Humphrey Polepole: Tafakari, tumeuzwa, tumepigwa bei. Rostam Aziz amepewa migodi kwa bei ya kulangua!

Humphrey Polepole: Tafakari, tumeuzwa, tumepigwa bei. Rostam Aziz amepewa migodi kwa bei ya kulangua!

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Rostam Aziz kupitia kampuni yake ya Taifa Mining walinunua hisa katika Mgodi wa Mwadui. Mwishoni mwa 2024 na mapema 2025, Kampuni yake ya Pink Diamonds ilinunua hisa toka Petra Diamonds katika Mgodi wa Williamson Diamond Mine (Mwadui) na kuifanya kampuni ya Taifa Mining kumiliki hisa asilimia 75.

Disemba 15, 2021, Petra walitangaza kuingia mkataba wa awali (usiofunga pande zote) na Caspian Limited. Mwaka 2023, Petra Diamond walitangaza kuingia makubaliano kwa nyaraka ya kimkataba (Memorandum of Understanding) na kampuni ya Caspian Limited (kwa sasa Taifa Minining and Civils Limited).

Mauziano hayo yalihusisha kuuzwa kwa asilimia 50 pungufu ya hisa moja ya taasisi iliyokuwa ikihodhi hisa za Petra, kwa takribani Dola za kimarekani milioni 15 (Takribani TZS Bilioni 35.9 za kitanzania).

 
Polepole ameelezea jinsi Rostam alivyojitwalia Mgodi wa Makaa ya Mawe kwa bei chee (Bilioni 5 tu).

———

Rostam Aziz anamiliki hisa katika kampuni kadhaa zinazojihusisha na uchimbaji madini ya makaa ya mawe, hasa kampuni yake ya Taifa Mining and Civils ambayo ilinunua hisa za kutosha katika Mgodi mkubwa kabisa nchini wa TANCOAL, kutoka Intra Energy Corp. mwaka 2021

Rostam alikuwa mwanahisa mwenye hisa nyingi katika kampuni ya TANCOAL, ambayo inaendesha mgodi wa Makaa ya Mawe wa NGAKA (mgodi mkubwa kuliko yote nchini)

Taifa Mining ilinunua hisa nyingi toka Intra Energy mwishoni mwa mwaka 2021 na hisa binafsi za Rostam ndani ya Taifa Group ziliwekwa bayana mwanzoni mwa mwezi Aprili 2025
 
Hili Nalo ukiwa Mzalendo na mwenye Akili lazima likusikitishe kwelikweli !!.

Magufuli mwaka 2017 alikamata kafurushi kadogo ka almas kakitoroshwa kakiwa na Thamani ya abilioni 60.

Baada ya Magufuli Kufa, Serikali ya Samia ikauza 30% ya Mgodi huo Kwa Rostam Aziz Kwa Bilion 30 achimbe miaka na miaka!!.

Daahhhhh ama kweli Wahuni wameishika Nchi !!.
 
Hii sheria ikipitishwa ndo kiboko ya Uchawi kila mtu atatimiza uwajibu wake kabisa ndo mwanzo wa kua na Tanzania mpya mwisho wa Uchawa nayaona maendeleo ya nchi kwa kasi ya ajabu. Nilikua najiuliza inakuaje Rais hawezi kushiktakiwa kwasababu inaama anaweza kuuza rasilmali zote za nchi hakuna cha kumfanya tulichelewa sana mwizi wa kuku anafungwa wezi wa rasilmali za nchi wako kwenye V8 just imagine Seth singa singa anadunda anakuja kufungwa DeD kakwapua milion 400 sio fair jela zimejaa maskini tu
 
Hili Nalo ukiwa Mzalendo na mwenye Akili lazima likusikitishe kwelikweli !!.

Magufuli mwaka 2017 alikamata kafurushi kadogo ka almas kakitoroshwa kakiwa na Thamani ya abilioni 60.

Baada ya Magufuli Kufa, Serikali ya Samia ikauza 30% ya Mgodi huo Kwa Rostam Aziz Kwa Bilion 30 achimbe miaka na miaka!!.


Daahhhhh ama kweli Wahuni wameishika Nchi !!.
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Nilivyomsikia Polepole ni kuwa zile asilimia 30 Rostam alinunua toka kwa kampuni ambayo ilikuwa inamiliki asilimia 70 hivi. Kwa nini kampuni hiyo iliuza hisa kwa Rostam badala ya serikali, hatuwezi jua. Nipo tayari kukosolewa hapa otherwise, tupo pamoja.
 
Nashindwa hata kuendelea kuandika lolote katika hili.

Kweli kabisa, Mgodi wenye Uhai wa miaka karibu 400, unauza Asilimia 70 yake Kwa Bilioni 5??.



Alafu kumbe hata hiyo Bilion Tano hajalipa yote, kalipa Bilioni 2, na bado Serikali hailipwi chochote tangu Uchimbaji wake .


INATIA HASIRA .. hivi Hawa Machawa ,wa Mama anaupiga mwingi, wenzetu ni Watanzania kabisa???.


Wanaanzisha Matozo Kila Mahali kumkandamiza Mtanzania, ili hali Pesa ipo tele ?.
Aah, bilioni 5!!!!??? Oktoba 29 mbali sana aisee
 
Akizungumza kwa njia ya mtandao Balozi wa zamani nchini Cuba amesema tumeuzwa tumepigwa bei.
Mpuuzieni huyu juha hana lolote. Anabwabwaja wakati awamu iliyopita ndo hao hao walituonea Na kumuua akwilina na kutoa statement za kukera eti risasi ilienda juu halafu ikatua kwa akwilina.

Yani wabongo tunasahau haraka sana. Eti leo hii takataka hii inaitwa shujaa.
 
Nashindwa hata kuendelea kuandika lolote katika hili.

Kweli kabisa, Mgodi wenye Uhai wa miaka karibu 400, unauza Asilimia 70 yake Kwa Bilioni 5??.



Alafu kumbe hata hiyo Bilion Tano hajalipa yote, kalipa Bilioni 2, na bado Serikali hailipwi chochote tangu Uchimbaji wake .


INATIA HASIRA .. hivi Hawa Machawa ,wa Mama anaupiga mwingi, wenzetu ni Watanzania kabisa???.


Wanaanzisha Matozo Kila Mahali kumkandamiza Mtanzania, ili hali Pesa ipo tele ?.
..eti kodi kupata hela mfuko wa kukabiliana na ukimwi, halafu unampa mtu mgodi wa lifespan miaka zaidi ya 100 kwa billion 5 ndio maana ya kuweka waziri wa madini aina ya huyu aliyepo..ambae hata umpe ukatekista hataweza! Mavunde..tunawekewa watu wa ajabu kabisa, hata huyo mwenyekiti tume ya madini huyo mama ni vikaragosi tu..ili wawe rubber stamp kuhalalisha uporaji!
Nchi hii ina laana!
 
Back
Top Bottom