Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Anazuga.Danganya kubwa hiyo.kwa nini asiwaambie hao wanajipendekeza waacha mara moja kama alivyozuia mikutano ya kisiasa!!
 
Kila jamaa wakianzisha uzushi, mnawakosoa sasa wataishi vipi ? Kikwete alisema jamaaa wana viwanda vya uongo. Jamaa mnawaumiza sana ki saikolojia Mme wabana kila kona.


Akiri yako inafikiri pole pole zaidi ya jina la mwenezi wako,mjadala wa Magufuli kujiongezea muda wa uongozi ulianzishwa na wanaccm akiwemo Rais wa awamu ya II mzee Mwinyi,na mahafidhina wa Ccm Zanzibar huku Juma Mkamia akijaribu kabla ya kushindwa kupeleka hoja hiyo bungeni.

Ni wapi wapinzani wamezusha?Si ndiyo ninyi mlikurupuka na kuja na kauli mbiu ya "Magufuli haki?" Mlitaka abaki wapi?
 
Tumeona kakataa miaka 7 kama ilivyopendekezwa na Nkamia na kupondwa na Ole Sendeka & co. Jee mapendekezo ya Heche ya miaka 4 mbona nayo hajayazungumzia? Au anayakubali baada ya kuona kazi aliyosukumiziwa imekuwa ngumu kuhimili miaka mitano?
 
Mkuu hata hiyo saba ni kwavile vigingi vya chama vilisimama mwanzo kabisa kuipinga,lakini ingekuwa tayari tumeshaumia.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
wanaopendekeza miaka saba wanaona karibu kama ufupi wa dhakari yaoo. hiyo miaka saba sio ya magufuri tu ni miaka saba ya kila raisi atakaye ingia.

sasa fikiria akiingia raisi ambaye hana nia njema na taifa miaka saba hali itakuwaje?
 
Hajaamua tu jamaa,hata leo akiamua kua rais wa milele hakuna mtu atamfanya kitu,zitapigwa kelele kidogo tu afu maisha yanaendelea fresh tu.

Hii ndio bongo,ya mabingwa wa forex.
 
Hajaamua tu jamaa,hata leo akiamua kua rais wa milele hakuna mtu atamfanya kitu,zitapigwa kelele kidogo tu afu maisha yanaendelea fresh tu.

Hii ndio bongo,ya mabingwa wa forex.
kweli ni kuwa hajaamua tu au bado anapima upepo

nani ataenda kifua mbele pindi akiamua?
 
ngoja huyu mrwanda aje kwanza maana ndio amekua idol wake.... kila kitu anakopi huko, hata hii miaka saba anayoikataa nadhan ni danganya toto tu, ni plani imeshaandaliwa lakini wanajifanya kuwapumbaza watu mara paaap naye anabadili upepo anasema amekubali kwa nia ya dhati na watanzania wamemuomba haoni sababu ya kukataa... muda utasema
 
kweli ni kuwa hajaamua tu au bado anapima upepo

nani ataenda kifua mbele pindi akiamua?
Aisee mkuu hakuna hata mmoja atasogeza pua yake.

Cha msingi tuombee tu alichokisema ndio akimaanishe otherwise ndo basi tena.
 
Aisee mkuu hakuna hata mmoja atasogeza pua yake.

Cha msingi tuombee tu alichokisema ndio akimaanishe otherwise ndo basi tena.
Never ever trust "African political leaders" kwao maneno yakuongea sio kitu hawanaaga aibu wala huruma na wananchi wao hata kdgo WaPo kwa self survival
 
Aisee mkuu hakuna hata mmoja atasogeza pua yake.

Cha msingi tuombee tu alichokisema ndio akimaanishe otherwise ndo basi tena.
Ziko dalili kuwa baada ya kumsikia Sendeka na kukurupuka kwa Ndugai kwa kauli hiyo ameshtuka kuwa hata ndani ya chama chake anao upinzani mkubwa wa sirisiri ambao ni hatari sana
 
Tumeona kakataa miaka 7 kama ilivyopendekezwa na Nkamia na kupondwa na Ole Sendeka & co. Jee mapendekezo ya Heche ya miaka 4 mbona nayo hajayazungumzia? Au anayakubali baada ya kuona kazi aliyosukumiziwa imekuwa ngumu kuhimili miaka mitano?
Muwe mnajifikiria kabla ya kuposti
nyuzi zina maswali ya kimchepuko!
hakunaga ma GT kabisa siku hizi
 
Never ever trust "African political leaders" kwao maneno yakuongea sio kitu hawanaaga aibu wala huruma na wananchi wao hata kdgo WaPo kwa self survival

Ukweli mtupu mkuu,hakuna mwanasiasa yoyote duniani narudia tena yoyote ana interest ya kumtetea mwananchi,wao ni tumbo lao kwanza basi.
 
Ziko dalili kuwa baada ya kumsikia Sendeka na kukurupuka kwa Ndugai kwa kauli hiyo ameshtuka kuwa hata ndani ya chama chake anao upinzani mkubwa wa sirisiri ambao ni hatari sana
Sasa mkuu ole sendeka ana nguvu gani kwenye chama?Kusema wabunge wanaweza kumfanyia impeachment rais?

Nakwambia mkuu,hata jamaa akisema anabadili hizo terms ndani ya CCM hakuna atakayekohoa hata mmoja bora hata wabunge wa wapinzani watajitutumua ila ndo hivyo wako wachache na atapitisha anachotaka.

Tena tusimtie hasira akaamua kubadilisha mawazo aisee,hahah.
 
Bora alivyotolea ufafanuzi.....

Sisi wengine tunaona lini atamaliza muda wake aende, halafu miccm eti inataka kumuongezea miaka mingine 2!
Hata mi ccm haimtaki tatizo Lao ni unafiki na kajipendekeza
 
Back
Top Bottom