Amani na utulivu ni sera kamili ya CCM. Chadema ni watanzania kama watanzania wengine walio chini ya Katiba ya 1977. Sera hii imeifanya tz haikuzalisha wakimbizi wengi kwenda nchi nyingine hata za ulaya na marekani. Mtanzania ambae yuko Marekani au Ulaya anatamani kurudi Tz fasta. Wale waliowahi kuishi huko wananielewa nisemacho.
Hivyo, usishangae kusikia sauti za maridhiano zikisikika kutoka miongoni mwa wanaCCM. Hata hivyo, CCM inaweza kutawala kwa amani kabisa hata bila maridhiano kwakuwa wananchi wa kawaida hawana tatizo, wanaishi mitaani, maofisini, mashambani, kwenye madaladala, maofisini, kwenye baa, viwanja vya mpira na kwenye matamasha kana kwamba hakuna kilichotokea.