Hukumu ya kifo Kwa vijana wa Kuluna Gang DRC iwe fundisho Kwa panya road

Hukumu ya kifo Kwa vijana wa Kuluna Gang DRC iwe fundisho Kwa panya road

Je chanzo cha hao vijana kua wezi na wauwaji ni kipi?

Vijana hao wakisha uliwa itakua ndio solution? Au it's the matter of time only kisha watakuja kuibuka wengine coz bado source ya tatizo itakua ipo pale pale?

Kama hukumu imetolewa na Mahakama hilo wala silipingi na wala halina mjadala.
Kongo wanaishi kibabe sababu ya vita, wana ardhi nzuri ya kustawisha mazao ila ukilima yakifikia kuvunwa wanajeshi wanakuja kuvuna na huna cha kuwafanya..!!!

Kongo ukivusha magendo mwanajeshi ndo anakusindikiza kikubwa mpunga 😹😹

Hao watoto jirani bora ukutane na simba sio hao, wanaua na kubaka.!!
 
Hao jamaa wamehukumiwa ila mpaka Sasa bado hawajauwawa nahaijathibitishwa zile.clip zamaneneza ni ile ajali ya meli iliyozama ziwa kivu naile clip yawasimali wakiuwawa kwarisasi. Lkini haijafahamika
 
Wezi wa kalamu ambao wakiandika tarakimu wanaweza kukomba bilioni kadhaa na kusababisha wagonjwa kufa hospitali kwa kukosa matibabu, vipimo kwa kutumia vifaa tiba vya MRI, TScan Ultra Sound Xray n.k wakafariki dunia kutokana na mafisadi wanaotumia wizi wa kalamu katika ofisi za serikali, mashirika ya umma.

Mafisadi hawa wenye vitambi na suti wala rushwa na wezi wakubwa nao washugulikiwe
 
Huko DRC vijana wahuni wa mtaani, wanaotishia amani Kwa kuvamia makazi na kuuwa raia mjini Kinshasa, wamehukumiwa adhabu ya kifo

Waziri wa sheria bwana Mutamba, ambaye amekuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii huko Kinshasa aliamuru vijana hao zaidi ya 200 kuuwawa na adhabu imetekelezwa

Watu ambao wamewahi kufika Kinshasa wamesema hakuna haja ya kuwahurumia, maana Kuluna Gang ni hatari sana DRC

Wakazi wa Kinshasa wanampongeza sana waziri Mutamba Kwa hukumu yake hiyo

Marekani na mataifa makubwa yamekaa kimya na kuonyesha kuunga mkono mauaji hayo ya Kuluna gang

Hapa kwetu Panya road na wadudu tunaowalea, nadhani tupige Congo
Hawa wahuni wanaweza baadae kuja kuwa kama Kuluna gang huko DRC
Mbona hawajawahukumu wahuni wanaojiita M23 ?
 
Ndo maana Africa hatuendelei ko mpaka mataifa makubwa yatoe comment
 
Mnaowatetea kuluna ni wapumbavu kabisa. Wale sio binadamu wa kuonea huruma imagine wanakata matumbo ya mama wajawazito wanachinja watu kuwatoboa macho gang raping wanavamia makazi kufunga mitaa kupora na kuuwa watu nenda Kinshasa uone huyo waziri anavyosifiwa Kinshasa ilikuwa haikaliki panya road wetu wanasubiri kwa ukatili wa Hawa wapumbavu.
 
Ukweli mchungu Sana ni kwamba hao vijana (siyo watoto) baadhi yao walifanya uhalifu mbaya sana kupita kiasi, hivyo wanastahili kupata adhabu kali ili iwe fundisho kwao na kwa Watu wengine katika Jamii. Isipokuwa Hukumu hiyo ya kifo imetolewa kiholela kwa Vijana hao, taratibu zote kabisa za kisheria hazikufuatwa katika kuwatia hatiani. Hivyo,wapo baadhi ya vijana wameonewa, hakustahili kuhukumiwa adhabu ya kifo, ila wapo baadhi ya vijana hao kweli kabisa wanastahili kupata adhabu kali ya kuuawa kutokana na makosa yao waliyotenda.
Kutokana na kuwepo kwa mkanganyiko huu mkubwa sana katika mchakato mzima wa kuwatia hatiani, na kutokana na sababu ya umri wao kuwa bado vijana wadogo(wengi wao), Mimi binafsi naona kama adhabu nzuri zaidi kwao ni kuwafunga vifungo vya muda mrefu gerezani badala ya kuwanyonga. Wabadilishiwe adhabu na kufungwa gerezani kwa mfano wafungwe miaka hata kumi, hii itakuwa fundisho tosha kabisa kwao.
Kifungo tena? Yan warudi wakiwa wamefuzu zaidi hapana mkuu
 
Duniani kote watoto wanalindwa why sababu they're vulnerable and naive, they're controlled by external forces, kama walikuwa wakora wao kama taifa na lina watu wazima wengi kuliko watoto, watoto hao ni zao la watu wazima ovyo. Tegemea huyo kiongozi kulipa huo udharimu wa kumwaga hiyo damu kama sio leo basi ni kesho.
Hao kuluna gang ni watoto?
 
Wanaingia kitaa wanafyeka watu shingo kama kuku.....Merci Mingi Pilato ya Kinshasa!!
 
Wakongo wanasema hao watoto ni wa madereva wa transit kutoka Tanzania 😹

Walimkamata dereva walimuingilia mtungo, unaambiwa hao watoto wanabaka mchana kweupe na watu wanashuhudia na polisi wanaona… ni haki yao kunyongwa
Kubaka tu?!

Mimi nikafikiri mauaji na kupora mali.
 
Back
Top Bottom