Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

Pamoja na elimu bure ila yaonesha bado kuna uelewa mdogo sana miongoni mwa watanzania
 
Alichosema Bashe

Akizungumzia suala hilo wakati akielezea
2936744

Hussein Bashe, rudi unyooshe maelezo! Umerusha lawama wa NGO.

Mkuu wa Mkoa wa D'salaam alilipishwa kodi na kupewa onyo kali kwa kupokea ama kuleta misaada ya madawati kwa niaba ya nchi. Serikali ikatoa tamko zito, hakuna kiumbe wala taasisi nje ya wizara ya mambo ya nje yenye kibali nchi hii cha kupokea chochote na lolote kwa niaba ya nchi . Sasa ni toka lini NGO zinaleta au zinapokea misaada ya nchi kwa niaba ya serikali ???????

Kama kuna ruksa basi rudini mkamuombe msamaha Paul Christian Makonda - give the devil his due - kwa kuleta misaada ya madawati bila serikali kuhusika kama walivyoruhusiwa hawa NGO wa michele ya virutubisho.
 
Kawaambia NGO? NGO ndiyo inaamua pesa za kodi za Wamarekani ziende kwa Wakulima wa Marekani au ziende kwa Wakulima wa Tanzania? Huo ni msaada. Take it or leave it. Aaiambie hiyo NGO warudishe mzigo wao wa mchele Marekani badala ya kuzungumza maneno mengi yasiyo na mantiki wala uhalisia. Anazungumza kama Waziri kwa niaba ya Watanzania wote kwenye hafla ya futari Msikitini?
 
2936744

Hussein Bashe, rudi unyooshe maelezo! Umerusha lawama wa NGO.

Muu wa Mkoa wa D'salaam awamu ya tano alilipishwa kodi na kupewa onyo kali kwa kupokea ama kuleta misaada ya madawati kwa niaba ya nchi. Serikali ikatoa tamko zito, kwamba hakuna kiumbe wala taasisi yenye kibali nchi hii cha kupokea chochote kwa niaba ya nchi. Sasa ni toka lini NGO zinaleta au zinapokea misaada ya nchi kwa niaba ya serikali ???????

Kama kuna ruksa basi rudini mkamuombe msamaha Paul Christian Makonda kwa kuleta misaada ya madawati bila serikali kujua kama walivyoruhusiwa hawa NGO wa michele ya virutubisho.
Msomali anaenda na upepo
 
Tena angekuwa uncle Magu viongozi wa hiyo NGO wangekula mboko, wanataka kutuulia kizazi chetu shupavu. Hii nchi ina watu wa hovyo sana, ilitakiwa wapewe masaa kadhaa huo mchele uwe umechomwa na TBS
Acha upunguani! Umejuaje? Tena huenda angepeleka na mwingine nyumbani kwake. Usipende kukariri maisha, watu hubadilika, hata wewe wa mwaka juzi na wewe wa saivi ni watu wawili tofauti. Usipende kukariri as if magu alikuwa malaika
 
Kwa uwezo wako wa kufikiria, unadhani tz tunahitaji msaada wa mchele, maharage n mafuta?? Vipi wasomali, palestines, Nigerians, Ukrainians...
Kwa fikra zako kwa stories za kuambiwa, kujisomea n uwezo wako wa kufikiria, unadhani America wana mapenzi hayo kweli ya dhati kwa watz?? Tukirudi kwenye historia, America amewahi kulisaidia taifa gani bila kuwa na agenda yeyote iliyojificha??
Hivi hujui uko Palestine kila kukicha sio chini ya watu 40 wanakufa kwa njaa? Kwanini asipeleke chakula chake kwenye taifa lenye uhitaji anatuletea uku ambapo tunategemewa na mataifa jirani tuwauzie mazao yetu ya ziada? Hatuna maendeleo kama yao, ila wasituone sisi maboya kiasi hiki.
Watanzania wengi bado ni masikini sana sawa tu na Wapalestina, Wasomalia au Wa-Ukraine walio vitani. Wanauhitaji sana huo msaada wa chakula wa Marekani, sio wanafunzi mashuleni tu, hata mtaani kwako Wamarekani wakija na hiki chakula utaona mafuriko ya watu wakigombania chakula.
Achana na hizo story za kujishaua kwamba tunazalisha sana, raia wengi sana bado wana njaa ya mchele na pia Samaki, soya, nyama na mayai bado ni vitu vya anasa kwao.
 
Kiburi chanini wakati watoto wetu wanaanguka njaa mashuleni huku walimu wakipepesuka kwa njaa??

Wizara ipime kama Mchele hauna shida upelekwe mashuleni, Mchele wenyewe bei ghali shule gani inaweza kununua ikalisha watoto wake???

Waziri anakaa Dar anaamini watuwote tunakula Kila tunapojiskia...huku vijijini kunawatoto hupigwa kipigo kikali kisa kudokoa wali kutokana na njaa kali waliyonayo. Tunakula mlo mmoja tuu labda siku ya bahati ndiyo tule milo miwili.

Msiweke kiburi kisa ninyi mnakula mnashiba na kuvimbiwa, chamuhimu Mchele unaenda liwa shule ambamo hawawezi nunua Mchele wetu ambao bei ni yajuu.

Nilini tutapata viongozi wazalendo wenye akili nzuri na wanaojua nchi yao na watu wake wanavyoumia hasa huku vijijini??
Hopeless leaders kabisa!!
Homeless wa kule mbona hawaonei huruma. Chakula bongo kingi sana. Walete hizo pesa tununue kyela wakapewe dodoma
 
Kuna watu wanaleta uzalendo uchwara tu bila kujua kuna familia kila siku zinalala wakiwa hawajui kesho itaishaje, hata kupata ugali na dagaa au maharage tu ni tatizo.
 
Homeless wa kule mbona hawaonei huruma. Chakula bongo kingi sana. Walete hizo pesa tununue kyela wakapewe dodoma
Nani kakuambia Homeless wa kule hawaonewei huruma?? Unafahamu chochote kuhusu housing projects?
 
Back
Top Bottom