msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Humphrey polepole na King msukuma hakuna asiyejua kuwa nyie ni miongoni mwa waliokuwa wanufaika wakuu wa utawala wa hayati Magufuli.
Ni katika kipindi hicho ambapo vijana tulipokuwa tukihoji masuala ya ajira mnatukebehi kwa maneno yaliyojaa kejeli na dharau kubwa
Nakumbuka wakati humphrey polepole ukiwa bado ni katibu mwenezi ulipoulizwa kuhusu suala la ajira ulisema serikali haiwezi kufanya kazi ya kuajiri tu hivyo vijana wajiajiri hata kwa kulima matikiti na nyanya.
Jambo la kushangaza baada ya Rais Samia kuingia madarakani ukapokonywa ukatibu mwenezi badala ya kujiajiri kwenye kilimo cha matikiti kama ulivyohamasisha vijana, unafanya harakati za kumpinga mheshimiwa Rais kwa sababu ya uchu wako wa madaraka. Mbaya zaidi vijana wale wale uliowaambia wajiajiri kwenye kilimo cha nyanya na matikiti ndio hao hao unataka wakuunge mkono kwenye hizo harakati zako uchwara za kumpinga Rais Samia. Je, unafikiri hili litawezekana au unapoteza muda wako bure tu?
Tukirudi kwa King Msukuma, huyu mara zote amekuwa ni adui wa wasomi hakuna asiyejua. kipindi chote cha hayati magufuli, Msukuma alikuwa na kazi ya kutukana wasomi tu hasa vijana walipokuwa wakiiomba serikali iwaajiri.
Lakini juzi kwenye sakata la RC Makalla na machinga, Msukuma huyu huyu anayetukana na kudharau wasomi anatoka na kujifanya kana kwamba anawatetea vijana wenye digrii waliojiajiri kwenye umachinga. Hapa ndipo najiuliza, hii huruma anayoionyesha Msukuma kwa vijana imeanza lini?. Sio unafiki huu?. Mbona wakati wa magufuli hakuwatetea zaidi ya kuwatukana na kuwafedhehesha?..
Hata hivyo vijana wanajitambua, hivyo humphrey na king msukuma kama mnafikiri mnaweza kuwatumia vijana hawa hawa mliowadhalilisha kipindi cha awamu ya tano kama madaraja ya kufanikisha maslahi yenu binafsi ya uchu wa madaraka kwa kumkwamisha na kumfitinisha Rais Samia tambueni kwamba mnapoteza muda wenu bure kwani hakuna kijana mwenye akili timilifu atawaunga mkono. Hivyo basi, kubalini kwamba zama zenu za kula mema ya nchi zimeshapita, mwacheni Rais afanye kazi yake maana fitina zenu kwake hazitawafikisha popote.