Mfumo wa dhulma unakwisha sasa.
Mbowe hatofungwa mana mashahidi upande wa serikali wameonekana walikua na nia ovu tu ya kutaka kumkomesha Mbowe kisiasa .
Majaji wanaojielewa dunia nzima hua hawapindishi haki.
Awamu ya mama samia Majaji wanaifurahiya mana inawapa nafasi kubwa ya kwenda Peponi.
Jaji ukivunja haki ya mtu ni dhambi kubwa sana kwa Mungu.
Awamu ya tano ilipotosha haki kila mahali.
Majaji walikua na wakati mgumu sana kusimamia haki.
Kuna Jaji alitoa hukumu ya ajabu kesi ya kikatiba yenye ushahidi kabisa kuhusu wakurugenzi kusimamia uchaguzi.
Jaji anasimama badala ya Mungu kuhukumu wanadamu humu duniani?
Hivyo Jaji hapaswi kutoka nje ya haki inayotokana sheria na ushahidi unaotolewa.
Mbowe sio Gaidi na hakuna ushahidi uliotolewa unaomuunganisha mbowe na kitendo chochote cha ugaidi hapa Tanzania na dunia nzima.
Na ikitokea Mbowe akafungwa kwa kuonewa ili kuwafurahisha wanadamu hasa wale wala rushwa waliombambikiza kesi basi ujue kuwa bado kitambo kidogo kikombe cha hasira ya Mungu kitajaa kwa taifa hili.
Hakuna nchi inayoombaga mabalaa lakini yanatokeaga tu kama kimbunga.
CCM kwa sasa haina nguvu ya ushawishi pamoja na kukalia vyombo vya dola na mapesa na kila aina ya rasilimali. Hivyo wakubali tu kuwa mbinu aliyotumia Sabaya na waliomtuma ilikua mbinu Mbaya na ovu sana ,haifai kabisa kutumika kwenye siasa ndani ya nchi moja.
CCM mjipange tu kushindana kwa haki bila dhulma na kuua watu. Sabaya alikisaidia Chama lakini sio madhumuni ya CCM hayo kama chama cha siasa.
Huenda Aliyemtuma Sabaya alikua na chuki na watu wa kabila Fulani lakini sio madhumumi ya Chama hayo.
Huenda wakati huo walipanga watu wa mrengo Fulani kuanzia kwenye vyombo vya dola ili kuwakomesha wapinzani lakini sio madhumuni ya nchi yetu kuingia kwenye demokrasia ya vyama vingi.
Mama Samia naamini kuwa anamuogopa Mwenyezi Mungu na anailinda katiba ya nchi.
Mana kwa nchi yetu ukitoka Mungu anayefuata ni Rais . Kwa hiyo Rais asiposimamia haki basi anajifanya kuwa mungu yeye. Akiwafumbia macho majaji wanaopotosha haki basi Mungu naye atamkataa.
Haki itatendeka kwa Mbowe kama ushahidi ulivyojieleza wenyewe.Mbowe sio gaidi.
Waliombambikiza kesi watapata fundisho kuwa wafuate utaratibu wakati wa kutekeleza majukumu.
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app