti, Shamba wanaita kondeni.

Sasa vituko full nilivipata sehemu fulani inaitwa jambiani, huko Kiswahili chao huwezi kukielewa. Niliuliza mtu anielekeze sehemu yaani alivyonielekeza hata sikumuelewa. Kuna mdada alimwambia jamaa "Kama unan'tenda nintende, Sio unanichezea kama kijibwa chaja"😀😀 Hapo jamaa anaambiwa kaa unanifanya nifanye sio unanichezea kama kimbwa kitoto... Jambiani, Kizimkazi na Makunduchi is a place to be. Nilipenda sana mazingira yake
 
Kumbe umefikia kwa Ally...!? Basi kheri hata hapo siyo mbaya ila fanya haraka ikiwezekana ufanikishe kabla ya hiyo tarehe 30. Halafu simu nayo umebadili au maana hupatikani?
 
[emoji23][emoji23] [emoji1787][emoji1787]

Makazi (Nyumba) wanaita Makalio
Utasikia mafuriko yameharibu makalio ya watu zaidi ya 600

Kubisha wanaita Kudinda
Utasikia mie nilimuambia fanya hivi usifanye vile yeye akadinda

Majina ya maeneo sasa ndiyo utacheka uzimie sijui Mchamba wima mara Kibanda maiti! Kuna sehemu inaitwa sijui Banda la Karafuu kata ya Pita na Zako!
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom