Babaviwanda
Senior Member
- Nov 9, 2022
- 111
- 213
Kuna mazao au bidhaa za kilimo zinaingizwa toka nje kila siku mfano ngano na sukari. Juzijuzi tu wakaruhusu Michele pia.Wewe ndiyo hujaelewa sasa. Serikali imeruhusu wafanyabiashara kutoka nvhi jirani kuingia nchini na kununua chakula kutoka kwa wakulima wa ndani kwa bei nzuri! Sina tatizo na hiki.
Changamoto iliyopo ni hii hapa; Kitendo hiki kimesababisha uhaba wa chakula nchini, na hivyo bei ya vyakula kuwa juu! Jambo hili limesababisha ugumu wa maisha kwa wananchi walio wengi.
Ndiyo nimetoa ushauri! Kama wakulima wetu wana uhakika wa kuuza mazao yao kwa bei nzuri kwa wafanyabiashara kutoka nchi jirani, kwa nini sasa wafanyabiashara nao wasiruhusiwe kuingiza chakula nchini ili kupunguza uhaba wa chakula na mfumuko wa bei ya nafaka?
Hayo yanafanywa kwa uangalifu ambao hautaathiri wakulima wa ndani. Uhaba unaosema si mkubwa wa kufanya kila kitu kiruhusiwe kuingia toka nje. Mazao yenye uhaba mkubwa ndio yanaruhusuwa kuagizwa toka nje.
Ndio maana nikakuambia hujaelewa lengo la kumlinda na kumwinua mkulima wa kitanzania. Unachotaka wewe ni unafuu wa mda mfupi kwa watu wachche wa mijini,lakini huoni ni kwanamna gani taifa litanufaika kama mamilioni ya wakulima watainuka na kuwa wakulima wa kisasa na wenye vipato vikubwa.