Huna kazi lakini kwenye simu una 50,000 Tshs tu, ifanyie hiki ninachokushauri...

Nmekuelewa Sana HAPA Mkuu
 
Dah
 
Mada nzuri na mleta mada amezungumzia kufua,kupika kama mfano tu sasa wanaume nao wanataka hizo hizo.

Kikubwa ni uangalie wew una ujuzi gani ambao unaweza fanya bila mtaji na ukajitangaza kwa njia ya business card. Inaweza kua hata ujuzi wa ufundi wa vifaa vya umeme, kuchonga fence, kufundisha watoto hesabu,English ,Dini (qur-ani) kama masomo ya ziada etc.

Mfano mimi ninapenda sana na ninaweza kufanya interior decorations kuanzia kukuchagulia rangi za kuta,sofa mapazia, kukufanyia shopping ya fanicha na mapambo na kukutengenezea pia(natengeneza pia mapambo ya ukutani,mezani ect.) So na mimi nmefikiria kutengeneza hizo cards .

Na kama kuna mtu hapa atahitaji huduma yangu KARIBU.
 
Safi Sana... napenda kuona kuna mtu anaelewa na anaweza jiongeza zaidi.

kuna mtu mawazo yameishia kwenye kufua na kupika,anasoma thread kama

anasoma nipashe au mwananchi,hajui hapa ni darasani panahtaji usome na uelewe..
 
Vip kuhusu usalama? Kuna watu sio waaminifu utaenda kufanya usaf aseme umemuibia hapa utaepuka Vipi huu mtego
 
Kuandika ni rahisi sana kuliko uhalisia wenyewe.
Nikuulize mleta mada :
Hivi wewe unaweza kufanya hizi kazi ulizoorodhesha kwenye huu uzi wako? Like seriously mwanaume mzima ukafue ch***pi na boksa za wanaume wenzako??

No way, huo ni unyonge kupitiliza. Anyways, wapo wadada wanafanya hizi kazi lakini kibongo bongo wanapitia nyakati ngumu sana.

Kwa Ulaya na Marekani, yes, kuna unafuu fulani kwa wanaofanya hizi kazi. Lakini kwa Wabongo bado hatujastaarabika kabisa. Hata Uarabuni bado sana, wanaofanya hizi kazi wanateseka.

Asikudanganye mtu. Hakuna kazi ngumu kama ya kwenda kumfanyia mtu kazi za usafi ndani kwake. Kibongo bongo inahitaji moyo wa chuma.
 
Muongozo mzuri sana...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Duh kweli haiingii akilini
 
Kuandika ni rahisi sana kuliko uhalisia wenyewe.
Nikuulize mleta mada :
Hivi wewe unaweza kufanya hizi kazi ulizoorodhesha kwenye huu uzi wako? Like seriously mwanaume mzima ukafue ch***pi na boksa za wanaume wenzako??
Ndio naweza kufua nguo za ndani za mwanaume mwenzangu

sio hizi safi tu hata zile ambazo kazichafua na haja nafua tena

kwa ubora wa hali ya juu,sina kinyaa,najua namna yakujitunza afya yangu

siogopi chochote,natafuta maisha sitafuti Show Off,ninapokua sina pesa nazitafuta sana mkuu

kazi pekee ambayo sitofanya ni yakumkosea muumba au kuvunja sheria za nchi,zingine zote nafanya.

ukinikuta natafuta pesa mkuu,wewe ukitaka hata kunitemea mate nitemee sitokufanya kitu,si unajiona

umeyapatia sana,its ok with me,ninachojua tu siku zote hakunaga situation Permanent,everything is temporary tu, hata hali hii ya umaskini wa kufua hizo nguo muda wake utapita tu,n muda tu boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…