Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Kama ni kweli hafurahishwi na mjadala huu , awakamate waliouanzisha maana wanajulikana awafungulie mashtaka kwasababu wamepotosha umma..asituletee maigizo hapa.
 
ETI MJADALA KWANI NANI KASEMA TUNAJADILI HUO MJADALA....HAYO NI MATUMIZI MABAYA YA TAARIFA KUTOKA IKULU [HASHTAG]#msigwa[/HASHTAG]
 
Hakuna haja ya Kubadilisha muda wa miaka na awamu za viongozi wa kisiasa (kuanzia Rais , Wabunge, Madiwani, na wengine).

Zaidi, tunahitaji muendelezo thabiti wa mipango ya maendeleo inayoachwa na kiongozi wa awamu moja kwenda awamu nyingine.

Tanzania , siyo Rwanda, DR Congo , Burundi au Uganda.

Amalize muda wake akapumzike awe mshauri na siyo kuongezewa hata siku moja.

Rais , JPM 2015 hadi 2025.
 
Asitake kutuzuga, hatulali ng'o...tabia na matendo yake yanadhihirisha ana mpango wa kukaa Ikulu milele?
Nafiki tu.

- Hapo linataka siku likisema NIMELAZIMISHWA KUONGEZEWA MUDA, NIMESUKUMIZWA kuongeza MUDA msilishangae.
- Nchi ya Vi-Wonder
 
mimi kama katibu mkuu wa vijana jamii forums nina muombea kila siku kwa mungu apewe miaka mingine 26 kutokana nakazi anayo ifanya huyu rais wetu kipenzi cha mungu😉😉
 
Naunga mkono hoja asituletee ya kuongeza miaka mingine. Pamoja na hayo inaweza kuwa ni njia ya kupima upepo wa siasa na kuchochea moto zaidi ili miaka miwili ijayo aseme "nimefikiria sana na wananchi wengi wanasema niongeze miaka , na mimi siwezi kukataa kwa sababu nilianza na miradi mikubwa (SGR, Fly overs, kuhamia dodoma, stieglers gorge na kama hiyo) naomba muda miaka 7 nimalizie". Binafsi Naomba huo mpango uishie alipoishia kusema miaka 5 inatosha. Tutafanya uchaguzi mwaka 2020, atakayepita atakuwa Rais wetu na kuendeleza gurudumu la maendeleo.
 
uzushi siku zote ni kipito cha malumbano

let me wish good lucky
 
Siasa zetu zimeshakuwa za ajabu sana. Kiongozi anapoingia madarakani watu wanaanza kujadili atakapotoka nani ataingia!.Hiyo ilikuwa kwenye awamu ya nne. Sasa awamu ya tano hoja za ajabu ni kuongeza kipindi cha uraisi! Nadhani Raisi amefanya vema kuliweka wazi hili jambo hivyo taifa liendelee na ajenda za maendeleo.Hoja za kujadili walau zingekuwa ni sera za awamu hii kuhusu sekta binafsi na umma na matokeo yake kwa taifa na uchumi wa mtu mmoja mmoja pamoja na kodi n.k. Ziwepo hoja za kusaidia kukuna vichwa na kufundishana na siyo kutetea kitumbua maana isije fika siku hata hicho kitumbua kikawa hakipo kiuhalisia bali kwenye majukwaa ya siasa tu.

Raisi angekuwa na nia njema,
Angeuzia huu mjadala usisambae kabisa kuanzia kwenye ngazi ya chama (Nipped it in the bud).
Nkamia na genge lake walianzisha hili fukuto mwaka jana hivyo tulitegemea yeye kama Mwenyekiti wa Chama angeyaongea haya mnamo mwaka jana kwenye vikao vya Halmashauri kuu ya Chama vile vilivyofanyikia Ikulu. Tulitegemea kuona Mwenyekiti wa Chama akikemea mawavo haya ya kifedhuli ya Uvunjwaji wa Katiba na Ubakaji wa Demokrasia kama ambavyo anakemea Ufisadi na Uhujumu nchi.

Lakini anapoleta hizi geresha zake kwa sasa ajue hamdanganyi mtu,
Hili suala ni la Kichama kwasasabu wabunge wake ndiyo walitaka walipeleke bungeni,
Yeye analifanya mjadala wa kitaifa huku akitumia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kufanya Propaganda za kitoto,
Anasahu kwamba huu ni mjadala wa CCM kama Chama kwasababu hata ukienda bungeni unaweza kuzua taharuki...
 
Back
Top Bottom