Hapana, kesi ipo kwakuwa ni kweli alichosokisema wamekifanya. Kama angekuwa amesema maneno matupu tu basi bila matendo hata mm ningeungana na wewe kuwa maji moto hayachomi nyumba na maneno hayavunji mfupa. Makosa yapo kweli ila unachosema wewe ni matundu kwenye sheria ya kuthibitisha. Lakini kila sheria, kila Katiba, kila tamthilia na kila movie lazima mwisho wake iishie kwa maslahi kwa umma. Yaani hakuna movie duniani itakayoruhusiwa kuuzwa na kuchezwa itakayoidhia majambazi yameshinda.
Kosa walilofanya ni kuharibu mali za taifa kwa maslahi yao. Yaani wameharibu mali za watu wengi wakiwemo watoto, wazee na walemavu ambao hawana nguvu za kujitetemea bali maslahi yao yanategemea nguvu ya mahakama, bunge, serikali, taasisi na watu wengine kuwatetea haki na maslahi yao.
Mali ya umma hata kama akiwa mnyama kama twiga ana haki kubwa mbele ya haki ya mtu mmoja au kakundi, lazima alindwe na sheria, serekali na bunge kwa gharama zote kwaajili ya maslahi ya umma.
Mali zilizochomwa, watu waliokatwa vidole, watu waliokosa usafiri wa mwendokakasi ulioharibiwa, watu walipoteza haki kwa nyaraka zao kuchomwa kwenye serikalo za mitaa, polisi waliouliwa, watu waliochomewa sheli, magari na biashara zao kama Shishi food nao pia wanaisubiri hii kesi itatoa hukumu gani. Mali zile hazikuwa za Samia bali zilikiwa zetu mimi na wewe na walioko matumboni.