Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Sera za kuzuia mazao yasiuzwe nje ni sera mfilisi. Hakuna kiongozi mwerevu anayeweza kufanya hivyo.

Ushauri ulio mzuri, ni Serikali kwenda kununua mazao kwa wakulima ikashindane na wanunuzi wengine.

Siyo jukumu la mkulima kumtunza mtu yeyote. Kuna wakati Twiga cement walikuwa wanapeleka cement South Africa, halafu tunaagiza cement toka Uganda.

Tukitaka kilimo kikue, kistawi na watu wengi waingie kwenye kilimo, ni lazima tukifanye kuwa ni biashara, na biashara unapeleka pale ambapo unaona utanufaika zaidi.

Jukumu la kuwa na hifadhi ya kutosha ya chakula ni la Serikali, siyo la mkulima
 
Mkuu nchi imejaaa wajinga kwa kiwango cha kutisga, unacho swma ni sahihi kabisa, na Zambia wenyewe wampeiga Bun kuuza mahindi nje ya nchi, hili swala lipo sana Duniani huko kwa nafaka zile ambazo hutumiwa na mass,

bashe anacheza na akili za wajinga wa nchi hii, jiulize Zambia kwa nini kazuia? Kwani ni Serikali ndio inalima mahindi kule Zambia?

Bashe ni mjanja mjanja anaye jua kucheza na akili za wajinga wa nchi hii ambao ni % kubwa sana
Unajiona una akili sana kuliko wengine, wakati yaweza kuw kinyume chake.

Hivi unadhani kilimo cha Zambia ni kama cha Tanzania. Waulize wanaoijua Zambia wakueleze kilimo cha Zambia.

Zambia, kilimo kinaendeshwa na makampuni tu. Mzambia ukimwambia eti mtu maskini anaweza kuwa mkulima, hawezi kukuelewa kabisa. Ndiyo maana kule Zambia, kuzunguka mashamba makubwa ya makumpuni kuna vijiji vingi. Wakazi wa vile vijiji kila siku ni kwenda kufanya kazi kwenye mashamba ya kampuni. Jioni wanapita supermarket ya hapo nyambani wanachukua chakula, wanasaini. Watakatwa kwenye mishahara yao mwisho wa mwezu.

Serikali ilichofanya Zambia ni kuyaambia makampuni yote ya kilimo kuwa itayanunua mahindi yao yote wasiende nje kutafuta soko. Sasa wewe hapa unaposema etu Serikali izuie mahindi kwenda nje, ina mkataba na kila mkulima wa kuyanunua mazao yake yote?

Mkulima anafanya biashara, wala siyo wajibu wake kuwatunza watu wa mjini.
 
Haya maneno unayoongea ni upumbavu mkubwa sana. Wewe kama hauna familia ya kulisha huwezi kuelewa mleta mada anaongea nini.

Ni siku si nyingi tumekuwa tukinunua nafaka kwa bei ya juu isivyo kawaida sababu ya kuendekeza kuwaachia hawa wachuuzi kununua nafaka na kuuza mipakani. Ni muda wa kuratibu huu uchuuzi wa hovyo.
Yaani mnavyopenda kuwaonea wakulima!na wao pia wanahitaji pesa za kusomesha watoto wao, kufanya shughuli nyingine za kujiletea maendeleo. Acheni choyo
 
Unajiona una akili sana kuliko wengine, wakati yaweza kuw kinyume chake.

Hivi unadhani kilimo cha Zambia ni kama cha Tanzania. Waulize wanaoijua Zambia wakueleze kilimo cha Zambia.

Zambia, kilimo kinaendeshwa na makampuni tu. Mzambia ukimwambia eti mtu maskini anaweza kuwa mkulima, hawezi kukuelewa kabisa. Ndiyo maana kule Zambia, kuzunguka mashamba makubwa ya makumpuni kuna vijiji vingi. Wakazi wa vile vijiji kila siku ni kwenda kufanya kazi kwenye mashamba ya kampuni. Jioni wanapita supermarket ya hapo nyambani wanachukua chakula, wanasaini. Watakatwa kwenye mishahara yao mwisho wa mwezu.

Serikali ilichofanya Zambia ni kuyaambia makampuni yote ya kilimo kuwa itayanunua mahindi yao yote wasiende nje kutafuta soko. Sasa wewe hapa unaposema etu Serikali izuie mahindi kwenda nje, ina mkataba na kila mkulima wa kuyanunua mazao yake yote?

Mkulima anafanya biashara, wala siyo wajibu wake kuwatunza watu wa mjini.
Safi Sana watu wa mjini waache kudeka....mapori nchi hii ni mengi
 
Kuna watu wanatetea hili la kuuza mazao nje ona marekani hadi chakula kimetolowa kodi ili kuweka maisha mazuri kwa wananchi wao
 
Usiwapangie wakulima wapi wauze mazao yao, ardhi kanunua mwenyewe, mbolea kanunua mwenyewe, kaotesha na kupalilia mwenyewe, kavuna mwenyewe halafu baada ya kuvuna unataka umpangie wapi pa kuuza, hii sio akili ni mavi.
Wakulima hawafaidiki popote na mpango wa Waziri Bashe bali wachuuzi wa mazao ndio wafaidika wakuu na Bashe anafahamu ila ni mnufaika wa mpango huo ndiyo maana kajizima data
 
Huu ujinga ulimezeshwa na nani ndugu..
Ata ukiambiwa udadavue source of Tanzania budget both (internal and external sources) and justify it in economic distribution uwezi.

Nina uhakika wa asilimia 100 huna hiyo justification ya kwanini watu wa mjini walipie ruzuku ya mbolea, wachangie capital investment ya bank ya kilimo na upuuzi mwingine wa uwekezaji Bashe anaofanya.

Huyo jamaa hana huo uwezo wafikra, anachokera ni kutokuwa na huruma kwenye hiyo mitazamo yake jinsi kwa anavyo umiza watu.

Haya yote tungeyakwepa isingekuwa mtu mmoja tu; Jakaya Mrisho Kikwete.

Siku nikikamatwa na kunikuta ya kunikuta I can live with that in hell. Hila nimetokea kulichukia hili lizee ndio lilioharibu uraisi wa Samia.

Back to my game Sixers vs Celtics; after that there’s Suns vs Nuggets. See ya in the morning.

Huyo msomali ni mnyama, fisadi na huruma hana. I don’t care.

Sina chuki na Bashe as a human being ila fikra zake (matter of fact mademu wa kisonjo wananipa wazimu na shepu zao balaa ‘warya’) hila Bashe ni nuisance lifisadi na lijinga lisilokuwa na huruma.

Mods Blame it on J.D nonetheless it is what I have always thought; so I can live with the consequences.
 
Nyie ndio Wazazi wenu kule bushi wana lala njaaa na Daily wanahitaji pesa za chakula, sasa mkiwa mjini mnajiona wajanja sana
Hao wazazi wako waliopo bush kwenye mashamba na Bado wananjaa inabidi wapigwe na njaa zaidi ili iwe fundisho
 
Nakuunga mkono mkuu, hao wengine wanaokwambia nenda kalime ni wasubilia mishahara,wao hawajui kuweka akiba, wanakula mpaka mshahara wa mwezi ujao.

Lakini kwa mtu makini, na taifa masikini, huweka akiba ya chakula, dunia nzima kwa sasa ina uhaba wa chakula.
 
Nimeona baadhi ya maeneo mahindi yameanza kuvunwa hasa mkoa wa rukwa na nimeona malori kutoka Kenya na wanunuzi karibia wote wanapeleka shehena ya mahindi Zambia na congo...hatukatai watu kuuza nje lakini kwa kuwa maeneo mengi ya nchi hawakulima mahindi ya kutosha na mikoa mingine kama morogoro mahindi yameharibika mashambani kwa kukosa mvua za kutosha ...nakushauri Tena kwamba zuia kwanza mahindi yasiende nje ili tujitosheleze ...au serikali kupitia nrfa iingie kununua kabla hatujabaki na mabua !! Nakufahamu hupendi kushauliwa na mtu lakini asiesikia la mkuu huvunjika
Acha upuuzi wako wewe,mwaka Jana mahindi yalikuwa kidogo na hayakuzuiwa ndio ije kuwa mwaka huu yamejaa Kila sehemu?

Harafu muwe mnaacha ushenzi wenu , mkulima hayuko hapo kukuza tumbo lako anafanya biashara ya Kilimo kama unayofanya wewe Kwa hiyo tusipangiane.
 
Hivi unadhani kilimo cha Zambia ni kama cha Tanzania. Waulize wanaoijua Zambia wakueleze kilimo cha Zambia.

Zambia, kilimo kinaendeshwa na makampuni tu.

We jamaa wewe,kilimo cha makampuni gani huko michina imejaa mpk inalima kabeji.
Inauza kila kitu mpk mitaani ni michina,
migahawa ni michina,
Mpk kupima uzito michina
Kuchoma mahindi wamo
Kuuza yeboyebo wamo.
Kuuza vyura na minyoo wamo
Kuuza nyuchi na tako wamo
Huko Zambia ni km Kiujumla nchi ya kwao.
Wamejaa wanafanya watakacho.
Wazambia ni vijakazi tu wanatemewa mpk mate na wachina acha kulambwa vibao.
 
Maombi yangu ni mama apite 2025 na Bashe aendelee kubaki kuwa Waziri wa kilimo. Baada ya mavuno ya mwaka huu kama bei zitaendelea kuwa nzuri hivi hivi au zikiongezeka zaidi (ambayo ndo sala yangu kubwa kwa sasa) nna mpango wa kufanya uwekezaji kwenye kilimo cha kisasa na kutanua uwekezaji wangu. Mwenyezi Mungu akinipa afya na uhai by 2030 ntakuwa na story nyingine kabisa ya kiuchumi.

Wakati huo wewe mtoa mada endelea kuliangalia hili kama tatizo meanwhile wengine tukiiona kama fursa. After some years ntakuja kuwa motivation speaker wako na kwa wenzako wenye mawazo kama yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waswahili wanamsemo ‘damu nzito kuliko maji’.

Ni mwehu tu sio kwa sababu ya rangi au ethnicity yake; bali kipato chako anaweza kushabikia upuuzi wa Bashe.

Na Ndio maana huyo ‘Jakaya Mrisho Kikwete’ hana tofauti na Tippu Tip.
 
Hakuna mtanzania mwenye kipato kizuri halafu mwenye ndugu unga-unga wanaemtegemea yeye. Na wanapokwama shida zao wakampelekea huyo, akamuelewa Bashe.

Huyo mtu anaepigiwa simu anaweza mudu gharama za kupanda maisha kama yeye, ila atapo pokea simu za mizinga ya njaa kutoka kwa nudge zake mungu anajua anavyotatua kwa uelewa wa mazingira yao.

Na ndio asilimia kubwa ya familia za watanzania bara; atujui huko visiwani.

Ni jitu jinga au lifisadi lenye roho mbaya linaloweza tetea ujinga wa Bashe. Lakini kwa wale wenye ndugu wenye vipato vidogo tunajua vilio vyao vya gharama za, kodi zao za Pango, mishahara yao, gharama za chakula na wengine na unattainablility ya vipato vyao.

Unakuta mijitu mijinga inatetea sawa tu kupanda kwa gharama za chakula; how stupid.

Get rid of this idiot on that ministry. Mamillioni ya watu wanaumia bila ya sera ya price stability kwenye chakula. Halafu waziri mwenye ana huruma; we vipi.
 
Mataahira na wapumbavu hawatakuelewa mkuu!

Kwa utaahira wao wanafikiri anaefaidi eti ni mkulima,
Njaa itakapoanza atakae kuwa wa kwanza kulia ni huyo huyo mkulima
 
Simtamsahau huyo mzee na udikteta wake alinitia hasara mbaya kidogo niugue presha,,,nilinunua mahindi nikaweka stoo Mara paap nikaskia linaropoka hakuna kuuza mahindi nje hata kusafirisha nje ya wilaya hakuna aisee nilipata hasara mbaya gunia nikawa nauza 36,000 wakat nilinunua 60,000 kumpata mteja nayo ikawa shughuli,,,yule mtu mungu amuweke mahali anapostahili
Yule Sumry tajiri Laela Sumbawanga aliuza mabasi yote akageukia kilimo cha mahindi. Magufuli alipofunga mipaka alipata hasara kubwa sana. Wanaolalamika bei za mahindi ni kubwa nao wajiunge tulime wote. Maana bado 85% ya ardhi ya Tanzania hailimwi
 
Back
Top Bottom