Humphrey Polepole, Musukuma na "Kakikundi" kao tunawatazama kwa makini sana!

Humphrey Polepole, Musukuma na "Kakikundi" kao tunawatazama kwa makini sana!

Shukrani mmewafanyia nini wasukuma pumbavu nyie,wasukuma wanaendelea na maisha yao kama kawaida bila kelele nyie tu mnajishtukia kwa unafiki wenu,mama hana ushawishi ni empty set
Atawashuhurikia ipasavyo, hili kukomesha chuki zenu
 
Nadhani uliwahi kuiona picha ya Polepole akimchungulia kwa umakini Mama Samia akimpiga jicho kama vile anataka kujipendekeza kwake, siku ile ya uapisho wa kwanza kabisa wa mawaziri.

Mpiga picha aliyelinasa lile tukio atakuwa ni wa kimataifa, kwani aliweza kuunasa unafiki ukisomeka machoni moja kwa moja machoni mwa watu.
Jamani acheni kumpaisha polepole.
Ni dhaifu hana impactiiiiii
 
Nadhani uelewa wako una tatizo. Mama kusimama kuwa mgombea wa CCM hilo halina tatizo kabisa na ni LAZIMA awe yeye! Mnachoshangaza wewe na wenzako wenye chuki na Hayati Dkt Magufuli ni kuendelea kumbeza Dkt Magufuli mkidhani mnaongeza kura za Mama Samia. Kumbuka kupigia kura na NEC ya chama chetu CCM ni tofauti na kura za NEC. Nyie kosa lenu kubwa ni kubeza kundi kubwa ambalo bado linaomboleza kifo cha Dkt Magufuli. Na mjue TISS na vyombo vya ulinzi na usalama vilifanya kazi kubwa sana chini ya Dkt Magufuli na Dkt Magufuli aliwapa kipaumbele sana ktk kuthibiti rushwa. Sasa ninyi mnapomdhihaki si tu vyombo vya ulinzi na usalama vinawaondolea mamlaka ya kutawala bali mnaviumiza kiroho kwa sababu wao ndiyo taasisi ya urais na siyo mtu. Akili zitawarejea 2025 mkiendelea na hizi propaganda zenu chafu.
Punguani vyombo vilikua vinaelekezwa kwenda kufanya dhuluma, kuiba,kuua,
Hata CDF hakufurahishwa na ushetani wa wakati ule sema amekaa mtu wa dini zaidi angeweza kumchomoa mshamba yule
 
Huyo magufuli aliye kuwa anawadanganya mchana halafu usiku anakopa? Hebu jiulize alikuta deni Tsh ngapi na akaliacha Tsh ngapi halafu uje useme hapa alikuwa hakopi au laa! kadanganya sana wajinga yule mzee
Bora aliyekopa akajenga barabara na madaraja, kuna watu walikopa zikaishia mifukoni mwao, RIP JPM.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
You are simply asleep…

Siku uki wake up ndio utamuelewa Polepole…

Tofauti ya sisi na hizo nchi za kimagharibi unazosema ni kwamba mabeberu wanazipenda nchi zao wameziendeleza….wewe nchi yako changa inajikongoja unamtegemea huyo beberu akutoe kwenye umaskini ndio maana unasiasa zisizofungamana na upande wowote, miaka yote ya uhuru na hizo siasa zako zimekufikisha wapi…mnazidi kushabikia watu waliopewa madaraka na kuprove failure kwa miaka yote tuliowaamini…CCM kilianzishwa na watu wazalendo na wenye uchungu na nchi ila it is very unfortunate kimekuwa abused na wachumia tumbo na weak people…We need an evolved human beings kuendesha hicho chama maana naona kinaendeshwa na the same minds zilizotuweka kwenye mess..wao nashauri wangekaa pembeni kabisa…zije akili mpya zinazojiamini…ushauri wao hauhitajiki tena we have the minds of our own…Mungu yupo pamoja nasi always…

Ukimwambia kiongozi abane matumizi gharama ni kubwa..vikao,semina,safari zisizozalazima tunawaumiza wananchi hakuelewi anakuita majina ya ajabu sijui diktekta…sasa wacha tule tozo mpaka akili ziamke..

Na mnukuu Raisi Mwinyi kwenye hotuba yake ya mazishi ya JPM…”kijana amefanya mengi kwa miaka mitatu yaliotushinda sisi miaka 40”….hujiulizi?! JPM sio malaika tofauti yake yeye ali wake up akapindua meza wachache sana walimuelewa ndio maana ikamuwia vigumu sana kuiendesha nchi ikawa km one man show..but he was so powerful alipambana kiume..narudia tena na tena..bado nchi hii ni changa inahitaji dikteta zaidi ya JPM…ili apush akili zilizolala tutoboe

Hizo theory ulizomezeshwa na cyllabus za wakoloni ukapata masters ya political science jitahidi utoke nje ya box uanze ku question mambo.. thank me later
Kama unataja akili kama za shetani mkuu uko sahihi,maana shetani mkuu aliweza kupiga chenga za kishetani na kufauli kuwa na himaya aloimiliki.
Kama jpm aliua, alipiga watu risasi,alihamishia mali chato, alileta ukabila,udini akaiba hela ktk akaunt za watu, akatenganisha koo, familia na ushenzi wote, I BEG TO BE WITH YOU, THE SUN OF LUCIPHER[emoji120]
 
Kwa hiyo tumerudi rasmi kwenye minyukano?! Mama weeee [emoji15]
 
Wafukuzeni tu Kama mna ubavu kuliko kila siku povu JF,mujumulisheni na Gwajiboy.
Halafu tutajua mizizi yenu ni mikoa ipi hasa.
 
Awali ya yote niseme nimezitama clips walizoachia masaa machache yaliyopita Humphrey Polepole na huyu Ndugu yetu "Darasa la saba" Joseph Kasheku Musukuma almaarufu King Musukuma!

Ukizitazama na kuzisikiliza kwa makini utagundua zote kwa pamoja zinafanana kwa maudhui japo zimetolewa na "Wahadhiri" wawili tofauti.

Kwanza, "Wahadhiri" wote wamejinasibu kwa kujitahidi sana kuchagua maneno ili kuonekana wanamheshimu Rais Samia na wanamuunga mkono ama yeye binafsi, Serikali yake ama Serikali ya CCM lakini wote ni WANAFIKI wakubwa sana!

Pili,wote wanataka waonekana wana ajenda ya kutetea masikini kama mtaji aliouacha "MWENDAZAKE"na ambao wanataka kutuonyesha kuwa Rais Samia haujali na ameamua kumsaliti "MWENDAZAKE"!

Tatu,"Wahadhiri" wote wamemshambulia sana Mheshimiwa Amos Gabriel Makala, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kama mtu wa hovyo, mtu ambaye hana maarifa , mtu ambaye alishashindwa maisha na Rais Samia amefanya makosa na kumpa Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam!

Kabla sijaenda mbele nizungumzie mambo mawili kwanza ili twende sawa.

Mosi, siungi mkono jinsi wamachinga pale vingunguti walivyofanyiwa baada ya kupewa mwezi mmoja, lakini siungi pia uwepo wa wamachinga kila mahali na kubembelezwa kwao. Wamachinga hawana impact yoyote ya maana katika uchumi wetu zaidi ya kutudidimiza kwa kuuwa uchumi wetu na kuvuruga miji yetu! Ni ujinga kwa mtu kama Mbunge badala ya kuibua mikakati na kuishauri Serikali namna ya kuja na miradi yenye tija kwa Taifa itakayowa-absorb wamachinga na kuwafanya wazalishaji wa kweli kwenye production chain.

Pili, huyu Amosi Gabriel Makala ni nani? Simjui sana ila najua elimu yake ni nzuri tu! Ana Masters( MBA) na pia ana CPA ( Certified Public Accountant), amewahi kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC), Mkuu wa mikoa kadhaa (Kilimanjaro,Mbeya,Katavi) kabla ya kuletwa Dar es Salaam. Amekuwa Mbunge na Naibu Waziri wa Habari.

Na niseme huyu ndo mtu ambaye kwa sasa naona alikuwa ame- qualify kuwa KATIBU MKUU WA CCM kama profile ingekuwa na maana yoyote ndani ya CCM!
Huyu ndo mtu ambaye Polepole kwa kujificha nyuma ya kichaka cha shule ya uongozi anamfundisha namna ya ku- deal na mamalishe wa masaki!

Musukuma yeye kutokana na uhafifu wa elimu yake (Darasa la Saba) hawezi kujificha kama Polepole ,amefunguka kuwa Mhe.Amosi Makala ana magenge ya Urais 2025!

Humphrey Polepole na Musukuma ni WANAFIKI sana, rejeeni mambo yao huko nyuma!
Polepole aliwahi kukana maelezo yake wakati wa mchakato wa katiba na mstakabali wa CCM katika uchaguzi huru na haki (Clip zipo humu)!

Musukuma wakati wa safari ya matumaini ya Lowasa alienda hadi uwanja wa Sheik Amri Abeid pale Arusha lakini baadaye alimgeuka na ndiye aliyevujisha "Habari" za Lowasa kujinyea Chato!
WANAFIKI sana watu hawa!!

Turudi kwa huyu Humphrey Polepole, najua amehitimu Masters ya DS ( Development Studies) hivi karibuni!
Kwenye clips zake alizotoa huitaji kuwa na elimu ya kutengeneza roketi (rocket science) kujua ana gubu na Rais Samia na Serikali yake baada ya kupigwa chini.
Hiki alichoki- hadhiri leo kwenye "Dependency theory"ni ujinga tu na kupinga safari ya Rais Samia kule Marekani (UNGA)!

Polepole tuambie Magufuli alikuta deni la Taifa ni kiasi gani na aliacha limefika kiasi gani?

Na kama alikopa basi atueleze Magufuli alikopa kwenye taasisi zipi?

Polepole acha gubu kwa Rais Samia na Serikali yake!
Sikubaliani na pointi zako zote.Nianze na ya kwanza; Sio kazi ya mbunge kuishauri serikali katika day to day activities. Kazi kubwa ya mbunge ni kuwatetea wananchi dhidi ya maamuzi yoyote yanayoonekana kutokuwa na faida kwa wananchi. Serikali ndio inatakiwa kutetea maamuzi yake na hatua mbali mbali inazozichukua.
Kwa ushauri wako katika pointi ya kwanza, unawapoteza wabunge wetu wawe kama mbunge aliyeshauri serikali kuja na tozo za kuwaumiza wananchi.
 
Sukuma gang mmechanganyikiwa. Mmebakiza kuporomosha matusi tu.

Kazi inaendelea kwa kasi zaidi. Sasa hivi tunakwenda kujenga madarasa ya sekondari ELFU KUMI NA TANO. Nani kama mama?
Mkijenga ni jambo jema sana,kila la heri kwa hilo,shida maneno mengi vitendo sifuri yaani kama January Makamba😂😂😂
 
Humprey polepole na Josephat ( mrundi) ni adui wakubwa wa serikali ya awamu ya sita: Hawa watu wanakutana wanapanga pamoja ni wasemaji wa kundi linalopinga serikali kwa kila jambo
 
Rais Samia ni dhaifu hawezi kuongoza nchi makini kama Tanzania. She falls below presidential standards.

Anafaa sana kuwa mwenyekiti wa NGO za akina mama au VICOBA/ VIKOBA.

Hili linchi lenye kila rasilimali halipaswi kuwa omba omba. Gesi, madini maliasili, wanyama, mbuga, makaa ya mawe, ardhi safi na kubwa, nguvu kazi ya kutosha, wasomi mahiri na mengine mengi.

Tanzanite, almasi, dhahabu, migodi mikubwa Africa. Kodi, Tozo sijui nini. Rasilimali kila kona.

Tulikuwa na Rais shupavu anaitwa John Pombe Magufuli alikuwa anatambua kwamba sisi sio watu wa viwango duni vya kujikomba komba kwa mabeberu na matapeli wa Ulaya.

Huyu Chief Hangaya ana miezi mitatu tu kashaanza kujibembeleza na kujibebisha kwa wazungu.

Yaani ni mwendo wa ukike kike tu. Mara mie jinsia yangu ya kike, mara maumbile yangu ya kike sijui yamefanyaje.
Jpm alifilisi nchi ndugu na kutufukakarisha tu. Daily nchi hii tajiri lakini watu wanazidi kuwa maskini na wala hajali kabisa. Ni kakpindi chake ndo hakuajiri kabisa na hakuongeza mishahara kabisa na hakutaka kusikia hilo halafu unasema nchi tajiri wakati watu wanazidi kuwa maskini. What a stupid stupendous
 
Humprey polepole na Josephat ( mrundi) ni adui wakubwa wa serikali ya awamu ya sita: Hawa watu wanakutana wanapanga pamoja ni wasemaji wa kundi linalopinga serikali kwa kila jambo
Polepole inatakiwa ashtakiwe kwa uhaini, ana Nia hovu na Nchi,

Serikali haraka inatakiwa imtie mkononi Polepole na msukuma, Wahaini hawa
 
Kuongoza nchi iliyo na idadi kubwa ya watu wajinga bhana nikazi Sana. Yani mtu kuwa na mitazamo tofauti tu tayari ni adui wa taifa?

Mleta mada akili zako nikama za kina mahita tu.

Spika wa bunge la Marekani alichana hutuba ya rais Trump na bado hakuchukuliwa Kama adui wa taifa, iweje leo watu kutoa mawazo yao na kuongea wanachokiamini wachukuliwe Kama maadui wa taifa.

Think beyond mkuu!!
 
Kuongoza nchi iliyo na idadi kubwa ya watu wajinga bhana nikazi Sana. Yani mtu kuwa na mitazamo tofauti tu tayari ni adui wa taifa?

Mleta mada akili zako nikama za kina mahita tu.

Spika wa bunge la Marekani alichana hutuba ya rais Trump na bado hakuchukuliwa Kama adui wa taifa, iweje leo watu kutoa mawazo yao na kuongea wanachokiamini wachukuliwe Kama maadui wa taifa.

Think beyond mkuu!!
Hao waimba mapambio wanataka kila mwananchi awe kasuku.
Hovyo kabisa
 
Hoja wanazo na pia naunga mkono haki ya kutoa maoni yao kwa uhuru na bila ya woga. Tuwapinge kwa woga.

Mimi nawachukia kwa unafiki wao tu. Ingalikuwa ni jambo linalowezekana, natamani katiba au sheria zetu ingekuwa zinakataza unafiki. Ni mojawapo ya matatizo makubwa zaidi yanayoturudisha nyuma kama nchi/taifa.
 
Back
Top Bottom