Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Humphrey Polepole: Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala wa kuongezewa miaka ya Urais kutoka 5 hadi 7

Muongo anatengeneza mazingira tunamjuwa kama tulimzaa huyo ikulu atang'olewa tu hata akipanga kubaki miaka saba asidhani sisi matahira au mazoba
 
Sawa ngoja waje

Habari ya mjini or HOT NEWS ni 2 tu:
  • RIPOTI YA IFM KUHUSU MDORORO WA UCHUMI TANZANIA!
  • UPINZANI KUSUSIA CHAGUZI NDOGOO 3 ZA MARUDIO NA CCM KUKOSA WAPIGA KURA!!!!
Hizi zingine sijui Kusikitishhwa na kuongezewa miaka 7 ya kukaa madarakani...!au Intarahamwe Kagame kumtembelea Intarahamwe mwenzie ni longolongo tu........!!!!
Stay tuned........!
 
Alikuwa wapi siku zote kukanusha kwa kutoa taarifa rasimi?
Hiƴo ni baaɗa ƴa wapiga kura nao leo kususia ƙwenɗa ƙupiga kura. Wanaficha aiɓu wanataka kesho wakae front page siƴo haɓari za kususiwa uchaguzi na wapiga kura
 
Hoja ya hapa kazi tu,majipu mbona haisikiki tena kulikoni?
Majipu yenyewe yamekaa sehemu nyeti, unatangaza kupiga vita ufisadi ukisema mafisadi yanakimbilia CHADEMA halafu kubwa la mafisadi unamwita ikulu tabasamu kuubwa, unasema utawatumbua wala rushwa halafu kwa ushahidi wa video DC anatoa ahadi za rushwa kununua madiwani wa upinzani, takukuru wanambwela mbwela na mtoa rushwa anapandishwa cheo.
Leo hata polepole hawezi muita Lowassa fisadi, utamuitaje fisadi wakati kiongozi wa vita vya ufisadi kamsifia live kwenye viwanja vya ikulu live?
 
Kusema ni kazi ya mdomo, tumesikia, lakini ya moyoni hayajulikani. Ukweli ni muhula wa 2, kauri itakuwa tofauti.
 
Hoja wa kuongezewa muda wameibua Ccm wenyewe alfu wanaikemea wenyewe kuna Sanaa kubwa sana hapa
Ni kweli mzee tunaandaliwa ili ɓaaɗaƴe aseme mimi sikutaka na nilisha sema huko nƴuma ila wananchi wameniomɓa nienɗelee.Ƙama alisha twamɓia hakutaka ƙuwa rais ila alisukumizwa je atashinɗwa kusema alisukumizwa na wananchi aenɗelee kuwa rais?
 
Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala unaoendelea juu ya kuongezwa kwa kipindi cha Urais kutoka miaka 5 hadi miaka 7.
View attachment 674687
Naomba kuuliza
Hivi kuna mjadala unaoendelea juu ya kipindi cha urais kweli,
Hii habari mbona ni ya muda sana,
Kwa nini wakati wanaccm wapipoanza kuomba na kuibua mjadala huo kipindi kile jamaa hakusema anasikitishwa
Lkn mjadala umeisha ndo anasema anasikitishwa,
Hii maana yake nini,
 
Kama Uongo ukimaanisha Uongo basi ni Ukweli.

Issue ya kuongeza muda itakuwa hot baada ya 2020, muhula wa pili , sasa hivi ni maandalizi tu ili watu wazoee lisiwe jambo geni
 
Taratibu wanaanza kuwaandaa waTz kisaikolojia kwa mbinu ile ile ya PK. Ionekane wananchi ndo walimtaka akae zaidi kumbe ni geresha.
 
Njia moja mbadala wa kuanzisha mjadala, ni kuanza mjadala. Hivi karibuni Nchi jirani mwetu Raisi M7 waliweza kubadilisha Katiba kuondoa ukomo wa miaka ya anayegombea Uraisi wa nchini humo. Katika kurupushani hizo, wabunge wengi hawakuwa wanakubaliana na jambo hilo...maoni yangu hawa wamepewa miaka miwili zaidi ili tu wapitishe mabadiliko hayo

Unapoanza kuona hayo, basi uwezekano mkubwa propaganda ya CCM ndio imeanza.

Vitu vya kutafakari kama huu utakuwa mjadala wa kitaifa na kama haya ni ya kweli

Hakuna mjadala wa kubadilisha katiba ya nchi kwa ajili yaku wabeba CCM-bali itakayo mbeba mtanzania(mzalendo) kama ilivyo kwenye rasimu, na ilenge matakwa ya wananchi wote na sii baadhi ya Club Cha Mwino!

Mjadala wa kujiondoa katika Commonwealth( Huu bado ni ukoloni) ambayo haina tija katika karne hii.

Mjadala huu unganishwe na mijadala ya kupitia mikataba yote ya nchi kila baada ya miaka mitatu, na iipe bunge nguvu ya kuvunja kama haina tija kwa mwananchi.(barabara siyo tija)
........namengine mengi ambayo "tunaweza" kuweka katika mijadala ya taifa ambayo kwangu binafsi ninge shauri ifanyike miaka ya miwili ya mwisho wa chama kilicho madarakani. Kuridhia
Aluta Continua....
 
Alikuwa wapi siku zote kukanusha kwa kutoa taarifa rasimi?
Mkuu mbona alisema kule Tanga ktk mojawapo ya hotuba yake hana mpango wa kubadili katiba kuongeza muda wa muhula wa uraisi.

Alimjibu Prof. Majimarefu. Au ulitaka hadi kwa maandishi?
 
Rais Magufuli hafurahishwi na mjadala unaoendelea juu ya kuongezwa kwa kipindi cha Urais kutoka miaka 5 hadi miaka 7.
View attachment 674687
Mjadala gani na unaendelea wapi?!
Mbona wanatufanya as if kuna watu wanataka hiyo miaka 7. Si kina nkamia akawakanye kwenye ccm yao huko.

Aheshimu katiba na ukomo wa madaraka upo kikatiba.
 
Back
Top Bottom