Humu JamiiForums hakuna wife material, kijana usidanganyike

Humu JamiiForums hakuna wife material, kijana usidanganyike

Inawezekana Nina pasaka chache na eid chache humu JF lakini kwa uchunguzi wangu mke bora hayupo JF, wanawake wengi wapo JF kwa ajili ya stress zao za mahusiano au ndoa.

Embu niambie Kuna member gani waliwahi kukutana JF mpaka wakaoana, na kuwa na familia kabisa, mtakaonijibu mje na ushaidi.

Mwanamke anatumia ID fake anaweza kweli kuwa mama Bora wa familia, washazoea kuigiza maisha. Vijana wa JF acheni kwenda PM mtapigwa na kitu kizito, humu kila mtu yuko single.

Kama umeshindwa kupata mke uko mtaani kwenu usijidanganye uje JF kutafuta mchumba, umeishaaaa.
Kwamba humu kuna mashangazi peke yake? Basi tugawane hayo hayo.
Na wao ni watu pia
 
Kwa kuwa wewe haufaham haimaanishi kuwa hakipo.

Wapo waliooana kutoka humu na wanafamilia nawafaham.

Wapo mabinti swafi kutoka humu, wapo washkaji wenye vision na wataalam wenye kujielewa kutoka humu.

Ishi na watu vizuri, utakavyojiweka humu ndivyo utakavyovuna humu.

Ushauri: fungua ID isiyo fake pia utaona mbeleni.
 
Pandisha uzi ukielezea walichokufanyia ili tuelewe zaidi bro.

Punguza kuzunguka sana bro unafanya watu wasikuelewe ilihali unaweza kuwa na nia njema ila kuzunguka sana kukafanya usieleweke na kuonekana wa HOVYO na sisi wanaume wenzako na hata hawa dada zetu.

Mbona ndugu yangu Liverpool VPN alianzisha uzi akafunguka na watu wote tukamwelewaaa?
Jamii forum iko huru una haki ya kutoa mawazo yako
 
Mnahangaika kumpa proof mtu aliye desperate na maisha yake huko halafu anakuja jf kusimanga watu[emoji1787]

Mwanaume kamili anayejitambua huwezi kuta yupo kulialia humu jf.
Shida ni kuwa tunapokutana na changamoto fulani mahali. (Mfano mtu katapeliwa JF) basi hudhani JF wote ni matapeli.

That's a logical fallacy, Hasty Generalization.
 
Kwa kuwa wewe haufaham haimaanishi kuwa hakipo.

Wapo waliooana kutoka humu na wanafamilia nawafaham.

Wapo mabinti swafi kutoka humu, wapo washkaji wenye vision na wataalam wenye kujielewa kutoka humu.

Ishi na watu vizuri, utakavyojiweka humu ndivyo utakavyovuna humu.

Ushauri: fungua ID isiyo fake pia utaona mbeleni.
Mkuu best comments in this thread umemaliza kila kitu,inabid Wana Jf wajifunze kwako unajibu kwa hoja Kama wew sio wanakurupuka na kutoa huruma Wana jibu kihisia tu
 
Eh kasema unadhani hii Dunia si imeisha nilishasema sintokuja huku ila nakuja.
Yaani hadi magari ya wanaume asilimia kubwa ni ya wanawake, ofisi , kila kitu , Cha wanawake . Hadi Kodi wanalipiwa an wanawake asilimia kubwa Kwa Sasa
Kwamba huko duniani uliko wanawake ndio wanamiliki pesa na vitu kuliko wanaume? Dunia ya wapi hiyo?

Wewe binafsi umewazidi kipato wanaume wangapi?

Wewe sema una bahati ya kukutana na mapunga, au huwa una date na vitoto vidogo kuliko wewe.

Siku zote mwanamke atafuatwa na wanaoendana nae (wanaommudu), huwezi kuwa wa low standard kisha utarajie kuvutia wanaume wanaojielewa.

We pambana na hao unaowavutia.
 
Shida ni kuwa tunapokutana na changamoto fulani mahali. (Mfano mtu katapeliwa JF) basi hudhani JF wote ni matapeli.

That's a logical fallacy, Hasty Generalization.
Kabisa,Inabidi adeal na hao matapeli.
Kuna wenzie nao walio desperate kama yeye wanakuja kumuunga mkono kwa kutukana wanawake wote hata ambao hawawajui.,anatukana utadhani anawajua[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom