Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

Wewe pia huelewi nahisi ulikuwa unakuwa wamwisho darasani.
Haijasemwa mahali Tz hatuna chakula...watoto wameteseka njaa miaka na miaka, msamaria kawaletea chakula Toka chanzo rahisi kwake fungua ubongo usijidai tajiri wewe nimaskini wakutupaaa!
Watoto wanaanguka njaa wape Sasa chakula wewe au unataka wafe,kama wamelia shida wameletewa uliza viongozi wako kwanini wanakuwa wajinga KIASI hiko.
Nikimtumia mtu mwenyeshida ya mchele dar toka shinyanga inamaana dar kuna njaa??
Elewa viongozi wa taifa lako ndiyo wanapaswa kubeba aibu ya kushindisha watoto wetu njaa mashuleni huku wakifanya kazi ngumu yakusoma!!! Viongozi wanatembelea V8 watoto shule wanaanguka njaa where is your hearts??
Wewe hujielewi unatetea viongozi kijiiinga bashe ninani yako? Waziri mkuu ajiuzulu Kwa kushindisha watoto njaa mpaka marekani wanasikitika wanawaletea watoto chakula!! Heartless idiots
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣.
Unafurahisha sana we jamaa.
Still we bado huelewi halafu unaandika mambo mengi yasiyohusika.
-Sikumtetea Bashe,labda uoneshe sehem ni wapi nimemtetea Bashe au serikali,ndio maana nikasema serikali INATAKIWA IWAJIBIKE MAANA TANZANIA HAKUNA UHABA WA CHAKULA KIASI TUPEWE MSAADA WA CHAKULA.Kwa hii kauli inaonesha nimeikosoa serikali na ndio maana nikaongezea kusema kuwa sio kila msaada wa kupokelewa Tz hatuna shida na msaada wa chakula serikali ijitizame.
-Nimeupinga huo mchele kwakuwa unasemekana umetiwa virutubisho na asilimia kubwa ya vyakula wanavyotoa hawa jamaa ni GMO vina madhara yake baadae kadri unavyotumia hivi vyakula.
Pia nikakuuliza je,huo msaada wa huo mchele ndio suluhishi ya kukomesha njaa shuleni??
We jamaa aisee embu kuwa muelewa.
 
Aliulizwa Obama kitugani huku fanikiwa ktk uongozi wako na unaumia kutofanikisha alijibu kuwa"ni kutopatikana kwa chanjo ya cancer wakati mamilion ya Wamarekani wakiangamia kwa mwaka".ni kweli ocean road wagonjwa wa cancer wapo lakini huwezi linganisha rate ya cancer Tanzania na first world countries Sababu ni Nini Sasa?
Ni vyakula vya GMO madaktar wengi wameeleza hili wew kama sio daktar au expert wa mambo ya afya huna la kusema ktk hili
Kama unaowatoto wape vyakula hivyo uje uone matokeo yake.
Nakupa mfano mwepesi kuku wa kisasa anaingizwa sokoni akiwa na wiki Tano Hadi sita lakini kuku wa kienyeji wa umri huo huwezi mleta sokoni... Mmesha tengeneza miili ya kisasa kama kuku wa kisasa bado hamjatosheka mnataka na watoto wasio na hatia wasiojua lolote mharibu miili Yao,lakin hukumu yenu ipo(1korinthi 3:16-17)
Nchi kama Tanzania inashindwa kulisha watoto mlo kamili?
1 peeled grape fruit
1peeled orange
3 stalks celery
Couple of mint leave
Hence take 1 glass×3
Hiyo inasaidia kuongeza vitamin C mineral and nutrients.
Sasa mambo kama haya Hadi uletewe na Wamarekani?
Ninyi ndio mnaofanya waafrika tutukanwe na akina Trump
Soma kitabu Cha Dr TAMARA St.JOHN M.BA "Healing through detox"
Cancer inaendena na maendeleo kwa sababu ya lifestyle, umri na upimaji unaotokana na huduma za afya bora.

Nchi zilizoendelea watu wake wana pesa hivyo wanakunywa sana pombe na kutumia bidhaa nyingine nyingi ambazo zinasababisha kansa.

Kansa inaathiri sana pia watu wenye umri mkubwa na wazee ndio maana nchi kama Japan kuna kiwango kikubwa cha kansa, Waafrika wengi wanakufa wakiwa na umri mdogo.

Nchi zilizoendelea watu wanapima sana afya zao na kansa nyingi zinatambuliwa hospitalini tofauti na nchi zetu masikini.
 
Dar es Salaam. Saa chache baada ya kuibuka kwa mjadala katika mitandao ya kijamii juu ya mchele ulioongezwa virutubisho ulioletwa Tanzania kutoka nchini Marekani, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amefunguka akisema waagizaji hawakupaswa kuleta mchele huo kutoka nje, kwa kuwa Tanzania ina hazina ya mchele.

Akaongeza kuwa kama ni virutubisho, bado shirika lililoagiza mchele huo lingenunua mchele wa ndani na kuwaomba wafadhili wao wauongezee virutubisho hapahapa nchini, huku kila mtu akiona kuliko kuagiza kutoka nje ya nchi.

Mjadala wa mchele huo ulianzia katika mtandao wa X, baada ya ukurasa wa Ubalozi wa Marekani kuweka picha iliyokuwa ikionyesha viroba vya mchele huo, huku ikiambatisha na ujumbe uliosomeka:

"Chini ya mpango wa 'Pamoja Tuwalishe', Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, imetoa msaada wa kwanza wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani moja kwa moja hadi shuleni katika eneo la Dodoma nchini Tanzania."


Ujumbe huo uliendelea kueleza kuwa msaada huo unalenga zaidi kutoa milo yenye lishe kwa wanafunzi wa shule zaidi ya 300 zinazoshiriki, huku ukieleza kuwa mbali na mchele huo, pia wataanzisha bustani za shule na kufunza mbinu za kuvuna.

Alichosema Bashe

Akizungumzia suala hilo wakati akielezea miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan na yale aliyoyafanya katika sekta ya kilimo, Bashe amesema Tanzania inazalisha mchele na maharagwe kwa kiwango cha kutosha.

"Tumewaambia ile NGO, waambieni Wamarekani kuwa mchele upo maharagwe yapo nchi hii, zile fedha wanazotumia kuwapa wakulima wa Marekani wawape Watanzania. Tununue mchele kutoka Tanzania, maharage kutoka hapa Tanzania, halafu hivyo virutubisho mnavyotaka kuweka muwekewe hapahapa Tanzania wote tunaona," amesema Bashe na kuongeza kuwa ameieleza NGO hiyo kuwa Tanzania inajitosheleza kwa chakula.

Maoni mtandaoni

Elisha Mbise alitoa maoni yake katika ujumbe ulio katika ukurasa wa Ubalozi wa Marekani akiandika: "Tanzania tuna chakula cha kutosha...mchele umejaa kila mahali. Walete vitu vya maana, wajenge maabara, walete vifaa vya hospitali, vifaa vya kufundishia, vyuo vya ufundi. Hivi ndivyo vitu vinavyoweza kugusa elimu na afya kama kweli wana nia na kusaidia hayo maeneo.’’

Naye Dani Zayumba aliandika: "Tanzania hatuhitaji chakula cha misaada bali tunahitaji mabadiliko ya mitalaa ya elimu, ili tuweze kujilisha wenyewe. Mnaweza kufananisha mchele wa Mbeya na Marekani kweli?’’

Credit: Mwananchi digital

View attachment 2936741

Hapo awali Balozi wa Marekani ukiandika kwenye Mtandao wa X Kwamba, "Chini ya mpango wa 'Pamoja Tuwalishe', Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, imetoa msaada wa kwanza wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani moja kwa moja hadi shuleni katika eneo la Dodoma nchini Tanzania. Zaidi ya kutoa milo yenye lishe, wanafunzi katika shule zaidi ya 300 zinazoshiriki, pia wataanzisha bustani za shule, na kujifunza mbinu za kuvuna maji ya mvua. Ikiwa ni mfano kamili unaoweza kuigwa, programu hii inaakisi ahadi na dhamira ya dhati ya Marekani ya kukuza afya, elimu, na fursa kwa watoto kote ulimwenguni."
View attachment 2936743View attachment 2936744
Waziri wa Kilimo bado hajasema. Kwani kibali kilitolewa na nani. Utaratibu wa kuingiza bidhaa kama chakula nani anashughulikia. Ni namna gani tunalinda soko la ndani kwa mazao tunayo zalisha ndani
?
 
Halafu baada ya miaka kadhaa watoto wetu waanze kukataa jinsia zao [emoji3]
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣.
Unafurahisha sana we jamaa.
Still we bado huelewi halafu unaandika mambo mengi yasiyohusika.
-Sikumtetea Bashe,labda uoneshe sehem ni wapi nimemtetea Bashe au serikali,ndio maana nikasema serikali INATAKIWA IWAJIBIKE MAANA TANZANIA HAKUNA UHABA WA CHAKULA KIASI TUPEWE MSAADA WA CHAKULA.Kwa hii kauli inaonesha nimeikosoa serikali na ndio maana nikaongezea kusema kuwa sio kila msaada wa kupokelewa Tz hatuna shida na msaada wa chakula serikali ijitizame.
-Nimeupinga huo mchele kwakuwa unasemekana umetiwa virutubisho na asilimia kubwa ya vyakula wanavyotoa hawa jamaa ni GMO vina madhara yake baadae kadri unavyotumia hivi vyakula.
Pia nikakuuliza je,huo msaada wa huo mchele ndio suluhishi ya kukomesha njaa shuleni??
We jamaa aisee embu kuwa muelewa.
Fact tatu in a nutshell...
1.) Waliotoa msaada wasilaumiwe wametusaidia Kwa miaka na miaka na haijathibitishwa kuwa wametupa kisichofaa.
2.) Shida ya chakula tunayo maana watu wengi hawawezi kununua hicho chakula mashuleni ndiyo kabisaaa. Sikuizi wahisani wanatoa vitu sio Hela... mkipewa Hela hazifiki kwawatoto.
3.) Ukiwa maskini punguza kiburi kitu hukitaki pakia ukirudishe usimchafue anayekusaidia kisa siasa za kijinga.
Sijui unaeleweka??
 
Kwa nini huo msaada wa chakula hawajapeleka kwenye nchi ambazo zimepigwa na njaa kama somalia ambako watoto wanakufa kwa utapia mlo huko ndio wanahitaji lishe sio hapa Tanzania, yani wanataka kusema kwamba hata swala la lishe na lenyewe tumeshindwa hadi tupewe msaada 🤔🤔 haya ni matusi, Kuna walakini mkubwa kwenye huo msaada usiokua na maana waupime vizuri wasije kuingiza watoto matatizoni tena ikiwezekana urudishwe ulikotoka
Wanataka kuongeza idadi ya machoko
 
Kwani vibali vya kuingiza mchele vilitoka wapi kama vilitoka kupitia ofisi yake
 
Mkuu umeshatembea huko vijijini ukawaona watoto wanavyoteseka na njaa na walivyodumaa. Lishe duni ni tatizo kubwa Tanzania. Kama wewe na watoto wako mnajitosheleza hapo ulipo shukuru Mungu, kuna watu huko hawajui mchana watakula nini. Cha msingi hapo Serikali ijiridhishe usalama wa hicho chakula kama Kipo Sawa mm sioni shida. Mchele na chakula kilichopo tz ni Kwa wanaojiweza Tu.
Serikali ishughulike nao hao wasio kuwa na chakula na sio msaada toka marekani
 
Fact tatu in a nutshell...
1.) Waliotoa msaada wasilaumiwe wametusaidia Kwa miaka na miaka na haijathibitishwa kuwa wametupa kisichofaa.
2.) Shida ya chakula tunayo maana watu wengi hawawezi kununua hicho chakula mashuleni ndiyo kabisaaa. Sikuizi wahisani wanatoa vitu sio Hela... mkipewa Hela hazifiki kwawatoto.
3.) Ukiwa maskini punguza kiburi kitu hukitaki pakia ukirudishe usimchafue anayekusaidia kisa siasa za kijinga.
Sijui unaeleweka??
-Waliotoa misaada (USA) hakuna asiyejua kama misaada yao mingi ilikua ya maumivu na masharti mengi.
Ukitaka mifano naweza kukuletea,labda kama utakua mgeni nao hao majamaa sio tu Tz bali ulimwenguni.
-Tanzania hatuna shida ya chakula,UNAPOSEMA KUNA SHIDA YA kitu INAMAANA KUNA SCARCITY YA HIKO KITU,TANZANIA HATUNA FOOD SCARCITY,ila mifumo yetu haijakaa kiwajibikaji ili raia waweze kunufaika.Kuhusu hili nakupinga mpaka kesho.Sema Tanzania kuna sehemu wana shida ya chakula ila sio kwamba Tanzania kiujumla ina shida ya chakula.
-Kuhusu upande wa siasa huko sikujihusisha na siko huko mie nimeeleza uhalisia unaotakiwa kuelezeka.
 
Watuchezee sisi tuliokomaa lakini sio Watoto wetu.
 
Huo msaada unaweza kuwa na walakini !
Hata chanjo ya korona kuna Baadhi Zina matatizo.
 
We ushtuki tu mchele uongezwe virutubisho ili iweje?wawapelekee wasonja au huko Zambia watu wana njaa kufa mtu.
 
Asante Wamarekani kwa kulisha wanafunzi wetu mashuleni chakula bora
Mkuu kwanini Serikali wasiweke utaratibu wa kutoza kila shilingi mia kwa watumishi binafsi na wauma kwenye Mishahara yao na kuwatoza asilimia 10 vyama vya Siasa vinavyo Pata Ruzuku.
Na kwenye timu za ligi kuu nazo zikatwe Makato ya viingilio na Nyumba za Obada nawenyewe watoe fungu la kumi ili watoto wetu wapate chakula mashuleni.
 
Ninakuomba radhi sana Job Lusinde Ndungah

Nakuomba radhi mzee John Malichera

Nawaomba Radhi wagogo wote popote mlipo mimi.mhaya sio mtani wenu kamwe.

Ila SIWATANII NASEMA KWELI

Natafakari kifo cha Hayati John Pombe Magufuli leo nikiwa HYDOM sijafanikiwa kwenda kanisani kumwombea na kwaombea Marehemu wote walio tangulia mbele za haki.

Ewe adhira naomba nikusimulie

Mie ninae andika hapa niliwai bakia nusu nidakwe na polisi nikiwa na fedha feki pale maeneo ya Posta jiji la walenyeku(najua nimekuacha nenda kasome KAMUSI YA 1988 TUKI itakupa maana ya neno ilo).
Aliyeninusuru ni mgogo mmoja alie kuwa omba omba nilimrushia lire zigo la hela na yeye akaingia pahala ambapo usingeweza amini kama anazo yeye.


Natafakari kifo cha Hayati magufuli na uijgwazwaji wa mchele wenye virutubisho kutoka ulaya mpaka ndani ya tanzania
Tena kutoka bandarini mpaka Katikkati ya nchi Dodoma kama sikosei ulianza kusambazwa kwa wagogo.

Najiuliza

Kibali cha kuingiza chakula kinatolewa na wizara ya Kilimo kwa taasisi binafsi

Kwa NG'OS kwa kuwa hawalipi kodi basi upewa kibali na wizara ya fedha kwa ajili ya kuto tozwa kodi
Je wizara kilimo ilijua ili au wizara ya fedha?

Je katika utawala wa Magufuli ilo nalo lingetazwa au linngechukuliwa hatua?
 
Aibu sana

Wote tunaonekana wezi aisee hatuaminiki tena.

Wanajua wakileta hela zitaibiwa zote.
 
Mnalalamika ujinga mtupu mbona tunaagiza ngano nje,sukari nje nk. Mchele bongo bei ghali ndomana huko Dodoma wali kwao ilikuwa ni anasa Sasa wanakuletea kutoka kwao maana ni msaada kwao umewazidia Sasa hapo unalialia Nini...
Waafrika wengi wanaujinga wahali ya juu mmno ukae ukijua kunawatu wanashinda na kulala njaa kwa kukosa chakula Sasa huo Mchele mwingi ukowapi?? SI bei zingeshuka na kilamtu angenunua!! Ujinga sana ninyi
Umeajiriwa huko nini. Ni yupi mbinga angetoa au kupokea
 
Huu ni uwekezaji mkubwa wa Marekani kuzalisha kizazi cha mashoga. Hii nchi imekuwa rahisi sana kuingilika na kila mtu. Nachelea kusema Serikali ni dhaifu sana
Hivi Sisi watanzania ni wakupewa chakula kweli Wakati tunalisha Kenya, South Sudan na wengine
Hata ukiwa mjinga si unaelewa kuna kitu nyuma ya pazia
Bibi mkubwa anafanya kazi ya kuzunguka tu.
Mafuta ya alizeti yamejaa nchi nzima Mnataka Yale ya kuletea watoto wa kiume hamu ya kupandwa
Mmeamua kuangamiza Wanaume kabisa jamani
Kwani HAKI Sawa ni Lazima Wanaume nao waolewe?
Mahindi yamejaa kila upande Nani kusema kuna njaa
Kwa nini Serikali inashindwa kuwalinda wananchi wake? Inaniuma Sana
Viongozi wa nchi mnanunuliwa kama Njugu
Tanzania kitakuwa kitovu cha Mashoga
MTANIKUMBUKA
 
Back
Top Bottom