HURUMA: Mdude Nyagali awatoa machozi wajumbe wa Kongamano la Katiba Mpya

HURUMA: Mdude Nyagali awatoa machozi wajumbe wa Kongamano la Katiba Mpya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mfungwa wa Kisiasa aliyeishinda Serikali ya Tanzania Mahakamani , baada ya kupangua mashitaka ya uongo yaliyotungwa na RPC wa Mbeya Ulrich Matei na washirika wake ya kusafirisha na kusambaza Madawa ya kulevya , leo amehudhuria Kongamano muhimu la Katiba (Katiba day) ambapo wameonekana watu mbalimbali wengi wakiwa ni akina mama Wakitokwa na Machozi , ikiwa ni ishara ya kumhurumia .

Mdude au Martin Luther kama anavyoitwa na vijana wa kileo , ambaye amepewa nafasi ya kusalimia Wajumbe hao aliwekwa selo kwa siku 414 kwa kesi ya uongo ili kumkomesha kutokana na itikadi yake ya kisiasa .

BAVICHA_&_CHASO_(@bavicha.tz)_posted_on_Instagram:_“Mdudeeeeeeee!!_✌️✌️✌️”_•_Jul_1,_2021_a...jpg

Instagram(1).jpg

Instagram(2).jpg

John_Heche.’s_Instagram_profile_post:_“Kongamano_la_katiba_mpya_leo_Dar”%22_.jpg
 
Kwakweli Mdude alitekwa mara kadhaa kabla ya kubambikiwa kesi ya kutoa Madawa ya kulevya Afghanistan na kuja kuyasambaza Mkoa wa Mbeya

Kama Nchi Huru tulifika pabaya sana Mungu katuletea Raisi Samia tunamuona kama Lulu ing'arayo.
 
Katiba Mpya ni muhimu sana, uwepo wa Mdude kwenye hilo kongamano ndio kunachagiza zaidi upatikanaji wa Katiba Mpya.

Hatuwezi kama taifa kuendelea kuishi kwa kutegemea hisani za viongozi wa CCM, akiwepo mbaya aonee raia, akiwepo mwenye huruma ndio raia wapate afadhali, hili lazima liondoshwe.

Tujiulize, kama leo Magufuli bado angekuwa Rais wa hii nchi, Mdude angekuwa wapi kwa jinsi mahakama zetu zilivyokuwa zimeshikwa na ikulu? ni wazi, Mdude angekuwa anatumikia kifungo wakati huu tena kwa makosa ya kubambikiwa.

Tuamke sasa, wakati ndio huu, Katiba Mpya ni lazima ipatikane ije kutuweka huru kwenye nchi yetu, irudishe usawa wa raia kwenye taifa letu bila kujali itikadi, rangi, wala dini zetu, na rasilimali za nchi yetu zitunufaishe sote sio kikundi kidogo cha watu pekee wanaolindana.

Wale wote wanaopinga upatikanaji wa Katiba Mpya ni wanyonyaji wanaoishi kwa kunywa damu za watanzania wenzao (zombies), akili zao bado zimelala, tusichoke tuendelee kuwaamsha wala tusiogope eti tutalala sisi, wataamka tu, kwa sababu Katiba Mpya itakuwa kwa manufaa yao pia.
 
Kwakweli Mdude alitekwa mara kadhaa kabla ya kubambikiwa kesi ya kutoa Madawa ya kulevya Afghanistan na kuja kuyasambaza Mkoa wa Mbeya

Kama Nchi Huru tulifika pabaya sana Mungu katuletea Raisi Samia tunamuona kama Lulu ing'arayo.

Mdude akiweza kuacha matusi na lugha za kuudhi kwa viongozi wakuu wa serikali anaweza kuja kuwa mwanasiasa mzuri
 
Usanii ni nini ?
Sasa hivi hao jamaa mataga huwa wanaongea tu
Mdude akiweza kuacha matusi na lugha za kuudhi kwa viongozi wakuu wa serikali anaweza kuja kuwa mwanasiasa mzuri
Mdude kama angekamatwa kwa kosa la kutukana hapo tungesema amestahili lakini unamtumia watu wamteke na kumtesa kisha unambambikia kesi ya uongo ni ujinga wa hali ya juu wa Dikteta yule
 
Ngoja tuone mama naye akizingua kama ataanza kuporomosha matusi. Mdude ni mwanaharakati mzuri lakini sijui alikuwa anapata faida gani kuporomosha matusi non stop. Kwa matusi yale hata sasa akianza kumtukana mama laivu namna hiyo watamkamata tena.
 
Back
Top Bottom