Hukumu kesi ya Lissu iwe kinga na zindiko

Ya Oct29 yana namna yake mpya yataletwa kwa ushahidi wake mpya kabisa, brand new. Uchunguzi bado unaendelea.
Uchunguzi unaofanywa kwa tume ya muhalifu namba moja! Utakuwa ni mjinga kusema uchunguzi unaendelea watu wauaji wanatamba tu.
 
Samia ndio mtuhumiwa namba moja kwenye hili. Ni suala la muda tu.
 
Nikuambie kitu, mngemvizia Lisu siku hiyo ya Mo29 aandamane mtaani ndio hicho unachosema labda kingekuwa na uzito. Sasa hakuwepo mtaani. Sasa Tuipe muda mahakama ifafanue, tutarejea kwenye hili
Inakubidi ujifundishe vitu vingi ili uwe na general knowlexge.

Wafuatao wote wana makosa katika kutenda kosa.
1. Aliyepanga mchongo wa uhalifu
2. Aliyepembelemba namna ya kutenda kosa
3. Aliyetekeleza uhalifu
4. Mnufaika wa uhalifu

Hawa wote wana makosa. Sio lazima uonekane eneo la tukio ndio uwe umehusika. Kinachotakiwa ni ushahidi wa kukuunganisha na watekelezaji wa uhalifu.
 
Ila ukiiba uchaguzi na kutangazwa kwa kura za uongo uko sahihi kwababu wewe ni rais una kinga ya kutoshitakiwa kwa uovu.
 
Ila rais aliyeagiza jeshi lijiandae kwa uchaguzi yeye yuko sahihi. Kama mnadhani rais atakuwa salama kwenye hili maana yuko juu ya sheria, basi mnajidangaya. Ni sula la muda tu, mhalifu sahihi atafahamika.
 
Ila rais aliyeagiza jeshi lijiandae kwa uchaguzi yeye yuko sahihi. Kama mnadhani rais atakuwa salama kwenye hili maana yuko juu ya sheria, basi mnajidangaya. Ni sula la muda tu, mhalifu sahihi atafahamika.
Yaani uchome miundombinu halafu uachwe uishi, wewe nani? Uchome mali za watu binafsi halafu uachwe tu wewe ni nani, ukate watu vidole halafu serikali ikenue tu hiyo serkali au uharo.

Kama umekasirika sana ni vema kuning'inia kwenye korodani za mzee wako badala ya kwenda kukata vidole vya wengine
 
Mkuu ngoja nikupe mwanga katika mzigo walioubeba Majaji...

Hii kesi ni ngumu kuliko unavyofikiri...

Hukumu itakayotengenezwa inatengeneza Sheria Mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwepo Tanzania, pengine na Duniani

Tuseme Majaji waseme ..kuvuruga Uchaguzi ni Uhaini, Kuzuia Uchaguzi ni Uhaini, Kukinukisha ni Uhaini na Kuhamasisha Uasi ni Uhaini...
Unajua matokeo yake ?

Tume ya Uchaguzi na Sheria zake zitajaa neno Uhaini Kila section...

Mfano wasimamizi wa Uchaguzi au Polisi wakivuruga mwenendo wa Uchaguzi uwe mdogo au mkubwa tayari ni Uhaini

Mkurugenzi akikimbia kumuapisha wakala..anakuwa amevuruga taratibu za Uchaguzi...anakuwa ametenda uhaini

Ukimkamata mtu anaweka kura bandia..anavuruga Uchaguzi..hivyo ametenda kosa la uhaini..

Kwa hiyo tambua kwamba process za Uchaguzi zitakuwa zinabanana na UHAINI...itakuwa ni Sheria ya aina yake Duniani...
Tusubiri hukumu...lakini nakuhakikishia kesi hii ni ngumu sana kuliko unavyofikiri... Huko ndani kunawaka moto....
Ina maana mtu akienguliwa kwa makosa...mtumishi wa Tume atakuwa amefanya kosa la kuvuruga Uchaguzi...na Sheria Mpya itabidi itumike ambayo ni uhaini
 
Naelewa ugumu ulioko kwa majaji. Hata hivyo, dhambi ambayo itakuwa ndogo (the least evil) kwao ni kuangalia maslahi ya umma kwanza (majority well-fair).

Unaposema unakwenda kuuvuruga uchaguzi ni sawa na tangazo la kwenda kuvuruga zoezi la kikatiba la kila baada ya miaka 5 ambalo ndilo linalompata Rais wa Kikatiba wa nchi. Kama ukifanikiwa kuuvuga usifanyike uchaguzi kabisa maana yake Katiba imevunjwa, pili nchi itakosa Rais halali wa Kikatiba ambalo ni kosa pia. Hata Katiba yetu nadhani haina ibara inayoelezea hali itakuwaje kama uchaguzi hautafanyika kwasababu kundi la watu limeuzuia.

Sasa sijui mahakama itahuku nini, dhamira tu ya Lissu ya kutaka kuvuruga uchaguzi au nini?. Hata hivyo, chadema wenyewe wamethibitisha kuwa kuruga uchaguzi ulikuwa ni mpango wa chadema kama chama na sio Lissu peke yake. Hata Heche na Mnyika na viongozi wengine wa chama walisikika wakiendelea na msimamo huo hata baada ya Lissu kukamatwa.
 
Hakuna kesi pale zaidi ya maigizo, nitashangaa sana Kama majaji hawataipiga chini na kumwachia Lisu 💯
 
Mkuu, Uchaguzi usipofanyika... Rais aliyepo madarakani anaendelea na majukumu...
Nakupa mfano... Kipindi Cha Uchaguzi ikitokea mgombea Urais akafariki... Basi jua Uchaguzi utasogezwa mbele hata miezi mitatu..

Pia katika udharura Uchaguzi unaweza kusogezwa mbele.. sio lazima kwamba ni miaka mitano tuu..
 
Hakuna kesi pale zaidi ya maigizo, nitashangaa sana Kama majaji hawataipiga chini na kumwachia Lisu 💯
Hapana, kesi ipo kwakuwa ni kweli alichosokisema wamekifanya. Kama angekuwa amesema maneno matupu tu basi bila matendo hata mm ningeungana na wewe kuwa maji moto hayachomi nyumba na maneno hayavunji mfupa. Makosa yapo kweli ila unachosema wewe ni matundu kwenye sheria ya kuthibitisha. Lakini kila sheria, kila Katiba, kila tamthilia na kila movie lazima mwisho wake iishie kwa maslahi kwa umma. Yaani hakuna movie duniani itakayoruhusiwa kuuzwa na kuchezwa itakayoidhia majambazi yameshinda.

Kosa walilofanya ni kuharibu mali za taifa kwa maslahi yao. Yaani wameharibu mali za watu wengi wakiwemo watoto, wazee na walemavu ambao hawana nguvu za kujitetemea bali maslahi yao yanategemea nguvu ya mahakama, bunge, serikali, taasisi na watu wengine kuwatetea haki na maslahi yao.

Mali ya umma hata kama akiwa mnyama kama twiga ana haki kubwa mbele ya haki ya mtu mmoja au kakundi, lazima alindwe na sheria, serekali na bunge kwa gharama zote kwaajili ya maslahi ya umma.

Mali zilizochomwa, watu waliokatwa vidole, watu waliokosa usafiri wa mwendokakasi ulioharibiwa, watu walipoteza haki kwa nyaraka zao kuchomwa kwenye serikalo za mitaa, polisi waliouliwa, watu waliochomewa sheli, magari na biashara zao kama Shishi food nao pia wanaisubiri hii kesi itatoa hukumu gani. Mali zile hazikuwa za Samia bali zilikiwa zetu mimi na wewe na walioko matumboni.
 
Unaongelea ibara gani ya Katiba?

Sanasana nionavyo mimi Majaji wanaweza kumuachia Lissu lakini wakakifuta/kukisimamisha chama kwasababu ushahidi wote wa mshitakiwa umeonyesha ulikuwa ni msimamo wa chama. Yaani hata ukimnyonga Lissu chama kitaendelea na msimamo wake uleule wa kuasi, kukinukisha, kuuvuruga uchaguzi vibaya sana, kuchoma miundombinu na kukata watu vidole. Kundi la kigaidi badala ya chama cha siasa. Yaani hata maneno aliyoyasema Lissu sio yake bali yalikuwa ya chama kama vile mashahidi wa Lissu walivyothibitisha.
 
Huna akili👎🤮
 
Mahakama hii haiangalii uzito wa ushahidi wala kuaminika kwake' Jaji Ndunguru
 
HUkumu ya kesi hii ni mtihani kwa majaji dhidi ya Taifa na wananchi mmojammoja kwakuwa itatumika kuhukumu watu
Hivi mpaka unaoonyesha ukiuvuka unakuwa umeingilia mwenendo wa kesi unachorwaje?
 
Wapi alisema mkachome vitu au kuuana? Kuna sehemu yoyote Lissu alitoa maneno kuwa polisi waue raia? Kuna sehemu alisema watu wachome vitu?

Yeye aligusia uchaguzi ambao kwa mujibu wa tume ni uchaguzi uliovunja rekodi ya watu kupiga kura na haijawahi kutokea. Sasa huo uliovurugika ni upi? Au mlipika data enyi mahayawani?
 
Lissu yupo gerezani tangia mwezi wa nne. Chama kilifungiwa tangia mwezi wa tano. Uliona wapi Chadema kama chama ikiongoza watu kwenda mtaani kuchoma na kuua? Mjinyee wenyewe lawama muwapi wengine.

Mlijichanganya kujiona mnajua kila kitu na kuwa mnaweza kufanya lolote. Na mkijichanganya tena ndiyo mtaondoka kabisa mapema iwezekanavyo hilo wekeni akilini.
 
Huna akili👎🤮
Wewe ni mwehu!! Yaani useme kama vile na mfanye kama vile halafu kusiwe na consequencies kwako. Nchi ya mama yako hiyo?

Yaani Jaji ahukumu kuwa hata yeye hakuona chochote kibaya kwa Lissu na chadema wakati nchi imeungua moto, watu hawana vidole vyao mpaka sasa na mwendokasi haufanyikazi hadi sasa!!!! Heeeeeee!! Hebu ajaribu aone!!

Mahakama inaweza kukosa kosa la Lissu peke yake lakini haiwezi kukosa kosa la chadema la kuwa na msimamo alioutangaza Lissu, kuitisha mkutano na kualika waandishi wa habari ili msimamo wa kuzuia uchaguzi na kuasi na kukinukisha uwafikie watu wengi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…