Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!
Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!
Utawasikia "
Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)
Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!
Huku Zanzibari;
- Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
- Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
- Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
- Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
- Pombe wanaita- moja moto moja baridi
- Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
- Shule huku zinaitwa skuli
- Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
1. Hakuna mzanzibari jina Ali akaita Arii hata siku moja.
2. Maamrisho yote ya dini mwanamke hatakiwi kupaza sauti yake. Ndio maana huwezi kumsemesha mwanamke tu njiani na akapaza sauti yake.
3. Round about inaitwa round about kama ilivyo, maana ya ikipinda ni kile kitendo cha gari kupinda kutoka kwenye round about na ukute baada ya round about kuna kituo.
4. Kuna tofauti baina ya sufuria na dishi na hayo yote yanatumika Zanzibar. Sufuria ni sufuria, ( basin) ndio linaitwa beseni au dishi.
5. Kisima kinaitwa kisima, ila ninyi wa huko bara ndio kwa kutokujua baadhi ya maneno ya kiswahili ndio hamuelewi hata hodhi mnaita kisima. Kisima cha kuvuta, ndio ni kisima cha kuvuta maji kwa kamba. Lipi geni hapo?
6. Pombe inaitwa pombe, labda kama huelewi maana ya moja moto moja baridi tafuta maana, ila ukweli pombe ni pombe acha uongo.
7. Acha uongo, chupi zinaitwa chupi kwa vile huelewi maana ya hafu ndio unapotosha, hafu maana yake ni gaguro muulize hata bibi yako atakujibu.
8. Kwa vile bara ilitawaliwa na Mjerumani ndio maana mmezoea kuita shule kwa vile imetokana na neno la kijerumani Zanzibar wanaita skuli inatokana na neno la Kiingereza School.
9. Ni kweli kabisa chepe koleo wanaita pauro au beleshi ni kiswahili hicho.
10. Hela inaitwa Pesa ni kwa sababu kiswahili kimechukua maneno ya kutoka katika mataifa mbali mbali. Neno
Pesa limetokana na neno la Kihindi
Paisa. Sasa hata ninyi mnaotumia
Hela imetokana na neno la Kijerumani
Heller.
Unawaona kama Wazanzibari hawajui kiswahili kumbe wewe ndio hujui Kiswahili.
Ukiachana na yote kila sehemu kuna mila, silka, tamaduni, desturi zake, hivyo usitake tamaduni zenu na mila zenu ndio zifuatwe na kila mtu au kila sehemu mnayoingia. Jifunze kuheshimu mila, silka, tamaduni, desturi, za wengine ili na za kwako ziheshimiwe. Na usilolijua jenga mazoea ya kuuliza, kwani kwani kuuliza si ujinga ila ni kutaka kujua.