Huna sababu ya kuwa baba wa kambo hasa ukiwa chini ya miaka 45

Hakika wew ni professor na mhadhiri wa ngazi za juu
 
Hivi Watibeli wanatokea mapori gani hapa tz?
 

Wewe unatatizo la kusoma kwa ufahamu.

Embu isome mada vizuri kisha uielewe.

Hakuna sehemu nime attack single mother

Nilichoongea ni ukweli ambao hutaki kuusikia.
Kwa mfano single mother amechoka kuishi na wewe. Anataka kuondoka(mpeane talaka) hapo kosa lake liko wapi?
Sasa siangalii kosa lake. Naangalia nini hasara za mwanajme
Ndiyo ila wengi wanajilipua

Wanajilipua kwenye bomu lenyewe
 

Wewe uliwahi kusikia child support akadaiwa baba wa kambo?
Embu acha kufurahisha watu humu bado tupo kwenye kesi ya Lisu
 
Pia hakuna mtoto wa kambo wala wa nje ya ndoa wote ni watoto

Na kuwa single mothers sio tatizo

Binadamu wote ni wabinafsi sana kwahiyo katika kuishi ni muhimu uweke mifumo yako vzr kwakuwa hata watoto uliowazaa wanaweza wasiwe na msaada wowote kwako


Kuzaa ni kama kubeti tu

Wazee wengi wanaoteseka walikuwa na mentality za kuzaa watoto ili waje wawasiidie uzeeni na Sasa wanapata shida
 

Kupasha kiporo ni kisingizio tuu.
Hoja kuu mara nyingi ni Utegemezi wa wanawake hali inayopelekea kuwa dilemma kwenye kumtunza mtoto.

Pili ni suala la malezi, mtoto anahiyari ya kumchagua baba mzazi
 
Hujakutana na mwanamke mzuri mpaka ukalelea watoto wake 5.

Muulize Diamond Platimuz utaelewa hili.
 
Hawa wote % kubwa wahudumiaji wa watoto wa kambo mkuu, unaweza kuta mtibeli katoka kulipa ada akililia penzi hajajua tu kuwa keshachangia sehemu yake kwa mtoto wa kambo.

Mimi siwezi kufanya kitu kama hicho Mkuu.
Mimi kama ni msaada natoa kwa watoto wenye uhitaji, Yatima na wenye maisha duni

Lakini siwezi msaidia mtu asiyehitaji msaada, baba yake yupo na amekimbia wajibu wake.

Kusapoti mtoto aliyetelekezwa bila kumchukulia hatua mtelekezaji ni kuchochea na ku-encourage utelekezaji indirectly
 
Na hii tabia kuzaa watoto ili waje wakusaidie baadae ni upumbavu wa hali ya juu sana
 
Kwani utajua sasa Mtibeli? Kila pesa unayompa mwanamke unahakiki inaenda wapi?
 
Kuzaa nje ya ndoa hakuna tatizo lolote na kuwa baba wa kambo hakuna tatizo lolote

Tatizo lipo pale hiyari yako itapotofautiana na hiyari ya mtoto na huyo mwanamke.
Jambo lolote ambalo ni hiyari lazima uliendee kwa tahadhari kwa sababu mbele kunakurukana.

Hiyari inabadilika muda wowote. Sasa unapowekeza kwenye jambo la hiyari na utumie nguvu zako zote ni kwamba umeamua kujilipua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…