Hukumu dhidi ya Tundu Lissu yadhihirisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Wakala wa CCM

Hukumu dhidi ya Tundu Lissu yadhihirisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Wakala wa CCM

Niliahidi wiki iliyopita kwamba nitaandika tena baada ya hukumu dhidi ya Tundu Lissu ambayo tayari ilikwishavuja hata kabla ya mashtaka kuandikwa.

Hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza rasmi kumfungia mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu kutojihusisha na kampeni kwa siku 7.

Wiki iliyopita niliandika hapa kwamba taarifa zilizokuwepo ni kwamba makubaliano ya CCM na Mkurugenzi wa Uchaguzi Charles Mahera ni kwamba Tundu Lissu azuiwe kwa siku 14 kufanya kampeni.Huenda baada ya taarifa hizi kuvuja ndiyo sababu ya kupunguza siku hizo na kuwa 7.

Angalau kilichojionyesha dhahiri kwa Sasa ni kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijifichi tena bali imeamua kukaa mstari wa mbele kupambana na Tundu Lissu na Chadema.

Kwa wiki nzima iliyopita Mkurugenzi wa NEC Charles Mahera amekuwa akijitokeza mbele ya wanahabari kumshsmbulia vikali Mgombea wa Chadema Tundu Lissu.

Mkurugenzi huyo wa NEC amefika mbali na kuanza kuijibia CCM hoja mbalimbali za kisiasa zinazotolewa dhidi yake na mgombea wa Chadema Tundu Lissu.Bila aibu na bila kupepesa macho Charles Mahera aliapa kushirikiana na Polisi kuishambulia Chadema na Mgombea wake Tundu Lissu kwa mabomu ya machozi na kupongeza kwa vurugu zile zilizofanyika kule Nyamongo dhidi ya Tundu Lissu.

Hukumu dhidi ya Tundu Lissu ni Utekelezaji wa maelekezo ya CCM na Charles Mahera kwa inayojiita Tume ya Maadili ya Uchaguzi isiyokuwa huru.

Tundu Lissu ameadhibiwa na Charles Mahera na genge lake bila hata kumpa Fursa ya kusikilizwa na wala kupelekewa mashtaka yanayomkabili.

Ni kichekesho Cha mwaka kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi yenye majaji wanaoheshimika kukubali Charles Mahera na genge lake kumhukumu mtu asiye na hatia bila hata kumpa Fursa ya kujitetea na Kisha kupima ule utetezi.

Wakati hayo yakifanyika Chama Cha Chadema kimeandika malalamiko matatu tofauti dhidi ya Mgombea wa CCM kukiuka Maadili na kanuni za Uchaguzi.Siyo tu kwamba mgombea huyo wa CCM hajaitwa kujitetea bali Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshindwa hata kutangaza hadharani kupokea malalamiko hayo.

Cha kufurahisha ni kwamba Watanzania si wajinga wanaelewa Sana na kufahamu kwamba adhabu ya kumfungia Tundu Lissu ni kumpunguzia kasi baada ya Mgombea anayeungwa mkono na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuelemewa kwa kila kona katika kampeni hizi.Hivyo ni kutafuta njia ya kumnusuru.

Kwa adhabu hii dhidi ya Tundu Lissu ni dhihirisho la wazi la uwakala wa Tume hii ya Taifa ya Uchaguzi kwa CCM.Anachoongea Hamphrey Polepole dhidi ya Chadema ndiyo hicho hicho anachoongea Mkurugenzi wa Tume Charles Mahera utadhani wamekaririshwa maneno.

Ziko hujuma nyingi zinazoratibiwa na CCM na wakala wao Charles Mahera dhidi ya Tundu Lissu na Chadema.Tutarajie makubwa zaidi ya haya katika wiki za lala salama za kampeni.

Nitaandika tena baada ya adhabu dhidi ya Tundu Lissu kumalizika tarehe 9/10
Tanzania hakuna Tume ya uchaguzi kuna Genge la ccm limejivika mamlaka ya kujiita Tume ya uchaguzi
 
Mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi

Lisu ana kiburi na hufanya kusudi

Tume imefanya vyema sana

Mamlaka nyingine nazo zinatakiwa kufanya kama tume (kuchukua hatua kali dhidi ya mgombea na penye ulazima kwa chama kizima)
Tume inafanya vyema sana kwa vigezo vyako vya kijinga kama wao? au una maana ipi?
 
Tume ya ccm italaaniwa sana endapo watathubutu kuingiaza ccm ikulu kinyume cha kura za watanzania
 
Tayari tume imekataliwa na idadi kubwa ya walipa kodi iweje tume wanaendelea kulipwa mishahara kutokana na kodi za wananchi ambao hawaitaki hiyo Tume? haya ni matumizi mabaya ya madaraka na pesa za umma
 
Kesho mkutano unafanyika wapi?
Adhabu unayosemea ni ipi wakati alishiikataa na haitambui. Kesho jumapili watu wake wa logistic za kampeni wameshaandaa mkutano tatizo liko wapi tena? au na wewe ni bendera fuata upepo
 
Kesho mkutano unafanyika wapi?
Mkutano wa kesho utawachambua viongozi wote wa Tume, kila mmoja ataanikwa mapungufu yake kwa uwazi mkubwa wataelezewa mabaya yao yote ambayo walidhani ni siri yao hakuna anayeyajua
 
Kesho mkutano unafanyika wapi?
Wanaangalia ratiba yake inamwelekeza kuwa wapi. Juzi alishautangazia ulimwengu na umma kuwa maamuzi ya adhabu aliyopewa ni batili na kampeni zake ziko pale pale. Yangu macho, nazi kushindana na jiwe
 
Si alisema anawafuasi ?,andamaneni kupinga adhabu hiyo kuliko kutumia muda mwingi kupotosha ,patheti

Unatamani kuona machafuko???? Usidhani watu waoga ndg, ni BUSARA tu za viongozi wa upinzani, people are tired mman!!!!
 
Hiyo adhabu haikubaliki na Hilo genge la maharamia wa CCM walioficha kwenye mgongo wa tume dawa yao inachemka.

Soon watalia kilio cha mbwa Koko.
 
Lisu piga kelele Tume ya ccm wasilipwe mishahara tokea Hazina kwenye pesa za walipa kodi, wambie Tume wakadai mishahara yao ccm kwa mwajili wao
 
Back
Top Bottom