Hussein Bashe, You are smart, you are potential, liangalie zao la Cocoa Tanzania

Hussein Bashe, You are smart, you are potential, liangalie zao la Cocoa Tanzania

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Mimi sio mpenzi sana wa siasa za watu ila napenda kukiri kuwa so far, kati ya watu ninaowaona wana akili na wanaweza kushika vizuri kijiti kutoka kwa Mama Samia coming 2030 ni Ndug. Hussein Bashe. Ana vision zisizotofautiana sana na Mama Samia hasa kwenye uwezeshaji, uwekezaji na biashara ivo si vibaya Chama changu kikaanza kumuandaa sasa kama alivyoandaliwa Ben Mkapa na Jakaya Kikwete.

Ninamuona Kama mtu smart, mwenye mawazo chanya yenye kujenga biashara na uwezo wa Taifa katika kukamata fursa za dunia hasa kiuwekezaji na kibiashara ambapo huu ndo Mwenendo wa Dunia yetu kwa sasa!

Nirudi kwenye mada, Leo BBC wametoa habari juu ya kilimo cha Cacao Kyela. Nilifika Kyela mwaka jana 2021 nikitokea Mbaba Bay na kusema kweli kuna potential kubwa sana kwenye zao la Cacao ambayo Tanzania Bado hatuja iutilize vizuri. Wakulima hawajahamasishwa kulima zao hili kwa wingi na pia elimu sahihi bado haijatolewa katika kuhakikisha zao hili linalimwa kwa wingi, kwa ubora na kumnufaisha Mtanzania.

Maeneo ya kwetu Nyasa, Ludewa na Kyela yanaonekana yanafaa sana kwa kilimo cha Cacao na yakitumika vizuri kwa wakulima kuhamasishwa kulima kwenye mashamba makubwa kwa ubora ni hakika hata Tanzania tunaweza kuwa na Brand yetu ya chocolate kama nchi zingine.

Naomba kama Serikali inavyoweka mkazo katika kilimo cha chikichi ambacho ingawa kitaliondolea Taifa letu na uhaba wa mafuta na kama Serikali ilivyoanza kuweka nguvu kwenye kuhamasisha watu kulima korosho kufikia kutoa hadi Miti kwa wakulima basi serikali ihakikishe pia unaweka nguvu kwenye zao hili la Cacao. Najua unaweza sana basi fanya hili.

Naamini uwezo unao na utafanyia kazi ushauri wangu.
 
Kwa nini wakulima wanasubiri serikali iweke mkazo ndiyo waanze kulima cacao? Halafu 2030 mgombea rais wa CCM atakuwa ni mkatoliki. Huwa wanabadilisha dini za wagombea wao kila awamu.
 
Kwa nini wakulima wanasubiri serikali iweke mkazo ndiyo waanze kulima cacao? Halafu 2030 mgombea rais wa CCM atakuwa ni mkatoliki. Huwa wanabadilisha dini za wagombea wao kila awamu.
Mimi ni mkatoliki ila siungi mkono kabisa huo utaratibu. Na Bora haujawai andikwa popote
 
Ni potential sana, siku zote anapoongea huwa ana substance. Tatizo ana damu ya kisomali, nauona ugumu wa CCM kulipitisha jina lake.

Yatakuwa yale yale ya Salim Ahmed Salim alivyofanyiwa fitina na wale wahafidhina wa CCM. Hata Samia anasagiwa kunguni humu jukwaani wakisema anao uarabu.

Kuna watu huwa wanajikita kuangalia upande hasi wa mtu na hawajaondoka wote kutoka katika mfumo unaotawala nchi.
 
Ndugu yangu ni kama vile wanasiasa hasa viongozi wakuu wanafanya makusudi kuikwamisha hii mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yaani Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi, hii mikoa kabla haijagawanya kwa sababu za kisiasa ili kuidhoifisha ilijulikana kama the Big Four hasa kutokana na kilimo na kuchangia asilimia kubwa ya kilimo cha chakula na biashara katika uchumi wa nchi.

Sasa badala ya kukazania mazao ya kimkakati ambayo yalikuwa yanalimwa huku sasa mazao haya ya kimkakati yamehamishiwa mikoa mingine na huku kwenye ilikuwa big four hakuna anayetilia umuhimu, kwa mfano mazao kama korosho,michikichi,kakao, kahawa ,chai,mahindi.

maharage huku Nyanda za Juu Kusini miaka ya nyuma ndio yalikuwa nguzo kubwa ,sasa korosho na michikichi inalizimishwa ipandwe Manyoni na wilaya nyingine ambayo ardhi ya huko imeyakataa ,wengi waliopanda mikorosho Manyoni na dodoma wanasaga meno kwani mazao hayo hayastawi kama ilivyo kwa mikoa hii ya Nyanda za Juu Kusini, sishangai hata viongozi wakuu hawafanyi hata ziara za kuona na kuhamasisha maendeleo, ziara nyingi kwa sasa ni mikoa ya Kaskazini,Mashariki , Kusini na Visiwani.
 
Mkuu kuwa serious kidogo basi, kuna mnyamwezi mwenye nywele hizo? acha utani bhana
Kwani nywele zina shida gani? Kina Zacharia Hanspope nywele zao zikoje? Mbona nao ni watanzania?
 
Ni potential sana, siku zote anapoongea huwa ana substance. Tatizo ana damu ya kisomali, nauona ugumu wa CCM kulipitisha jina lake...
Huyu kijana mwanzoni nilimuona kama mtaka madaraka tu lakini kumbe ni kichwa na mchapa kazi mkubwa , ni tofauti na wale watoto wa wenye nchi ambao pamoja na kupewa madaraka bado hawana uwezo wa kiutendaji kama Bashe, viongozi wengi vijana tulionao hawana uwezo bali wanatumia influence za wazazi wao.
 
Maamuzi yake siku zote yanatetea umma wa watanzania. Hao watoto wa wakubwa ukiwachunguza utagundua ni sehemu ya makundi ndani ya Chama.
 
Ndugu yangu ni kama vile wanasiasa hasa viongozi wakuu wanafanya makusudi kuikwamisha hii mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yaani Iringa,Njombe,Ruvuma,Mbeya ,Songwe,Rukwa na Katavi...
Kusema kweli Nyanda za Juu kusini imewekwa Kando sana kwa kipindi kirefu. Survival yao kusema kweli imekuwa ikitegemea sana juhudi binafsi!

Kwenye mikoa yote hii hakuna double road hata moja na wao ndo wazalishaji wa Chakula kulisha Tanzania nzima

SGR imeenda kujengwa kwenda hadi Mwanza ila hawa reli yao ya TAZARA ni mfu wakati ndo mikoa inayopeleka bidhaa na Chakula Malawi, Zambia, Zimbabwe na Congo
 
Unamtafutia matatizo Msomali wa watu.
Unataka akina tarehe 28 na 29 wamuue tu bure.
 
Back
Top Bottom