Humphrey Polepole upepo wa kisasi unakuandama. Chunga sana, Mungu ndio anakulipa hivyo

Humphrey Polepole upepo wa kisasi unakuandama. Chunga sana, Mungu ndio anakulipa hivyo

Huyo anatakiwa kupigwa na kitu kizito ,aache upumbavu kabisa ....
 
Wapambe, walinzi, chawa, viroboto, wahuni, wageni, etc ni maneno yalopata kutumika sana wiki jana na wiki hii yatatumika pia

hata vikombe kwenye sinia hugongana, vingine kuvunjika na vingie kuwa na mapengo na vingine kukwaruzika na vingine kubaki ka vilivyokuwa... tuendelee kula popcorn
🍿
🍿
🍿
 
Awamu ya 5 hakuwa na muda

Alikuwa na muda wa kupanga namna kununua watu, kufunga watu midomo, kutuma wasiojulikana kuumiza watu, kutesa na kuuwa watu ndo alikuwa busy kufanya hayo,

Angekuwa mwenye haki alipoona watu wanaonewa angepaza sauti kutetea, sasa ameachwa pembeni anaona mkuki ulivyo mchungu!!

Hatutaonea WANAFIKI huruma, akale alipopeleka mboga,
 
Bichwa lako halina kitu. Polepole anaongelea nadharia ya vitabu na mustakabali wa bara la africa na Tanzania, yaani ni sawa na wewe kujisomea hicho kitabu.
 
HUMPHREY POLEPOLE UPEPO WA KISASI UNAKUANDAMA. CHUNGA SANA. MUNGU ANAKULIPA.

Kwa Mkono wa Robert Heriel

Kisasi kisasi! Ni Jambo la hatari ambalo linaweza kuzuilika lakini ni ngumu kuzuilika.

Miaka kadhaa iliyopita wakati wengine wakifungwa midomo wasiikosoe serikali Ndugu yangu POLEPOLE alikuwa kimya, Hakuwa anapiga kelele Kwa sababu alikuwa sehemu ya Mfumo. Kama POLEPOLE angekuwa Mpenzi na Muumini wa Haki basi hizi kelele zake tungezisikia tangu awamu ya tano ambapo hakuna ubishi kuwa ilikuwa awamu iliyogubikwa na kuziba watu midomo.

Kama POLEPOLE angekuwa mkweli hivi leo kila mtu angeungana na yeye kuwa ni mwenye Haki kwani Hana Double Standard. Lakini POLEPOLE sio mwenye Haki, sio msema kweli Kama anavyojitanabaisha mbele ya Kamera.

Unajua hata watu Wabaya wanajua Fulani ni mwenye Haki Mwema.
Lakini ukishakuwa Double Standard hata waovu wanaona kuwa wewe ni Muovu Kama wao tuu. Hivyo hawaoni shida kukufanyia Uovu wao.

Kinachomtesa Polepole kwa sasa ni UPEPO mbaya wa kisasi unaozunguka katika mfumo wake wa maisha.

Ninachomuomba awe mjanja, awe makini ikiwezekana atambue kuwa kinachotaka kutokea ni muda wa malipizi.

Wakati miaka iliyopita walioikosoa serikali wakivamiwa na watu wasiojulikana, wakitekwa huku wengine wakipotea kusikojulikana mpaka hivi leo, POLEPOLE hakuwahi kusema kitu, Hakuwa kupinga Uovu huo. Aliona ni SAWA,

Leo anashangaa, anabweka anapozuiwa kuongea, anapozibwa mdomo asiongee mawazo yake. Polepole hapa unachokitafuta hukijui; kuna kisasi kinakutafuta ulipwe Sawasawa na Wale waliofanyiwa wakati ule ukiwa sehemu ya utawala upande wa CCM.

Ujasiri ulionao usiizidi Akili yako, huo ujasiri lazima ujue chimbuko lake ni lipi hasa, je mi ujasiri utokanao na HAKI? Hilo nalipinga Kwa sababu nilishasema kuwa ungekuwa mtu wa haki ungepinga tangu awamu ya tano.

Je, mi ujasiri utokanao na KISASI kinachokutafuta kukuangamiza ili uwe fundisho Kwa kizazi hiki na kijacho? Jibu ni ndio.

Hao wanaokuambia ukae kimya wanakuona unawakosea Kwa sababu mbona wakati wa awamu ya tano hukuwahi kuipinga SERIKALI wala kuikosoa?

Kimsingi wanayohoja alafu wewe hauna hoja ya kuwaelewesha kuwa iweje awamu ya tano iliyojaa ukandamizaji wa Uhuru wa kutoa maoni ulikaa kimya alafu leo hii kujifanya unaongea.

Hoja zako hazijibiwi Kwa sababu hawaoni sababu ya kukujibu na hawaoni kuwa hoja hizo unastahili kuzianzisha wewe mnafiki uliyenyamaza awamu ya tano.

Hata ningekuwa Mimi nisikubali nikujibu hoja zako na wala nisingekuruhusu uzitoe.

Yaani wakati unakunywa Castle Lite ulikaa kimya kusema ni pombe. Alafu Mimi wakati wangu nikinywa Serengeti unanyanyua mdomo wako kuwa niache kunywa pombe wakati hata Castle Lite nayo ni pombe labda kiwango tuu cha ulevi kilichopo.

Mwisho; jichunge Sana, ujasiri ulionao ni matokeo ya kisasi kinachokutafuta kukuangamiza ili kuwalipia wale walioumizwa wakati ule wewe ukiwa kiongozi.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Acha kutumia jina LA Mungu kipuuzi, HV polepole kamuuzi Mungu kuliko wengi wasio na matatizo hayo. Usichukue vipimo vya mwanadamu ukafananisha na vya Mungu.
 
Bichwa lako halina kitu. Polepole anaongelea nadharia ya vitabu na mustakabali wa bara la africa na Tanzania, yaani ni sawa na wewe kujisomea hicho kitabu.
Alitakiwa atoe yote hayo kipindi cha mwendazake, wakati wa utesaji wa watu, acha aonje joto ya jiwe!!

Kila mtu ashinde mechi zake bana!!!
 
Andiko lako ni zuri ila sasa unaharibu unapoanza kuziingiza Castle lite na Serengeti kwenye mambo ya kipumbavu(samahani kwahii lugha). Ila umeikosea sana Castle lite na Serengeti broo

😀😀😀😀

Wazee WA Bia Tamu mnisamehe asee
 
Awamu ya 5 hakuwa na muda

😃😃😃

Ati anazibwa mdomo 😃😃

Hivi anajua anachokisema???

Awaulize CHADEMA maana ya kuzibwa mdomo apate shule.

Wenzake hata hizo press zake zisingeruhusiwa,
Hicho kipindi chake cha shule ya uongozi wala kisingekuwa hewani.

Au amesahau wenzake namna wanavyozibwa mdomo na kujikuta Korokoroni Kwa kesi za usumbufu??
 
Hakuna anayeweza kumsikiliza pole pole.labda anayejitoa ufahamu.
Mama nae kapooza Sana.
Alitakiwa aanze na huyu.
Wampeleke hata hapo mabwe pande.akaonje maumivu ya mashujaa wa kukosoa serikali.
 
Hakuna anayeweza kumsikiliza pole pole.labda anayejitoa ufahamu.
Mama nae kapooza Sana.
Alitakiwa aanze na huyu.
Wampeleke hata hapo mabwe pande.akaonje maumivu ya mashujaa wa kukosoa serikali.

😀😀😀

Ati anazibwa mdomo!!

Wenzake hata hizo press zake hawapewagi nafasi.

Hata hicho kipindi chake kingezuiwa na sasa hivi angepaswa awe na kesi ya uchochezi Kama walivyokuwa wanafanywa wazibwa midomo
 
Bichwa lako halina kitu. Polepole anaongelea nadharia ya vitabu na mustakabali wa bara la africa na Tanzania, yaani ni sawa na wewe kujisomea hicho kitabu.

Hizo nadharia ndio alipaswa azionyeshe wakati akiwa kiongozi lakini akashindwa.

Alikaa kimya wakati wengine wakitekwa na kuuawa,
Alikaa kimya wengine wakizibwa mdomo na kupewa kesi za hapa na pale.
Leo anatoa shule ipi sasa??

Hiyo shule awafundishe watoto wake inatosha
 
[emoji3][emoji3][emoji3]

Ati anazibwa mdomo!!

Wenzake hata hizo press zake hawapewagi nafasi.

Hata hicho kipindi chake kingezuiwa na sasa hivi angepaswa awe na kesi ya uchochezi Kama walivyokuwa wanafanywa wazibwa midomo
Kama sikuwepo utawala wa polepole kipindi kile akiwa CCM nitamuamini.
Awalaghai ambao hawakuwepo.
Ujue anaweza akawa anaongea vitu vya maana.
Tatizo tayari alishachafuka.
Alafu watu bado hatujasahau.
Alijitoa Sana ufahamu mpaka akapachikwa pale CCM akawa kiongozi.leo katolewa anaanza maneno maneno.
Nani atamuamini?
 
Na hiyo ndio sababu anakosa uhalali.

Yeye anashangaa kuzibwa mdomo wakati huu wakati awamu ya tano yote watu walizibwa mdomo Kwa maumivu makali
 
Back
Top Bottom