Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Wanafanya kusudi kutukana
Kuna kituo Chao kimoja kinaitwa 'ikikuuma seema'
Konda mkifika anasema 'kikuuma'..

Wanapenda lugha za matusi sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna muda hata mie nahisi huwa wanafanya makusudi kabisa
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Aisee. Ila inawezekana tu maana kwa huko kwao hayo majina yanaweza kuwa na maana nzuri kabisa.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kazi kweli kweli
 
Ni kweli
Ila hilo Sitho ni ufupi
Ndo wabongo wakaliunga na la babake
Inakuwa hivyo..
Kulikuwepo na waziri anaitwa jina tusi kuliko Hilo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Niliona kuna mtu humu alishawahi kuweka list ya viongozi wenye majina ya ajabu kama hayo
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]


Wewe ebu acha kunivunja mbavu mbele za watu mie yani umenifanya ni-screenshot hii comment nije nicheke na baadae. Wewe umetembea sana huko aisee ngoja nami nijipange nije kwenda huko niinjoy maisha.

KENZY jipange tutaenda huko mchamba wima.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
We cheka tu mama, ila Zanzibar ni kuzuri sana.
 
Nafikiri her actual name ni Sithole Mbeki..


Kulikuwepo na waziri anaitwa Jackline Nthombeni.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Ila wasauzi nao majina yao ni changamoto
 
Hahah nyanya wanaita tungure, hiyo maji ya mferejini siku za mwanzo nilipata tabu sana naambiwa nenda mferejini halafu mimi natafuta mitaro.
 
Unafanya nini Zanzibar wewe au ndio umeenda kusimamia show ya terehe 27😂😂😂😂😂😂
 
sema wanavutia sana kuwasikiliza,wanavyovuta maneno.

kama mkazj wa dar akienda mikoani[emoji28][emoji28].

lazima wakushtukie.
 
Machangudoa walio Zanzibar ni WA bara na kwenda kufanyia ufuska Zanzibar. Hakuna changudoa mzanzibar.
Machangu wote pale zenji ni wabara ambao wamekwenda kutafuta kazi za mahotel wakakosa wakawa machangudoa au straight tangu wanatoka bara wamepanga kwenda kujiuza zenji.

Ndio maana pia imekuwa ngumu kupangishwa nyumba au chumba maana wanajulikana ni malaya tu
 
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
[emoji16][emoji16][emoji16]palinishinda

JESUS IS LORD[emoji120]
 
[emoji23][emoji23] Ni vituko vitupu

Siku hiyo nilikuwa Forodhani nauliza eti maeneo haya huwa wanapika vyakula kama wali au pilau! Yule dereva wa bodaboda aliyenipakia akaniambia huku sana sana wanapika bites na seafoods hasa mida ya jioni ila ukitaka vyakula kama wali harage (hapo kwenye harage nilicheka) au sembe (ugali wanaita sembe) labda utafute maeneo mengine!

Nikawaza kwani angesema tu wali maharage angekufa? Ukiwa mgeni kama haujawazoea unaweza hisi wanafanya makusudi!
Naomba nikurekebishe sio harage wanasema haragwe.
 
Duh nikisikia huko Zenji huwa nawaza kuwa ni sehemu ya kipekee sana.
Lafudhi kama hizo vyakula tofauti vyao, mavazi,
Kama hujui unaweza mtia dole kweli.
Vipi mkuu pisi zipo huko zinatafunika?
Watu wanaingia na pigo gani?
Hakuna kitu kigumu Kama kupiga pisi za kizenji. Yaani hapo unatakiwa uwe super star kwenye hiyo anga.
 
Kiukweli ni pazuri na pa kipekee sana asikuambie mtu!

Kuhusu pisi sijui mkuu mimi ni KE ila kuhusu lafudhi na lugha yao kwa sisi wabara tulivyo na vichwa vibovu huwa tunaishia kushangaa na kucheka wanavyoongea vile maana sisi tunaona kama matusi kumbe wenzetu kule kwao hayo maneno ni ya kawaida tu!
Usiombe uende huko vinijini, wakiongea unaweza usiam ilie kitu[emoji23]
 
Back
Top Bottom