Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Chupi inaitwa chupi (mitaani itaitwa KUFULI)
Hafu ni vazi la kizamani , Lipo kama sketi nyepesi hivi ,zamani wanawake wa kipwani walikuwa wakivaa hafu n'a sketi juu yake.
Round about inaitwa hivyo hivyo, ikipinda baada ya Kona. Sufuria ndogo Dishi ni sufuria kubwa, kisima kuna cha mashine na cha kamba (kutofautisha). Bomba la maji wanaita mfereji , shule wanaita skuli , chèpe pauro (sio Paulo).... Charles Hilary ana lafdhi ya kule, kalelewa na kukulia kule .... Mi naona wanaongea Sawa tu.... Au labda kwa kuwa ni mswahili wa kuzaliwa.... Ukienda Tanga / Mombasa wanalafudhi nyengineee, Mtwara / Lindi.... Kiswahili kikubwa (usisahau lahaja rasmi ya lugha ya Kiswahili ni Kiunguja mjini) Wasalimie Mchamba wima , Mwembe mchomeke .... Hongera kwa kufika Zanzibar. Kura mpe Serif na Lisu ....😁
Wewe unaongea unachokifahamu.
 
Hakuna tea hapo!.....
waulize wazanzibery kuna sehemu ni barabara inaitwa Kilima nyege
Kama sijakosea kabla hujafika Tanganyika International school ukiwa unaenda masaki kuna kamlima pale wanakaita kilima nyege.😅😅ukiwa unakimbiza gari halafu ukakapanda kwa speed basi unaeza hisia moyo umehama ukaenda kukaa sehemu ya kongosho au firigisi 😆😆
 
Huko ndio kwenye kiswahili sio kwenye mnakomix R na L
Yaani mtu hata R.I.P wanaandika L.I.P
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
Lahaulaaa!
 
Kabisa yani. Kule wanaweza wakakufanya ujione haujui kiswahili.
Kwasababu huko ndiko wanapoongea kiswahili, mixer lahaja, mixer krioli mixer isimu, mixer tamathali za semi. Sasa wasiojua kiswahili wataelewa vipi?!
 
Ni wazenji au wabara walio lowea zenji?
Sio wazenji, huwa wanatoka Bara na kwenda kufanya biashara Zenji. Maeneo yote ya Kaskazini Nungwi , Kiwengwa kote huko wapo. Na kuna wengine huwa wanakwenda kuuza nyuchi then wikiend wanarudi Bara.
 
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Watu wawili mwaweza kwenda hotel moja mkaagiza chakula kinachofanana na kiasi sawa lakini kila mmoja akachajiwa bei yake kulingana na anavyoonekana
 
-Hela zinatwa PESA

-Nyanya zinaitwa TUNGULE

-Watu watokao bara wote wanaitwa WANYAMWEZI

-Umeme huku haukatwi isipokuwa UNAZIMWA

-Mvua huku hainyeshi bali INAKUNYA

-Viazi vinaitwa MBATATA

-Daftari linaitwa BUKU

-Kalamu inaitwa PENI.....nk,nk,nk,

Tanganyika na Zanzibar ni nchi mbilitafauti,Lugha,mila,desturi na Utamaduni tafauti

If you don't know now you know

Fanya haraka uondoke Kabla hawaja Ku......
 
Watu wawili mwaweza kwenda hotel moja mkaagiza chakula kinachofanana na kiasi sawa lakini kila mmoja akachajiwa bei yake kulingana na anavyoonekana
Sio kweli, kwenye uaminifu na uadilifu Wazanzibari wapo vizuri. Hawafanyi upuuzi huo.
 
Yani we acha tu! Nilisikia eti aliyewahi kuwa Rais wa South Africa Thabo Mbeki ana mtoto wa kike anaitwa Sito Mbeki ila hiyo nahisi watu walizusha tu mitandaoni!
Wewe mdada nimecheka mpaka wenzangu hapa wananishangaa.
Huyo alitakiwa huko bongo awe addressed as Sito Thabo Mbeki.
 
Mkuu huo ndio ukweli,
Aslimia kubwa sanaa ya machangudoaa waliopo Zanzibar ni kutoka Bara.
Tatizo leo nyinyi watu wa bara munapenda kuyachukulia maneno munayo yasikia,
Na kuyamini kwa aslimia kubwa bila kufanya uchunguzi.
Naona humu munapigana uongo mwingi kuhusu Zanzibar yetu but hatupo kama munavyodhani.
Waambie hao umalaya asili yake ni bara
Na hao ni wabara wenzao
 
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!

1. Hakuna mzanzibari jina Ali akaita Arii hata siku moja.
2. Maamrisho yote ya dini mwanamke hatakiwi kupaza sauti yake. Ndio maana huwezi kumsemesha mwanamke tu njiani na akapaza sauti yake.
3. Round about inaitwa round about kama ilivyo, maana ya ikipinda ni kile kitendo cha gari kupinda kutoka kwenye round about na ukute baada ya round about kuna kituo.
4. Kuna tofauti baina ya sufuria na dishi na hayo yote yanatumika Zanzibar. Sufuria ni sufuria, ( basin) ndio linaitwa beseni au dishi.
5. Kisima kinaitwa kisima, ila ninyi wa huko bara ndio kwa kutokujua baadhi ya maneno ya kiswahili ndio hamuelewi hata hodhi mnaita kisima. Kisima cha kuvuta, ndio ni kisima cha kuvuta maji kwa kamba. Lipi geni hapo?
6. Pombe inaitwa pombe, labda kama huelewi maana ya moja moto moja baridi tafuta maana, ila ukweli pombe ni pombe acha uongo.
7. Acha uongo, chupi zinaitwa chupi kwa vile huelewi maana ya hafu ndio unapotosha, hafu maana yake ni gaguro muulize hata bibi yako atakujibu.
8. Kwa vile bara ilitawaliwa na Mjerumani ndio maana mmezoea kuita shule kwa vile imetokana na neno la kijerumani Zanzibar wanaita skuli inatokana na neno la Kiingereza School.
9. Ni kweli kabisa chepe koleo wanaita pauro au beleshi ni kiswahili hicho.
10. Hela inaitwa Pesa ni kwa sababu kiswahili kimechukua maneno ya kutoka katika mataifa mbali mbali. Neno Pesa limetokana na neno la Kihindi Paisa. Sasa hata ninyi mnaotumia Hela imetokana na neno la Kijerumani Heller.
Unawaona kama Wazanzibari hawajui kiswahili kumbe wewe ndio hujui Kiswahili.Ukiachana na yote kila sehemu kuna mila, silka, tamaduni, desturi zake, hivyo usitake tamaduni zenu na mila zenu ndio zifuatwe na kila mtu au kila sehemu mnayoingia. Jifunze kuheshimu mila, silka, tamaduni, desturi, za wengine ili na za kwako ziheshimiwe. Na usilolijua jenga mazoea ya kuuliza, kwani kwani kuuliza si ujinga ila ni kutaka kujua.
 
Back
Top Bottom