TUTETE KIDOGO - JUHUDI ZA NKAMIA na MUDA WA KUONGOZA
Nadhani WOTE tunajua kuwa hili jambo linaloendelea Sio bahati mbaya. . .
Kabla sijateta, natoa msimamo wangu kwamba kwa Hali ilivyo, namuunga mkono NKAMIA kwa asilimia kadhaa. . . simpingi.
Labda Tuanze hivi. . . ( hii story wengi mnaijua )
Kulikuwa na jamaa mmoja ammbaye alikuwa "mjinga mchangamfu." Alitokea kumtamani mrembo fulani aliyekuwa akiwaniwa na wanaume kadhaa. Kwa jinsi mrembo huyu alivyo na mvuto, Hata akikubali tu kuwa Rafiki yako wa kawaida tu, unajisikia kama uko peponi.
Basi, jamaa huyu Kafanya " njama " Za hapa na pale kwa kushirikiana na majamaa waliokwisha kumnasa huyu mrembo kwa nyakati tofauti, akafanikiwa kuwa karibu na huyu binti. Binti mrembo alimpa nafasi Ya urafiki wenye mipaka kwa miezi kadhaa, Ili kama analipa aongezewe MUDA.
Basi ikaenda ikaenda. . . mwezi wa kwanza, mjinga mchangamfu huyu anaonesha makeke, kwamba anajali, Yaani wale waliokwisha kuwa marafiki wa huyu mrembo wanaonekana hawakuwa "wanatosha" . . . jamaa anakaba, majamaa wengine hawapumui, hawapewi nafasi kabisa Hata Ya kumsalimia huyo mrembo, hadi kero. . .
Mwezi wa pili. . . jamaa akaona kama mrembo hashtushwi na makeke yake wakati mbinu zote hizo ni kutaka ammiliki Yule mrembo.. . . Changamoto ni kumtamkia wazi wazi kwamba anahitaji zaidi Ya ule urafiki. Akaanza kutuma wasela wa kumsifia kwa mrembo, kwamba Yeye ndiye anastahili zaidi kuliko wengine, Lakini jamaa akiwa na mrembo anajifanya kwamba hataki flani hivi, tena anasema anaufurahia na kuuheshimu urafiki wao wenye mipaka. . . . Lakini moyo umelegea kama kuti la mnazi. . .
Basi ikaenda ikaenda. . . siku zikasonga, mrembo anamwangalia tu jamaa anavyohanya kujichekeshachekesha, na kujisifiasifia. . .
Siku moja wakiwa mahali fulani, ghafla tu, mrembo akamwambia jamaa, "Leo Nataka nikupe. . . " Alitaka kumtest jamaa kama alichokuwa anatamka ndicho alichomaanisha. .
Jamaa akauliza "kweli uko siriaz?" mrembo akamjibu ndio, Kisha anambusu shavuni. . .
Kilichotokea; jamaa alizimia. . .
Sababu Za kuzimia ni kule kutoamini kwamba itatokea siku akubaliwe kirahisi vile. . .
* * * * * *
Mimi Nadhani, isiwe miaka 7, Iwe 50. Kwa sababu, kama miaka 5 haitoshi, Saba haiwezi kutosha. . . sote tunajua ccm imeshatawala miaka zaidi Ya 50, wala haikutosha, na sababu watakuambia, kwamba awamu ziliongozwa na watu tofauti, Japo wanasahau kuwa ilani ni Ya chama hichochicho na hakuna rais mwenye ilani yake, bali anaongoza kwa ilani Ya chama. . . . Lakini kuondoa kisababu cha "watu tofauti " apewe huyu mmoja. . . .
Kati Ya maamuzi magumu kabisa tunayotakiwa kufanya ni kwenye hili jambo. . maamuzi kama aliyochukua huyu mrembo. . .
Imani yangu ni kuwa, ndani Ya miaka hii mitatu " tumetangaziwa" maendeleo makubwa hasa kwenye ukuaji wa uchumi, viwanda, miundombinu, elimu nk. Sote tunajua kuwa "matamko" hayo yamekuwa yakishabihiana na "uhalisia." Sasa Nani mwenye akili timamu atakayekubali kupokea huu "uhalisia" ambao haujakamilika?
Pwagu na pwaguzi enzi zao walisema, mtoto akililia wembe, mpe ahangaike nao weeeeee. . baadaye atakurudishia tu, Lakini ukimwekea. ngumu atakusumbua, atavunja vyombo, atakughasi tu mpaka kieleweke. . . .
Nadhani wakati Umefika, Sio saba, hamsini itapendeza. . . . . trust me, mambo yatakuwa bomba kuliko Sasa.
Wapinzani wala msipambane, mkiendelea kupambana kuhusiana na hili mtapoteza. . . . kwa kauli moja, semeni ndiooooooo likifika bungeni, tena mpendekeze apewe 50 kabisa wala kusiwe na uchaguzi, hizo Hela zifanye Kazi nyingine. . . .
Mkifanya hivi, mtanishukuru baadayeeeee kwa sababu kutakuwa na MUDA mzuri wa kuishi kwenye "uhalisia" ambao utakuwa kama shamba - darasa kwa wanayerusalemu na mataifa yote.. . . shamba darasa hili litakuwa na manufaa sana, sana sana sana sana hapo " baadaye"
MWANZO NILISEMA NAUNGA MKONO HOJA KWA ASILIMIA KADHAA, SABA HAITOSHI. . . .
#50_itapendeza
#asomaye_na_aelewe
wasalaam
© BIBI HAPPY J