Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

kwahiyo umechukia sababu hajauliza!!!
Siwezi kuchukia ujinga, ila ni vizuri kama kitu hujui uliza. Mfano mzuri neno mchamba wimba, angalia kwenye post zake alivyolidadavua, je ndivyo ilivyokuwa hadi kupatikana kwa jina la eneo hilo?
 
Huwa natamani aje Rais wa kusema Muungano basi. Kila mtu arudi na akae kwao. Tuone nani ataumia Dadeki
Julius hakuwa chizi ndugu. Tukiwaacha kivyao eneo litageuka uarabuni fasta sana. Usitegemee kwamba watakufa njaa. Hayati Kuna jambo aliliona.
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi

Sio tia wanasema WEKA kama unashuka dule unasema konda niweke dole hata mimi mwanzoni nilipata shida sana naishi Dole.
 
Eti "wali harage"[emoji3][emoji3] hawa watu bhana na hiyo lafudhi yao sasa ni balaa.

Kufundisha wanasema kusomesha!

Utasikia "mwl Zuberi asomesha skuli gani"? Hapo anauliza mwl Zuberi anafundisha shule gani.
😂 😂
Rula wanaita mstari....wale watu hawafai kabisa...wanaweza kukuumiza kichwa kwa kitu kidogo.😂😂😂
 
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!

Uongo uliotukuka!!!!!
 
Sio wazenji, huwa wanatoka Bara na kwenda kufanya biashara Zenji. Maeneo yote ya Kaskazini Nungwi , Kiwengwa kote huko wapo. Na kuna wengine huwa wanakwenda kuuza nyuchi then wikiend wanarudi Bara.
Ina maana wa zenji hawafanyi ufuska si ndio? Basi hiyo ni nchi ya ahadi
 
Back
Top Bottom