Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MsimaliMtaje jina Waziri huyo tumpelekee kete zake aendelee kuzimua kwa moshi
kamataja kuwa ni basheMtaje jina Waziri huyo tumpelekee kete zake aendelee kuzimua kwa moshi
ulizwa hayo maswali anabaki kupandiaha majini ya kisomaliHiv ule mradi wake wa vijana umefia wapi? Maana baada ya pesa kutoka tu na watu wakazila sasa hivi kimya.
Bashe bado waziri mpaka dakika hii kwa misingi gani? Mnaona Mungu anavyowaumbua, wanajiropokea wanayoyapanga huko kwa siri.View attachment 3093770
Serikali huenda ikasitisha kupeleka huduma za kilimo kwa wakulima wa jimbo la Kisesa, wilayani Meatu, mkoani Simiyu endapo wakulima hao wakiithibitishia serikali kuwa tuhuma zinazowasilishwa mara kadhaa na Mbunge wa jimbo hilo Luhaga Mpina (CCM) kwenye sekta ya kilimo ni sehemu ya maagizo yao
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe Septemba 11.2024 wakati akiwa kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi anayoifanya wilayani Igunga, mkoani Tabora ambapo amesema Mbunge huyo mara kadhaa amekuwa akitoa tuhuma kuwa pembejeo (dawa) za kilimo na mbegu za mazao mbalimbali zinazopelekwa na serikali kwa wakulima kuwa ni feki, sambamba na hilo amesema Mbunge huyo pia amekuwa akidai wanunuzi wanaopelekwa kununua mazao ya wakulima wanatoa bei ndogo
Kufuatia madai hayo, Waziri Bashe amesema hivi karibuni anakusudia kwenda kufanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na wakulima wa jimbo la Kisesa ambapo atawaeleza kuwa endapo kinachozungumzwa na Mbunge Mpina ni sehemu ya maagizo yao basi serikali haitapeleka pembejeo za ruzuku, mbegu na hata wanunuzi, ili kutoa nafasi kwa Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga Mpina kuwapelekea wapiga kura wake pembejeo na mbegu anazoziona kuwa bora kuliko zile zinzoletwa na serikali na kisha baada ya mavuno anunue mazao hayo hususani zao la Pamba ambalo wakulima wengi jimboni humo wanalima
"Nchi yetu tumejenga utamaduni wa watu kutuhumu bila kuleta suluhisho la matatizo, sasa hilo sio kwenye sekta ninayoisimamia mimi (sekta/wizara ya kilimo), kwa hiyo nitaenda Kisesa wakaniambie wakazi wa Kisesa kama yale mawazo ni ya kwao serikali itaondoa, lakini kama yale mawazo ni ya Mpina serikali itaendelea kuwahudumia, kwa sababu lazima tufike mahali tuweke siasa pembeni kwenye maisha ya watu, na mimi hili nimeamua kama mbaya na iwe mbaya" -Bashe
Amesema wale wote wenye dhamira ya kudhoofisha jitihada za serikali kwenye maeneo mbalimbali wasichezee sekta ya kilimo kwa kuwa kiuhalisia watu wamewekeza kodi za wananchi, muda na nguvu
Aidha, Waziri Bashe ametoa rai kwa wakulima wa Pamba nchini kuendelea kulima zao hilo kwa kuwa serikali haiwezi kuleta wanunuzi wezi (wanaowanyonya wakulima), sambamba na hilo amesema serikali haiwezi kuwaletea wakulima dawa (pembejeo) na mbegu feki
"Hatuwezi kujenga Taifa ambalo mtu anaamka tu anatukana watu asubuhi, mchana, jioni, hawa wanunuzi wa Pamba hawa mwaka 2019/2020 mnakumbuka tulivyoteseka kununua Pamba nchi hii, watu wakaenda wakafanya siasa wakasema Pamba haiwezi kuuzwa chini ya 1200 Pamba si zilidoda hapa?, si mlikopwa mnakumbuka?, si ilikuwa mateso?, wao walikuwa na shamba hata hekari moja?, sasa siruhusu huo mchezo kwenye sekta ninayoisimamia na namaanisha katika hili" -Bashe
Katika siku hiyo ya kwanza ya ziara yake ya kikazi wilayani Igunga, mkoani Tabora Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amekutana na viongozi wa Bodi ya Pamba, wafanyabiashara, wawekezaji na wakulima wa Pamba
Sambamba na hilo amezindua mpango wa kitaifa wa kuongeza tija katika uzalishaji wa Pamba katika kijiji cha Mbutu wilayani humo, sambamba na kutumia fursa hiyo kueleza mipango ya serikali ya kujenga mabwawa na miundombinu ya umwagiliaji ya kutosha na kuwahakikishia wananchi kuwa maji hayatakuwa mateso kwa wakulima wilani humo.
Mjinga sana huyu jamaa,kodi za watz wakiwemo wa kisesa anataka azipangie yeye...... nikwasababu tu ni Tanzania,ila huyu msomali hapaswi kuwepo ofisiniLini amekuwa mkakamavu?
Nani alianzisha huo ugomvi?Bashe acha ujinga ,, Sisi sote tunajua ugomvi wenu NI wa kwenu binafsi na ndio maana unamuattack Mpina personally
Bashe bado waziri mpaka dakika hii kwa misingi gani? Mnaona Mungu anavyowaumbua, wanajiropokea wanayoyapanga huko kwa siri.
Kwahiyo nchi hii, ukiwatetea wananchi wewe ni adui wa ccm, adui wa Serikali? Hiyo kauli ya kuwanyima hiduma wananchi hao, kodi ni zetu wenyewe, halafu kimtu cha somalia kitupangie cha kufanya. Wanatuona nyanya mbichi hawa. Bashe must Go...
Soma vizuri, kasema anaenda kuongea na wananchi wa Kisesa.......kujua ukweli, sasa tatizo nini hapo?Naona kweli TATIZO LA AFYA YA AKILI NI KUBWA🙂
yani mpaka waziri unaongea upuuzi kama huu
Kwamba mpina ndo wananchi
Katika mawaziri anaaminika sana huyo ni bingwa wa sound na takwimu za uongoKazi kweli kweli,
Hivi bado ni Waziri kabisaaa!!!!?
Maneno mengi lakini bado wakulima hali zao ziko vile vile na malalamiko ni yale yale sijui tunapimaje mafanikio katika sekta husika kwenye utekelezaji wa maendeleo ya kweli kwenye kilimo mana bado zaidi ya 70% ya population inategemea Kilimo kwenye maisha yao ya kila siku lakini porojo porojo zimekua nyingi.Na MWANDISHI WETU, IGUNGA
WAZIRI wa Kilimo Mhe. Husein Bashe (Mb) amemtumia salamu Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina kuwa awe na shukrani kwa serikali achezee sekta nyingine sio kilimo ambayo ni tegemeo kwa Taifa.
Amesema chokochoko za uongo za mbunge huyo zinapogusa sekta ya kilimo hawezi kumvumilia, kwa kuwa taifa ni kubwa mno rasiliamali ni chache hivyo jitihada zinazofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan haziwezi kurudishwa nyuma na yeye kukaa kimya.
Amesema amejipanga kwenda Kisesa na kukutana na wakulima, ili kujua mbivu na mbichi kama mbwai na iwe mbwai kwani hataki utani na uongo katika sekta hiyo inayogusa maisha ya watu.
Waziri wa Kilimo Mhe. Bashe amesema hayo mara baada ya kuanza ziara ya kikazi katika wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora ambapo ameanza kwa kukutana na viongozi wa Bodi ya Pamba, Wafanyabiashara, Wawekezaji na Wakulima wa Pamba.
Pia amezindua Mpango wa Kitaifa wa kuongeza Tija katika Uzalisha wa Pamba katika Kijiji cha Mbutu wilayani humo.
Amesema “Watu hawalali usiku na mchana kutafuta suluhisho kwa sekta hii, yeye alipewa nafasi alifanya nini, ni kweli haoni mabadiliko makubwa yaliyofanywa na serikali”?
“Serikali haiwezi kuwaletea wakulima wanunuzi wezi, dawa feki na mbegu feki Kisesa nakuja mtanijibu sitaki utani katika kilimo mshambulie Bashe sio hii sekta hatuwezi kuwa na taifa linatukana watu linatukana serikali tunakaa kimya”
“Watu walikuwa na mateso walikopwa, pamba zilidoda sitaruhusu mchezo wa siasa sekta ninayoisimamia, msiwe na hofu miaka miwili tumetoa ruzuku ya mbolea bure na tutaendelea kufanya hivyo na tutaendelea kununua mazao,”alisema.
Soma Pia: Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
Bashe amesema, “Katika shughuli za uzalishaji na uchumi mimi sifanyi siasa yeye alikuwa Waziri kwa zaidi ya miaka 20 kule Kisesa nitaenda kufanya mkutano na kuwambia wana Nzengo kuwa mbunge wemu kasema dawa za serikali feki mbegu feki na wanunuzi wanawaibia serikali.
“Tunampa nafasi alete dawa, mbegu na kununua pamba nchi yetu tumekuwa na tamaduni ya kuacha mtu anachafua serikali na hana suluhisho, naenda Kisesa tutawauliza wakulima kama yale mawazo ni ya kwao serikali tutaondoa huduma kama ni ya Mpina tutaacha….achezee sekta nyingine sio kilimo mimi nimezaliwa uswahili kama mbwai mbwai nimeamua,”alisema.
Ameongoza kuwa “Mimi ndio Waziri wa Kilimo, mimi sio wale ambao una itest serikali tena kwa uongo halafu wizara inakupigia magoti,”alisema
Waziri Bashe ametumia fursa hiyo kueleza mipango ya serikali ya kujenga mabwawa na miundombinu ya umwagiliaji ya kutosha Igunga na kuwahakikishia wananchi kuwa maji hayatageuka mateso kwa wakulima wilayani humo .
Amesema anatambua kilimo cha pamba kinavyofanya vizuri Wilayani Igunga ambapo kitakwimu ni ya kwanza au ya pili, hivyo ni lazima kuwa na uzalishaji wa uhakika kwa kujenga mabwawa ya maji.
Amesisitiza kuwa, serikali imegawa trekta 500 powatila 800 kwa nchi nzima lengo ni kuimarisha sekta ya kilimo.
Soma Pia: Luhaga Mpina: Usambazaji wa sukari haukuwa ukifanywa na mfanyabiashara mmoja wa Mwanza pekee, Waziri Bashe alidanganya
Aidha ili kufikia malengo hayo, ni lazima kukubaliana kuwa ni marufuku kuzalisha kwa kutegemea maoteo na atahakikisha kinajengwa kituo cha wakulima kupewa elimu, kuendelea kugawa mbegu na dawa bure kama alivyoelekeza Rais Dk. Samia.
Amesema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa na ana nia ya dhati ya kuinua Sekta ya Kilimo, hivyo ni wakati wa Halmashauri nchini kuwa sehemu ya kutekeleza maono hayo kwa kuinua uchumi.
“Juhudi hizi zinazofanywa na Serikali ni chachu kwa Halmashauri na Wilaya kuamka ili kusaidia kuondoa umaskini. Serikali za Wilaya na Mikoa mna wajibu wa kusimamia mabadiliko haya, tunaleta kwenu Maafisa Ugani ili waje kuwa chachu ya mabadiliko katika Sekta ya Kilimo, watumieni ipasavyo,” amesema Mhe. Waziri Bashe.
Aidha, Mhe. Waziri Bashe amesema Maafisa Ugani hao wahakikishe kila Kata kunakuwa na zao la uzalishaji lenye matokeo ya baadaye katika kijiji.
“Lazima tupimane kwa matokeo ya kiuchumi, katika suala la uzalishaji tusiruhusu siasa. Zao hilo ni muhimu sana katika uchumi kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa,” amesisitiza
Mhe. Waziri Bashe. Akitoa taarifa ya utendaji, Bw. Marco Charles Mtunga, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba amesema kuwa ziara hiyo ni muhimu kwa Wilaya ya Igunga kwa kuwa inazalisha zao la Pamba kwa kiasi cha takribani tani 22,000 hadi 26,000.
Ameongeza kuwa hatua ya Wilaya hiyo kuwezeshwa zana bora za kilimo, mafunzo na kupatiwa Maafisa Ugani itakuwa na uwezo wa kuzalisha hadi tani 100,000 ambapo kwa kila mkulima ni wastani wa uzalishaji ni kilo 300 (ambayo ni tani 0.3).
Kwa sasa, zao la Pamba nchini linazalishwa kwa tani 284,000 ambapo malengo ya nchi ni kuwa na uzalishaji wa tani 500,000.
Mkutano huo wa awali, ulihudhuriwa pia na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Cornel Magembe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge na Mkuu wa Wilaya wa Igunga, Mhe. Sauda Mtondoke.
Aidha, Mhe. Cornel Magembe, amesema Mkoa wa Tabora upo salama na wanamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kupata msaidizi wa kweli wa Wizara ya Kilimo.
“Zao la pamba ndiyo limetufikisha hapa, uchumi wa Mkoa unategemea zaidi zao hilo na tunayo nafasi ya kurudisha zao la pamba kwa kufanya Kilimo cha kibiashara,” amesema Mhe. Magembe.
Amen 🙏Luka 12:2-4
Neno: Bibilia Takatifu
2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi.
Wanavisasi ndo maana vita haviishi nchini kwaoWanànchi wa kisesa wameikosea Nini serikali?
Kwani hawalipi Kodi Kama wengine? Kwani Kodi Yao haiendeshi serikali?
Wasomali especially wakimbizi Wana akili finyu Sana. Wanawaza Vita na visasi vya kiKoo visivyoisha.
Bashe msomali awe rais?Wanavisasi ndo maana vita haviishi nchini kwao
Mbaya zaidi kuna watu wanataka awe Rais bashe ni mtu hatari sana
Bado huwezi kutishia kupeleka huduma kisa matatzo yako ma mbungeSoma vizuri, kasema anaenda kuongea na wananchi wa Kisesa.......kujua ukweli, sasa tatizo nini hapo?