Humphrey polepole na King msukuma figisu zenu za kumhujumu Rais Samia hazitawafikisha popote

Sasa hapa ndio ujiulizwe vizuri kwanini sasa na sio wakati ule...

Hakikisha unatengeneza hoja(majibu) zaidi ya moja arafu kwenye hizo hoja chagua hoja(jibu) moja iliyo sahihi zaidi, using'ang'anie upande mmoja.
Wakati ule alikuwa kwenye cheo hivyo asingeweza kukosoa kwa sababu siku zote mbwa mwenye mnofu mdomoni huwa hapigi kelele ila leo anakosoa na kubweka kwa sababu alinyang'anywa tonge mdomoni baada ya kupigwa chini kwenye ukatibu mwenezi.

Pili# polepole anasumbuliwa na superiority complex maana anajiona kuwa ndiye mtanzania pekee mwenye akili kuliko wengine na anafikiri amezaliwa kuwa kiongozi hadi kufa kwake

Kwa hoja hizo mbili utagundua He's fighting for his own political interests and not otherwise na njia pekee anayofikiri inaweza kumfanya atimize hayo malengo yake ni kuhakikisha Rais Samia anatoka madarakani ndo maana unaona anafanya anayoyafanya
 
Wewe ndio unataka kuwachonganisha Polepole na Msukuma kwa Mama. Hautafanikiwa! POLEPOLE NA MSUKUMA NI MAJEMBE YA CCM!!
 
Nchi ikijaa chawa ,kama ww hatuwezi kutoboa.Kwa kuwa tunaangalia uteuzi tu.
 
Kuwa bungeni ndio kunaonesha ubora wa mtu?! Hivi huko mashuleni mlienda somea ujinga !!!??
 
Kufitinisha!!!?
au wanatoa maoni yao......
kuwa mkubwa blaza inchi ya kidemkrasia hii...
watu wana haki ya kutoa maoni na mitazamo yao.......
Ama unataka kuwapangia cha kusema!!?
 
Katika vitu alivyoshangaza Polepole ni kukubali uteuzi wa ukuu wa wilaya, cheo ambacho alikuwa anakilaani kila apitapo, mnafiki sana jamaa
 
Kufitinisha!!!?
au wanatoa maoni yao......
kuwa mkubwa blaza inchi ya kidemkrasia hii...
watu wana haki ya kutoa maoni na mitazamo yao.......
Ama unataka kuwapangia cha kusema!!?
Kwanini awamu hii?

Mbona awamu ya 5 walikuwa kimya hatukusikia wakitoa hayo maoni zaidi ya kumsifia JPM hata alipokuwa akitenda maovu?

AU kwakuwa Samia ni mwanamke hivyo wanamdharau kwamba hawezi kuwafanya chochote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…