Humphrey Polepole: Kazi ya shule ya uongozi itawafurahisha wenye mamlaka, ukiona unataka kuruka na mimi kwenye mtandao ujue wewe sio kiongozi

Humphrey Polepole: Kazi ya shule ya uongozi itawafurahisha wenye mamlaka, ukiona unataka kuruka na mimi kwenye mtandao ujue wewe sio kiongozi

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mh. Humphrey Polepole amesema hayo kupitia kipindi cha Shule ya Uongozi ambapo alisema ni kipindi kinachofanya kazi ya kusema ukweli, jambo ambalo linaendana na kauli maarufu ya Chama Cha Mapinduzi inayosema "Nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko".

Amesema wale watakaotaka kuruka na yeye kwenye mtandao wajue kwamba sio viongozi na wala hawapo katika mamlaka, kwa sababu yeye anafanya kazi nzuri ya kusema ukweli.

Sawa Ila Mimi ninavyo fahamu hapa Kuna polepole watatu
1. Yule polepole kipenzi Cha watanzania wa tume ya katiba mpya. (Warioba)
2. Yule polepole wa mwenda zake alieikana katiba.
3. Na huyu wa sasa mwalimu wa shule ya viongozi.
Hawa polepole watatu wakikutana watapigana mpaka watoane roho,Bora tu tumuombee wasikutane kabisa.
 
Eti ukweli!

Ila tusimshangae sana madaraka na kuwa na power kutamu sana asikwambie mtu.

We fikiria mwezi wa pili mwaka huu alikuwa na uwezo wa kumpigia simu waziri yeyote na kumuuliza kwanini hufanyi hiki na kile na waziri anaufyata.

Leo hata jokate ana nguvu kuliko polepole.

Lazima uchanganyikiwe tu na kujifanya msema ukweli kumbe mnafki tu mmoja.
 
Wala kipindi hakina shida.
ila shida ni huyo muendesha kipindi kwanini hakuanzisha kipindi ndani ya miaka 6 iliyopita?
kwanini iwe sasa?
 
Sawa Ila Mimi ninavyo fahamu hapa Kuna polepole watatu
1. Yule polepole kipenzi Cha watanzania wa tume ya katiba mpya. (Warioba)
2. Yule polepole wa mwenda zake alieikana katiba.
3. Na huyu wa sasa mwalimu wa shule ya viongozi.
Hawa polepole watatu wakikutana watapigana mpaka watoane roho,Bora tu tumuombee wasikutane kabisa.
Nita tafuta hatma ya yule wa mwendazake kwanza😂
 
mbona sehem nyingine TISS wanaletaga figisu hadi jambo linashindikana kwann washindwe kwa haka kakipindi??Au wanamkono wao hapo..wizara ya habari na Tcra nao wapo kimya.Mama anahujumiwaaaaaaaaaaaaaa
 
Aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mh. Humphrey Polepole amesema hayo kupitia kipindi cha Shule ya Uongozi ambapo alisema ni kipindi kinachofanya kazi ya kusema ukweli, jambo ambalo linaendana na kauli maarufu ya Chama Cha Mapinduzi inayosema "Nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko". Amesema wale watakaotaka kuruka na yeye kwenye mtandao wajue kwamba sio viongozi na wala hawapo katika mamlaka, kwa sababu yeye anafanya kazi nzuri ya kusema ukweli.
View attachment 1970501
Ameshaanza kuchanganya Dini na Siasa naona hapao anapiga siasa anapiga na Mathayo 🤣🤣🤣
 
mbona sehem nyingine TISS wanaletaga figisu hadi jambo linashindikana kwann washindwe kwa haka kakipindi??Au wanamkono wao hapo..wizara ya habari na Tcra nao wapo kimya.Mama anahujumiwaaaaaaaaaaaaaa
Kwakuwa Polepole ni ccm na wao ni ccm
 
Back
Top Bottom