Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Humphrey Polepole amesema kuwa
"Mambo ya Machifu yanatusaidia nini kama taifa?nasema jambo hili sio jema,naliona linadhoofisha Utanzania wetu,likiendelea bila kukemewa litaibua tuliyoyazika ya hisia za ukabila, usisi na uwao, Mwalimu Nyerere aliona mbali kukataa haya mambo kwani yataligawa taifa"
"Yapo maeneo uchifu ulishaondoka,haupo. Tulishakubaliana uchifu ni ukoo wenu, mna kiongozi wa ukoo mnazungumza mambo yenu binafsi ya kifamilia leo serikali ikizungumzia uchifu hawa nao wataomba kiongozi wao (wa ukoo) atambulike na apate nafasi huko serikalini"
"Mwalimu Nyerere alikataa jambo hili (uchifu), lina faida gani. Uchifu unataka kutuibulia zile hisia kwamba tuna ukabila kama hakuna wazee wataliona hili jambo, basi mawe yataona"
"Nchi yetu ina wakristo na waislamu, ikitokea mvua imechelewa kiongozi wa serikali huwa anawaomba wakristo kanisani wakaombe na waislamu msikitini wakaombe mvue zinyeshe, lakini huwezi kusikia kiongozi wa serikali akiwaomba washirikina eti wafanye namna mvua inyeshe"
"Kwenye shughuli za serikali ushawahi kuona tunawaita wanaoabudu miti waje kuomba kabla ya shughuli? sasa uchifu wa nini?. Hawa machifu walishafutwa kisheria, tunapowarudisha tunapanda nini?"
"Nenda pale Kilimanjaro, utasema Mareale ndio chifu wao, hapana wako wengi. Kwa hiyo nao wafanye uchaguzi kisha waje kumpata chifu wao wa wote. Kweli tunaenda hivi katika maendeleo"