Zanzibar sio kisiwa cha Waarabu, ni kisiwa cha watu weusi tena walikuwepo tangu mwaka 18KK, Waarabu waliingia Zanzibar pamoja na maeneo mengine ya mwambao wa Afrika Mashariki kwenye miaka ya 1600s, kipindi hicho Wareno chini ya Vasco Da Gama Kwenye mwaka 1499 tayari walikuwa wameshazunguka bara la Afrika, na kuweka makazi yao kwenye baadhi ya maeneo ya Zanzibar Kilwa na kuyatawala maeneo hayo. Watu weusi waliokuwepo Zanzibar walimuomba msaada Mwarabu kwa lengo la kuwaondoa Wareno na kwa hilo walifanikiwa. Baadhi ya ushahidi wa majengo ya wareno ni pamoja na Ngome Kongwe (Zanzibar). Lakini pia Mwarabu baada ya kutoa msaada nae alivutiwa na maeneo hayo ndipo Sultan Sayyid Said wa Oman akahamisha makaazi yake kutoka Oman na kuhamia Zanzibar, Sultan wa kwanza kutawala Zanzibar alikuwa akiitwa Majid bin Said ambae ni mtoto wa Sultan Sayyid Said akaanzisha kilimo cha minazi na Karafuu. Watumwa waliochukuliwa kutoka Bara wengi wao walikuwa wakiuzwa nje ya Zanzibar na wachache waliobakia Zanzibar walitumikishwa kwenye hayo mashamba. Iweje useme Zanzibar ni kisiwa cha waarabu??