Humphrey Polepole upepo wa kisasi unakuandama. Chunga sana, Mungu ndio anakulipa hivyo

Humphrey Polepole upepo wa kisasi unakuandama. Chunga sana, Mungu ndio anakulipa hivyo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
HUMPHREY POLEPOLE UPEPO WA KISASI UNAKUANDAMA. CHUNGA SANA. MUNGU ANAKULIPA.

Kwa Mkono wa Robert Heriel

Kisasi kisasi! Ni Jambo la hatari ambalo linaweza kuzuilika lakini ni ngumu kuzuilika.

Miaka kadhaa iliyopita wakati wengine wakifungwa midomo wasiikosoe serikali Ndugu yangu POLEPOLE alikuwa kimya, Hakuwa anapiga kelele Kwa sababu alikuwa sehemu ya Mfumo. Kama POLEPOLE angekuwa Mpenzi na Muumini wa Haki basi hizi kelele zake tungezisikia tangu awamu ya tano ambapo hakuna ubishi kuwa ilikuwa awamu iliyogubikwa na kuziba watu midomo.

Kama POLEPOLE angekuwa mkweli hivi leo kila mtu angeungana na yeye kuwa ni mwenye Haki kwani Hana Double Standard. Lakini POLEPOLE sio mwenye Haki, sio msema kweli Kama anavyojitanabaisha mbele ya Kamera.

Unajua hata watu Wabaya wanajua Fulani ni mwenye Haki Mwema.
Lakini ukishakuwa Double Standard hata waovu wanaona kuwa wewe ni Muovu Kama wao tuu. Hivyo hawaoni shida kukufanyia Uovu wao.

Kinachomtesa Polepole kwa sasa ni UPEPO mbaya wa kisasi unaozunguka katika mfumo wake wa maisha.

Ninachomuomba awe mjanja, awe makini ikiwezekana atambue kuwa kinachotaka kutokea ni muda wa malipizi.

Wakati miaka iliyopita walioikosoa serikali wakivamiwa na watu wasiojulikana, wakitekwa huku wengine wakipotea kusikojulikana mpaka hivi leo, POLEPOLE hakuwahi kusema kitu, Hakuwa kupinga Uovu huo. Aliona ni SAWA,

Leo anashangaa, anabweka anapozuiwa kuongea, anapozibwa mdomo asiongee mawazo yake. Polepole hapa unachokitafuta hukijui; kuna kisasi kinakutafuta ulipwe Sawasawa na Wale waliofanyiwa wakati ule ukiwa sehemu ya utawala upande wa CCM.

Ujasiri ulionao usiizidi Akili yako, huo ujasiri lazima ujue chimbuko lake ni lipi hasa, je mi ujasiri utokanao na HAKI? Hilo nalipinga Kwa sababu nilishasema kuwa ungekuwa mtu wa haki ungepinga tangu awamu ya tano.

Je, mi ujasiri utokanao na KISASI kinachokutafuta kukuangamiza ili uwe fundisho Kwa kizazi hiki na kijacho? Jibu ni ndio.

Hao wanaokuambia ukae kimya wanakuona unawakosea Kwa sababu mbona wakati wa awamu ya tano hukuwahi kuipinga SERIKALI wala kuikosoa?

Kimsingi wanayohoja alafu wewe hauna hoja ya kuwaelewesha kuwa iweje awamu ya tano iliyojaa ukandamizaji wa Uhuru wa kutoa maoni ulikaa kimya alafu leo hii kujifanya unaongea.

Hoja zako hazijibiwi Kwa sababu hawaoni sababu ya kukujibu na hawaoni kuwa hoja hizo unastahili kuzianzisha wewe mnafiki uliyenyamaza awamu ya tano.

Hata ningekuwa Mimi nisikubali nikujibu hoja zako na wala nisingekuruhusu uzitoe.

Yaani wakati unakunywa Castle Lite ulikaa kimya kusema ni pombe. Alafu Mimi wakati wangu nikinywa Serengeti unanyanyua mdomo wako kuwa niache kunywa pombe wakati hata Castle Lite nayo ni pombe labda kiwango tuu cha ulevi kilichopo.

Mwisho; jichunge Sana, ujasiri ulionao ni matokeo ya kisasi kinachokutafuta kukuangamiza ili kuwalipia wale walioumizwa wakati ule wewe ukiwa kiongozi.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Polepole ni mnafiki mmoja hivi, wakati wapinzani wanapotea, wanauawa, wanapewa kesi mbalimbali nchini, uchaguzi ulipokuwa unavurugwa na mengi mengi Je alikuwa wapi? Si alikuwa anafaidi kwenye ma-vieteee.

Asituchoshe, ni muda wa kupambana na hali yake, kutesa huwa ni kwa zamu - afu bado tunamdai chenji yetu ya yale manunizi ya wapinzani wakati wa kuunga juhudi.
 
Huyu huyu Polepole aliyekwenda kumtolea faini Msingwa baada ya michango ya kuwatoa viongozi wa Chadema ndani kufanikiwa!
 
Polepole amejiibia mwenyewe TV, na kujivurugia mari nyinginezo Kisha akaandika ujumbe kwenye kijikaratasi et acha kuicrash awamu ya SSH, Kama natania chukueni karatasi lenye ujumbe mpeleke polisi Kama majibu hayatasema ni mwandiko wa polepole!

Hizi ndo siasa za CCM, Polepole anajua vizur!
 
Wewe huelewi. Polepole hapingi ila anatoa elimu
Hiyo Elimu angeitoa awamu ya tano ambayo iligubikwa na uzibaji watu mdomo.

Yaani ni kusema H. Polepole anakosa uhalali WA kutoa elimu ya Haki na ukweli Kwa sababu alishindwa kuitoa elimu hiyo nyakati akiwa yupo sehemu ya uongozi wa awamu ya tano iliyojaa ukandamizaji Mkubwa.

Angejaribu kipindi kile leo hii hata mtoto mdogo angekuwa anamuelewa

Ila anachokifanya ni unafiki,
 
Kutoka uanaharakati kua mlamba viatu halafu unataka kujifanya mwanaharakati tena. Hakuna atakae kuonea huruma labda watu wa Human Rights mbali na hapo utaishi kama nguchiro huaminiki tena.
Dawa atiwe kilema tu Cha kwenye masaburi yake
 
Back
Top Bottom