Hussein Bashe, zuia mahindi kutoka nje kwanza nchi ijitosheleze

Kuna mazao au bidhaa za kilimo zinaingizwa toka nje kila siku mfano ngano na sukari. Juzijuzi tu wakaruhusu Michele pia.

Hayo yanafanywa kwa uangalifu ambao hautaathiri wakulima wa ndani. Uhaba unaosema si mkubwa wa kufanya kila kitu kiruhusiwe kuingia toka nje. Mazao yenye uhaba mkubwa ndio yanaruhusuwa kuagizwa toka nje.

Ndio maana nikakuambia hujaelewa lengo la kumlinda na kumwinua mkulima wa kitanzania. Unachotaka wewe ni unafuu wa mda mfupi kwa watu wachche wa mijini,lakini huoni ni kwanamna gani taifa litanufaika kama mamilioni ya wakulima watainuka na kuwa wakulima wa kisasa na wenye vipato vikubwa.
 
Nimeongea kuhusu Azam na Mo wanaouza bidhaa bei anayotaka hulalamiki. Mbantu kijijini akiuza mazao bei nzuri mnalia.

Mbona mna chuki kubwa pale mkulima anapotajirika lakini hamna chuki pale muhindi anapotajirika?
 
Badala ya kujibu maswali yangu bado unambwelambwela tu huna ulijualo kama unaelimu yoyote ya kiuchumi ni ya nadharia( makalatasi) huna ulijualo uchumi wa kwenye pdf kiuhalisia haupo.
Narudia kukuuliza tena mwanauchumi nisaidie wewe kama mchumi ungekependekeza bei ya mazao iuzwe shilingi ngapi ili mkulima afaidike na pia mlaji asiumie
Swali la pili umejibu kuwa umasikini ndiyo umesababisha watu wakimbilie betting ok sawa sasa kama mchumi unashauri wote tukimbilie betting ili tujikomboe kutoka kwenye umaskini
 
Kuna sehemu anakwenda vizuri bashe ila kuna maeneo pia naona anataka kuyasahau sijui niseme kuyatelekeza mwaka Jana bei ya pamba ilikuwa 1,800 mpaka 2,000 kwa kg, lakin kwa mwaka huu kidogo unataka kutuvuruga wakulima mmeanza kufungua msimu na bei elekezi ya 1,060 dah na ukizingatia mwaka huu wakulima wengi wameitika sana kulima pamba hapa kidogo kuna tatizo
 
Serikali ndiye msimamizi na regulator wa kila kitu katika nchi.

Serikali ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha nchi inakuwa na chakula cha kutosha wakati wote. Hilo siyo jukumu la mkulima.

Serikali inatakiwa kuingia sokoni na kununua mazao ya mkulima kama wanavyofanya wanunuzi wengine, ikiwezekana hata kwa bei nzuri zaidi. Kwa kuwa Serikali haifanyi biashara ya chakula, ina uwezo wa kununua kwa bei nzuri, na wakati wa upungufu wa chakula, kukiuza kwa bei ya chini.

Tukitaka chakula kiwe kingi, Serikali isiingie kwenye udhibiti wa masoko. Tukifanye kilimo kuwa chenye faida. Kikiwa na faida, wengi wataingia kwenye kilimo. Wengi wakiingia kwenye kilimo, bei hazitapanda juu kupindukia.
 
Na anavyopenda kujidai anaangalia maslahi ya mkulima wakati anawanufaisha madalali zaidi, wakulima wanabaki masikini.
 
Waacheni wakulima wapige pesa , uchumi unatengamaa tatizo sio unga kuuzwa Bei kubwa hata ukiuzwa elfu kumi kilo moja lakini kama pesa inapatikana Basi hamna tatizo naamini wakulima wakiwa well financially Basi hata sisi Mafundi tutapiga hela sana maana wakulima watajenga majumba ya maana nk

Mama yupo sahihi

Then kilimo kikiwa na faida watu wengi watalima na Bei itashuka automatically itakuwa supply kubwa kuliko demand
 
Ndipo ilipo HOJA yangu.

Kwanini hainunui vyakula wakati huu wa mavuno Kwa wakulima na kuwa na Hazina ya CHAKULA Cha kutosha Ili kuviuza masokoni Kwa Bei nafuu Ili kudhibiti mfumuko wa Bei masokoni miezi ambayo wakulima wako mashambani?

Na ndio HOJA ya mwandishi, mfumuko wa Bei sokoni uthibitiwe Kwa nzima mbalimbali.
 
Mataahira na wapumbavu hawatakuelewa mkuu!

Kwa utaahira wao wanafikiri anaefaidi eti ni mkulima,
Njaa itakapoanza atakae kuwa wa kwanza kulia ni huyo huyo mkulima
Acha tu mkuu. Watafaidika watu wote, mkulima atakuwa wa mwisho kama akipata hiyo faida.
 
Watu wana agenda zao ndio maana wapo hapa wanashabikia hovyo. Hawana hoja zaidi ya kalime wewe utafikiri wanauchungu na huyo mkulima, wakati anayoyafanya huyu Bashe yanaenda kumuumiza mkulima.
 
Wewe unalima? Au unalima kimawazo? Kuna mkulima anajua mpaka wa Namanga unafananaje?
Hahaha ndo hapo sasa. Eti mkulima anauza nje wakati wanauzaga shambani tena kwa bei ya hasara. Wangekuwa wanauza wao huko nje na walivyo wengi kwenye hii nchi kungekuwa na masikini?
 
Tatizo watanzania tunapenda mwisho mzuri ila kwenye michakato ya kuufikia huo mwisho mzuri hatuutaki kuusikia. Kwenye pembejeo za kilimo kuuzwa ghali wanaopiga kelele ni wakulima wenyewe na inabidi wanunue hvyo hvyo bei ghali wakati huo mmekaa kimya. Kaenyeka mkulima kwa gharama zake na kuvuja jasho kweli kweli eti mnataka auze mnavyotaka. Nendeni mlime yenu muuze kwa bei rahisi
 
Ila kumbukeni anaeenda kuuza nje sio mkulima nimfanya biashara ambaye ananunua kwa mkulima kwa bei ya chini.
 
Ila kumbukeni anaeenda kuuza nje sio mkulima nimfanya biashara ambaye ananunua kwa mkulima kwa bei ya chini.
Bei ya chini shilingi ngapi kama unadhani wananunua kwa bei ya chini unashindwa nini na wewe kununua ufanye biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…