Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Nimeona baadhi ya maeneo mahindi yameanza kuvunwa hasa mkoa wa Rukwa na nimeona malori kutoka Kenya na wanunuzi karibia wote wanapeleka shehena ya mahindi Zambia na Congo...
Hatukatai watu kuuza nje lakini kwa kuwa maeneo mengi ya nchi hawakulima mahindi ya kutosha na mikoa mingine kama Morogoro mahindi yameharibika mashambani kwa kukosa mvua za kutosha ...

Nakushauri Tena kwamba zuia kwanza mahindi yasiende nje ili tujitosheleze ... au serikali kupitia nrfa iingie kununua kabla hatujabaki na mabua !!

Nakufahamu hupendi kushauliwa na mtu lakini asiesikia la mkuu huvunjika
 
Nenda kalime na wewe ili uje uwauzie wanaoshinda kwenye betting wakisubiri bashe afunge mipaka
 
Hayo mahindi unayotaka nchi ijitosheleze nayo umelima wewe?
 
Mkuu nchi imejaaa wajinga kwa kiwango cha kutisga, unacho swma ni sahihi kabisa, na Zambia wenyewe wampeiga Bun kuuza mahindi nje ya nchi, hili swala lipo sana Duniani huko kwa nafaka zile ambazo hutumiwa na mass,

bashe anacheza na akili za wajinga wa nchi hii, jiulize Zambia kwa nini kazuia? Kwani ni Serikali ndio inalima mahindi kule Zambia?

Bashe ni mjanja mjanja anaye jua kucheza na akili za wajinga wa nchi hii ambao ni % kubwa sana
 
Ungejua tunavyohangaika na kilimo usingesema hivo jombaa. Niuze ndani ya nchi gunia moja elfu 36 anakuja mkenya gunia moja nauza laki 1 na 20 hata kama ni ww unamuzia nani hapo????
India Mwaka jana imezuia kuuza ngano nje unazania walikuwa wajinga? Serikali ya Kenya inavyo sa nchi nyingi zilishindwa kuwauiza mahindi kwa sabababu zina akiba kidogo uliwaza nini?
 
Watu kama huyu mleta mada wana mawazo ya kutoa watu kafara. Kwamba bora mkulima afe na umaskini lakini mfanyakazi anunue chakula kwa bei rahisi. Si ukanunue nafaka zinazokutosha uweke ndani?. Kumbuka mkulima anavyouza mapema ndivyo anavyorudi shambani kuzungusha hela
Your browser is not able to display this video.

Wakulima tuko na Bashe.
 
India Mwaka jana imezuia kuuza ngano nje unazania walikuwa wajinga? Serikali ya Kenya inavyo sa nchi nyingi zilishindwa kuwauiza mahindi kwa sabababu zina akiba kidogo uliwaza nini?
Acha kukimbia hoja???? Je huyo mkulima unaweza fidia gharama aliuzotumia shambani au unapuyanga jombaaa. Kuna mwaka nimelima mahindi napata gunia 60 nikasema nimeuaga umasikini bei ya soko la ndani tukauza elfu 24 gunia kisa kufunga mipaka. Mahindi hayo yalinitesa kukausha mvua zinapiga kila siku.
 
Kama una familia ya kulisha nenda kalime. Usitegemee wengine wakulimie na wakuuzie wewe kwa bei unayotaka, nenda kalime na uuzie familia yako kwa bei unayotaka ama uwape bure.

Ulivyo taahira unataka mimi nilime kwa gharama zangu halafu wewe uje ununue kwa bei ndogo ukalishe familia yako, kalime uwalishe mwenyewe.

Nimelima mwenyewe kwa gharama zangu na nitauza mahala napotaka.

Familia yako inanihusu nini mimi? Walale njaa, wafe njaa mimi nahusikaje? Walikuja kunisaidia kupalilia?

Wakulima wauze wanapotaka kwa bei wanayotaka.
 
hii ni hoja ya kijinga zaidi kwa mwaka 2023, nipo mbozi nanua debe kwa 12000, so acha tununue wakulima wanufaike na kazi yao
 
Mlizoe vyakula kuuzwa bei ndogo mtakoma term hii
 
1.Ardhi IPO 100%,

2. Watu wapo 100%,

3. Ujinga 80%,

4. Uongozi Bora 3%.

5. RUSHWA 98%.

Tukumbuke kuwa Bado shehena ya Kutoka nje Serikali iliyoagiza nje ya nchi Kwa kulipa Dollars haijaweza saidia Bei ya vyakula masokoni kushka Bei.

Ukihoji kwann wanaruhusiwa kuingia kununua direct Kwa MKULIMA tena Kwa Tshs wakati mbolea tumeagiza Kwa Dollars utaambiwa una nongwa na wakulima.

Tusubiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…