Katiba Mpya ni muhimu sana, uwepo wa Mdude kwenye hilo kongamano ndio kunachagiza zaidi upatikanaji wa Katiba Mpya.
Hatuwezi kama taifa kuendelea kuishi kwa kutegemea hisani za viongozi wa CCM, akiwepo mbaya aonee raia, akiwepo mwenye huruma ndio raia wapate afadhali, hili lazima liondoshwe.
Tujiulize, kama leo Magufuli bado angekuwa Rais wa hii nchi, Mdude angekuwa wapi kwa jinsi mahakama zetu zilivyokuwa zimeshikwa na ikulu? ni wazi, Mdude angekuwa anatumikia kifungo wakati huu tena kwa makosa ya kubambikiwa.
Tuamke sasa, wakati ndio huu, Katiba Mpya ni lazima ipatikane ije kutuweka huru kwenye nchi yetu, irudishe usawa wa raia kwenye taifa letu bila kujali itikadi, rangi, wala dini zetu, na rasilimali za nchi yetu zitunufaishe sote sio kikundi kidogo cha watu pekee wanaolindana.
Wale wote wanaopinga upatikanaji wa Katiba Mpya ni wanyonyaji wanaoishi kwa kunywa damu za watanzania wenzao (zombies), akili zao bado zimelala, tusichoke tuendelee kuwaamsha wala tusiogope eti tutalala sisi, wataamka tu, kwa sababu Katiba Mpya itakuwa kwa manufaa yao pia.