Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Acha uongo.
 
Lakini mbona kwao kwenyewe kuna mji unaitwa Makunduchi! Tena nasikia kiswahili wanachoongea wa kule Makunduchi ndiyo balaa bora hata cha wa huko mjini!
Yaani mtu akikuita mmakunduchi, ana maanisha wewe ni mjinga was mwisho. Ya wamakunduchi wale jamaa ni zero brain kabisa
 
Wanasema maeneo hayo yalikuwa na majani yenye miiba (mbigiri) enzi hizo kabla ya maji ya mfereji kuna, walikuwa wanachamba kwa kuburuza Makarios mchangani , sasa eneo hilo walishindwa kwasababu ya miba miba; Hivyo ikabidi wawe wanachamba wima kwa majani kama tissue! NDO PAKAZOELEKA MCHAMBA WIMA
Acha uongo!

Kuchamba ni kutawadha.
Wima ni ukiwa umesimama.
Eneo linaloitwa Mchamba wima, chanzo chake eneo hilo ilikuwa ikinyesha mvua wakati wa kupita maji yalikuwa yanajaa, hivyo ukipita inakuwa nisawa na unatawadha (kuchamba) ukiwa umesimama. Ndio maana ya kuitwa mchamba wima.
 
"Konda nishushie poro langu au wanasema kiporo"[emoji23][emoji23] poro ni mzigo kama vile unga wa kilo 25 au mchele.. akienda dukani kununua mchele wa kilo 25 au unga wanaita poro la sembe au poro la mchele.. for the first time kwenye gari kuna mama alikuwa anashuka akamwambia konda nishushie kiporo changu [emoji23][emoji23] mi nikajua uporo chakula kilicholala hatari tupu.[emoji28]
[emoji23][emoji23][emoji23] poro ni mfuko was kiroba.
 
Dagaa mchele wanaita UPAPA[emoji16][emoji16][emoji16].
ZANZIBAR napapenda sanaaa.
Msivunje Muungano nyie ni ndugu zetu..
Siyo kweli. Hivi chief unapata raha gani kuongea uongo.
Sardine = upapa
 
Wanajamii forum, naomba kuuliza. Hivi mtu huwa anajiskia raha gani kuongea uongo au kuongelea kitu ambacho hakijui ukweli wake? Kwanini kama mtu hajui maana au tafsiri ya kitu asiulize kwa wenye kujua? Au anapata faida gani kuongea uongo??
 
Kuna kipindi Zanzibar pombe ilikuwa mahotelin Tu na bar moja ya CCM.

Sijui sasa

Sasa condoms aisee zilikuwa zinauzwa Duka moja tu pale mjini
Mpaka sasa condom ni ishu mpaka uwe mzoefu.

Sehemu za pombe ziko kibao siku hizi
 
Na wanaoita markiti labda watu/wazee wazamani.
Tatizo watu hawaelewi, Zanzibar ilikuwa chini ya tawala mbili kwa wakati mmoja.
Ilikuwa ni Koloni la Waoman na Waingereza kwa Ujumla, hivyo kuita vyovyote vile ni sawa
English Market = Marikiti
Arabic (السوق) Souk = Soko
Sasa hapo tatizo lipo wapi hapo?
 
Acha uongo!

Kuchamba ni kutawadha.
Wima ni ukiwa umesimama.
Eneo linaloitwa Mchamba wima, chanzo chake eneo hilo ilikuwa ikinyesha mvua wakati wa kupita maji yalikuwa yanajaa, hivyo ukipita inakuwa nisawa na unatawadha (kuchamba) ukiwa umesimama. Ndio maana ya kuitwa mchamba wima.
Mulemule
 
Wanasema maeneo hayo yalikuwa na majani yenye miiba (mbigiri) enzi hizo kabla ya maji ya mfereji kuna, walikuwa wanachamba kwa kuburuza Makarios mchangani , sasa eneo hilo walishindwa kwasababu ya miba miba; Hivyo ikabidi wawe wanachamba wima kwa majani kama tissue! NDO PAKAZOELEKA MCHAMBA WIMA
[emoji115][emoji115]Mule mule wapi? Uongo ulioandika haufanani na maelezo yangu! Acha uongo!!

Back
Top Bottom