Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Yani we acha tu! Nilisikia eti aliyewahi kuwa rais wa South Africa Thabo Mbeki ana mtoto wa kike anaitwa Sito Mbeki ila hiyo nahisi watu walizusha tu mitandaoni!
😀😀😀😀

Aisee. Ila inawezekana tu maana kwa huko kwao hayo majina yanaweza kuwa na maana nzuri kabisa.
 
Niliendaga field huko 2012, nilishtuka kuambiwa nenda kachukue maji mferejini pale mkaoge 😂😂😂😂
 
Mgeni akifika Zanzibar, Watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!

Kuna kipindi Zanzibar pombe ilikuwa mahotelin Tu na bar moja ya CCM.

Sijui sasa

Sasa condoms aisee zilikuwa zinauzwa Duka moja tu pale mjini
 
[emoji23][emoji23] [emoji1787][emoji1787]

Makazi (Nyumba) wanaita Makalio
Utasikia mafuriko yameharibu makalio ya watu zaidi ya 600

Kubisha wanaita Kudinda
Utasikia mie nilimuambia fanya hivi usifanye vile yeye akadinda

Majina ya maeneo sasa ndiyo utacheka uzimie sijui Mchamba wima mara Kibanda maiti! Kuna sehemu inaitwa sijui Banda la Karafuu kata ya Pita na Zako!
😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀


Wewe hebu acha kunivunja mbavu mbele za watu mie yani umenifanya ni-screenshot hii comment nije nicheke na baadae. Wewe umetembea sana huko aisee ngoja nami nijipange nije kwenda huko niinjoy maisha.

KENZY jipange tutaenda huko mchamba wima.
 
mhhhh ..
Yes kwa nchi nyingi sana kuna maneno yanaingiliana ila tu yanakuwa na maana tofauti unakuta neno fulani kwa lugha fulani lina maana nzuri kwa lugha nyingine lina maana mbaya! Mfano South Africa neno "mkundu" (ashakum si matusi) ni jina la mtu na lina maana nzuri tu!
 
😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀


Wewe ebu acha kunivunja mbavu mbele za watu mie yani umenifanya ni-screenshot hii comment nije nicheke na baadae. Wewe umetembea sana huko aisee ngoja nami nijipange nije kwenda huko niinjoy maisha.

KENZY jipange tutaenda huko mchamba wima.
Ha ha! Usihofu
 
Duh nikiskia huko zenji huwa nawaza kuwa ni sehemu ya kipekee sana.
Lafudhi kama hizo vyakula tofauti vyao,mavazi,
Kama hujui unaweza mtia dole kweli.
Vipi mkuu pisi zipo huko zinatafunika?
Watu wanaingia na pigo gani?
Shida gonga mali ya mtu akubambe na "wao"wanakugonga vizuri tu huku "mpenzi"wenu anashuhudia na wala hawakutangazi mwenyewe tu unahama kimya kimya na wana namba yako wanakusalimia mpaka unabadili namba
 
Yes kwa nchi nyingi sana kuna maneno yanaingiliana ila tu yanakuwa na maana tofauti unakuta neno fulani kwa lugha fulani lina maana nzuri kwa lugha nyingine lina maana mbaya! Mfano South Africa neno "mkundu" (ashakum si matusi) ni jina la mtu na lina maana nzuri tu!
Ni kama wahindi wana makna ya akna KUMAR wakat huku ni tusi
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
 
Yani we acha tu! Nilisikia eti aliyewahi kuwa rais wa South Africa Thabo Mbeki ana mtoto wa kike anaitwa Sito Mbeki ila hiyo nahisi watu walizusha tu mitandaoni!

Nafikiri her actual name ni Sithole Mbeki..


Kulikuwepo na waziri anaitwa Jackline Nthombeni.
 
Back
Top Bottom