Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Haya maneno unayoongea ni upumbavu mkubwa sana. Wewe kama hauna familia ya kulisha huwezi kuelewa mleta mada anaongea nini.

Ni siku si nyingi tumekuwa tukinunua nafaka kwa bei ya juu isivyo kawaida sababu ya kuendekeza kuwaachia hawa wachuuzi kununua nafaka na kuuza mipakani. Ni muda wa kuratibu huu uchuuzi wa hovyo.
Kama serikali inaweza kununua mahindi kwa bei ya juu ili kunusuru walaji, kwa nini isitumie pesa hizo hizo kuwapa ruzuku wakulima ili walime kwa bei nafuu na kuuza kwa bei nafuu?
Wakulima wanalima kwa ukiwa na shida tele , wanakuja kuonekana na serikali wanapouza mazao yao tu.
 
Wakulima wauze watakako.

KAZI ya Serikali ni kuhakikisha inadhibiti mfumuko wa Bei za Bidhaa masokoni.

Njia za kudhibiti ni sirikali kununua na kutunza chakula ktk maghala na kuuzia wachuuzi masokoni Kwa Bei nafuu Ili Bei ziendane na vipato vya wananchi wa chini.

Wizara anayosimamia bashe imefanikiwa kiasi Gani ktk Hilo?

Kila kitu Bei juu, Mchele, Maharage nk nk.

Njaa Kali inakuja kuikumba Dunia wakati tunaendelea kuvuta shuka. Hazina ya CHAKULA Iko wapi?

Chakula sio mahindi na mchele peke yake kuna mihogo na viazi pia
 
NFRA vibali vilikuwa vinatoka kwa 72k kwa tani wanaovinunua wanauza kwa 92k kwa tani mnunuaji wa mwisho anayapata mahindi kwa 1200/kg ila wanunuzi wote wakubwa wanauziwa vibali na vigogo kwa mgongo wa wafanyabiashara. So kudhani eti ipo siku viongozi wetu watamtetea mtu wa chini haipo hiyo. Kuna wajinga wengi humu JF wanashabikia utoaji ruhusa ya kuuza mazao nje utadhani wanaishi nje ya nchi. Wakati hali ya maisha ni aghali sana kwa watu wengi.

Jomba walaji hatutaki mpange bei tunachotaka bei ya soko ndio iamue
 
Ondoa UPUMBAVU wako hapa. Kama huwezi kununua mahindi/unga kwa bei ya sasa, wewe ni mvivu hata ukifa taifa halina hasara.

Mambo ya kufunga mipaka kwa ajili ya ku control bei ya vyakula ili wavivu wa mijini wale kwa mteremko tuliyazika na Magufuli alipokufa mwaka 2021.

Waacheni wakulima wauze wanakotaka kwa bei wanayotaka
Simtamsahau huyo mzee na udikteta wake alinitia hasara mbaya kidogo niugue presha,,,nilinunua mahindi nikaweka stoo Mara paap nikaskia linaropoka hakuna kuuza mahindi nje hata kusafirisha nje ya wilaya hakuna aisee nilipata hasara mbaya gunia nikawa nauza 36,000 wakat nilinunua 60,000 kumpata mteja nayo ikawa shughuli,,,yule mtu mungu amuweke mahali anapostahili
 
Nimeona baadhi ya maeneo mahindi yameanza kuvunwa hasa mkoa wa rukwa na nimeona malori kutoka Kenya na wanunuzi karibia wote wanapeleka shehena ya mahindi Zambia na congo...hatukatai watu kuuza nje lakini kwa kuwa maeneo mengi ya nchi hawakulima mahindi ya kutosha na mikoa mingine kama morogoro mahindi yameharibika mashambani kwa kukosa mvua za kutosha ...nakushauri Tena kwamba zuia kwanza mahindi yasiende nje ili tujitosheleze ...au serikali kupitia nrfa iingie kununua kabla hatujabaki na mabua !! Nakufahamu hupendi kushauliwa na mtu lakini asiesikia la mkuu huvunjika
Kwa longe term, kuruhusu mahindi kutoka ni dawa

Kuyazuia ni kufubaza ukuaji wa sekta
 
Usiwapangie wakulima wapi wauze mazao yao, ardhi kanunua mwenyewe, mbolea kanunua mwenyewe, kaotesha na kupalilia mwenyewe, kavuna mwenyewe halafu baada ya kuvuna unataka umpangie wapi pa kuuza, hii sio akili.
Majibu kama haya niliyategemea
 
Kumudu bei za sokoni kwani hao wasiomudu wamezuiwa na nani kulima mazao yao?
Kwenye population ya 60 million Tanzanians. 30% sio wakulima na wanaishi mijini.

Hayo mazao ya shambani mengi yanauzwa magengeni hakuna cha VAT huko serikali aipati makusanyo ya hivyo.

Ilhali mpaka sasa huyo kichaa Bashe ameshapewa zaidi ya trillion moja kufanya upuuzi wake huko kwenye kilimo. Hiyo 30% ni sawa na 18 million people wakubwa na vichanga kwa wastani kila mtu kachangia tsh 55 elfu, hao wakulima waweze pata mbolea za ruzuku, Bashe afanye experiment za kipumbavu za kilimo.

Bado ujaweka mchango wa watu mijini kwenye kujenga hizo barabara zinazoenda mpaka kijijini na kuwafungulia masoko hao wakulima, mchango wao kufikishiwa umeme vijijini na mambo luluki.

Wanastahili zote kuangaliwa kwenye bei himilivu ya chakula; hizo hela zinazoenda huko azitoki mfukoni kwa baba yake Bashe ni kodi za watu wa mjini; bila ya wao hakuna mkulima wala watu wakwenda kununua hayo mazao.

Mkulima hana mchango wowote kwenye kodi ni kupe anaetegemea hela za walipa kodi mjini ili aishi; halafu mnasema watu wa majini hawana mchango kwa mkulima. Hizo sijui akili za wapi.
 
Nenda kalime na wewe ili uje uwauzie wanaoshinda kwenye betting wakisubiri bashe afunge mipaka
Muwe waelewa pia pale Serikali itakapofungua mipaka yake kuruhusu chakula kutoka nje, kuuzwa nchini. Maana na sisi ambao siyo wakulima, tunachoka kununua chakula kwa bei isiyo na uhalisia.
 
Aliyetoa jasho kuzalisha mahindi asipangiwe pa kuuza - ni jasho lake. Sawa na jasho la mfanyakazi, yaani mshahara, hapangiwi jinsi ya kuutumia.

Mambo ya food security katika taifa ni issue ya serikali. Iyanunue mazao kwa bei shindani na kuyahifadhi. Sio kumzuia mkulima kuuza atakapo.
 
Kumudu bei za sokoni kwani hao wasiomudu wamezuiwa na nani kulima mazao yao?
Siyo lazima kila mtu alime! Mfanyakazi analipwa mshahara, ambao atatumia sehemu ya huo mshahara kununulia chakula kutoka kwa mkulima.

Na mkulima akipata hiyo pesa, atanunulia mahitaji yake ya msingi. Maisha siku zote hutegemeana. Hatuwezi wote kuwa wakulima.

Na mfahamu fika hii biashara ya mazao mnayofanya na Wakenya hao na Wasomali, siyo endelevu! Siku wakiamua kununua hayo mazao yenu sehemu nyingine; mtalia na kusaga meno.

Lakini pia tusiwaone mkilalamika pale serikali itakapo ruhusu chakula kutoka nje, kuingizwa nchini ma kuuzwa kwa bei nafuu. Nyinyi wauzieni Wakenya na Wasomali hico chakula chenu kwa bei nafuu!! Na wakati huo huo Serikali iruhusu wafanyabiashara kuingiza chakula kutoka nje ili kupunguza mfumuko wa bei ya chakula.

Nadhani hamtalalamika. Maana kila mtu atakuwa ameshinda mechi zake.
 
Kwa nini sasa iwe lazima mkulima apangiwe wa kumuuzia mazao yake?
 
Muwe waelewa pia pale Serikali itakapofungua mipaka yake kuruhusu chakula kutoka nje, kuuzwa nchini. Maana na sisi ambao siyo wakulima, tunachoka kununua chakula kwa bei isiyo na uhalisia.

Kalime upate ya kwako ya bei ya uhalisia halafu uuze kwa bei ya uhalisia kama na wewe hutauza kama wakulima leo hii unavyolalamika wanauza
 
Nimeona baadhi ya maeneo mahindi yameanza kuvunwa hasa mkoa wa rukwa na nimeona malori kutoka Kenya na wanunuzi karibia wote wanapeleka shehena ya mahindi Zambia na congo...hatukatai watu kuuza nje lakini kwa kuwa maeneo mengi ya nchi hawakulima mahindi ya kutosha na mikoa mingine kama morogoro mahindi yameharibika mashambani kwa kukosa mvua za kutosha ...nakushauri Tena kwamba zuia kwanza mahindi yasiende nje ili tujitosheleze ...au serikali kupitia nrfa iingie kununua kabla hatujabaki na mabua !! Nakufahamu hupendi kushauliwa na mtu lakini asiesikia la mkuu huvunjika
Lima wewe ubakize ndani ...unafikiri wakulima ni manamba wa kujaza tumbo lako ukajaze choo!?
 
Kalime upate ya kwako ya bei ya uhalisia halafu uuze kwa bei ya uhalisia kama na wewe hutauza kama wakulima leo hii unavyolalamika wanauza
Ushauri wangu kwenu ni huu hapa; kama serikali inaruhusu wakulima/wafanyabiadhara kuuza chakula nje ya nchi kwa bei nzuri, basi iruhusu pia wafanyabiashara wengine kuingiza chakula nchini na kukiuza kwa bei nafuu.

Au unaonaje. Maana hakuna sababu ya haya malalamiko! Lakini pia kulazimisha Watanzania wote kuwa wakulima.
 
Haya maneno unayoongea ni upumbavu mkubwa sana. Wewe kama hauna familia ya kulisha huwezi kuelewa mleta mada anaongea nini.

Ni siku si nyingi tumekuwa tukinunua nafaka kwa bei ya juu isivyo kawaida sababu ya kuendekeza kuwaachia hawa wachuuzi kununua nafaka na kuuza mipakani. Ni muda wa kuratibu huu uchuuzi wa hovyo.
Kalime uuze Bei nafuu ...hamkawii kuwadharau wakulima,huu ni wakati wa mkulima kuheshimiwa
 
Back
Top Bottom