Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi kukosa Kura zote za Zanzibar za Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) inafikirisha sana. Haki ya Wazanzibar kuchagua iko Wapi?

Zanzibar 2020 Hussein Mwinyi kukosa Kura zote za Zanzibar za Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) inafikirisha sana. Haki ya Wazanzibar kuchagua iko Wapi?

Hussei Mwinyi ameonesha udhaifu mkubwa sana leo. Ni bora Magufuli asingempa nafasi ya kuongea..

Kitendo cha kukiri hadharani kwamba Zanzibar ni kugumu si rahisi yeye kushinda kama ilivyo huku bara na kuomba msaada CCM bara wamsaidie kwangu mimi naona udhaifu mkuubwaa.

Kashafaham hakubaliki na kashajua kapitishwa na wabara. Ataumia vibaya sana.
 
Utavunjwa tu(ni muda tu ndio utaongea), hakuna mzanzibar anayetaka MUUNGANO ,hauna faida kwao zaidi ya kuwanyonya tu!!
Nilitaka kupita kimyaaa ila kwa ushuzi huu siachi kunena. Nauliza tu swali; Tangu lini kupe kasema kuwa, huyu ng'ombe ndiye ananinyonya? Kwa akili yako unaona kuwa Tanganyika inaweza kumnyonya zanzibari?? Nenda kapime macho, huenda unasumbuliwa na mtoto jicho.
 
Hujui jumla ya wajumbe wa Nec Zanzibar ni 35.Hakuna kitu cha kuogopa sasa hivi duniani kama Mwenyezi Mungu na teknolojia ,bado unataka ushahidi?

Umemjibu vema kabisa. Na anasahau kabisa kuwa ZEC inamtaka mtu kuwa mzanzibar (wao wanaita mkaazi) ili kuwa mpiga kura au mgombea. Kama jamaa alikuwa Mbunge wa Mkuranga - wanamchukulia sio mzanzibar na ndio maana alishinda kwa kura za wabara!! Mimi sielewi ni kwanini wajumbe watofautiane kwa idadi kati ya nchi hizi mbili. Labda ni kwa kuwa siko katika siasa lakini ni dhahiri maamuzi ya wanaCCM Zanzibar yatafanywa na CCM Bara - siku zote!!

Naona njia nyeupe kwa Seif, ziliwemo kura nyingi za wanaCCM hasa baada ya mshindi kusema ataongoza Zanzibar kama JPM anavofanya Bara!
 
Nilitaka kupita kimyaaa ila kwa ushuzi huu siachi kunena. Nauliza tu swali; Tangu lini kupe kasema kuwa, huyu ng'ombe ndiye ananinyonya? Kwa akili yako unaona kuwa Tanganyika inaweza kumnyonya zanzibari?? Nenda kapime macho, huenda unasumbuliwa na mtoto jicho.
Cha kushangaza sasa , Ngo'mbe ndio anang'ang'ania anyonywe na Kupe!! Hakuna mzanzibar hata mmoja anayetaka muungano,mnawaumiza wazenji waachieni nao wawe wanakopa IMF na WB sio mpaka nyie mkope kisha muwape kama hisani.
 
Nadhani imefika wakati waelezwe kuwa, toto ukilibeba mgongoni nalo likalilia kushuka basi liachie lishuke hata kama ni kati ya mto. Wadhani mikopo ndo imetufikisha uchumi wa kati?
 
mmeshindwa siasa za hoja mmebakia kwenye propaganda tu.
 
Nadhani imefika wakati waelezwe kuwa, toto ukilibeba mgongoni nalo likalilia kushuka basi liachie lishuke hata kama ni kati ya mto. Wadhani mikopo ndo imetufikisha uchumi wa kati?
Vunjeni Muungano haraka! Mnawaumiza WAZENJI.
 
Kwani ulitengenezwa kwa saruji hata sasa uvunjike? Hapakuwepo maandishi bali maelewano hivyo tuelewane pia kuachana. Acheni kelele za chura
Inahitaji maridhiano ya pande zote mbili ,wanzanzibari hawataki ila wabara wanaung'ang'ania.
 
Maalim Seif yeye anatak
Ukiona baba yako anawagawia watoto wa Jirani Urithi ujue wewe ni mvuta bangi na mla Unga.

Akikupa Urithi utauza upate hela ya kulamba Unga.

++++++++++++++++++++++++++
du!!!
Nilitaka kuuliza kwani huyo Maalim Seif anataka kuifanyia nini Zanzibar ambacho mwinyi hawezi?

Ila comment yako hapo juu imejitosheleza🙏
 
Kwani ulitengenezwa kwa saruji hata sasa uvunjike? Hapakuwepo maandishi bali maelewano hivyo tuelewane pia kuachana. Acheni kelele za chura
Tulichanjiana damu na udongo pia hahaaa
 
yakhe haki imetendeka, chama ni cha muungano! kura zimepigwa kwa uwazi mshindi kapatikana mwenye ushawishi zaidi!! kwanini kule Zenji walimpa form ya urais Mwinyi kama si mwenzao? kama kosa basi ni lao machogo tunapeta tu ati!!
Hili suala si lakuchukulia poa. Limebeba jambo zito sana na litakujukujulikana huko mbele ya safari.
 
Inahitaji maridhiano ya pande zote mbili ,wanzanzibari hawataki ila wabara wanaung'ang'ania.
Maridhiano tayari maalim Seif hana tabu tunaoumia ni sisi
images.jpeg
 
Hawa wazanzibar watatawaliwa na CCM bara hadi wajute!!
CCM bara inawachagulia hadi Rais wao, so sad...ila they do have a chance to react...piga chini huyo mchagueni Mwanamapinduzi mwenye fikra kama kijana Maalim Self atawavusha!!
 
Kwaio ht Hussain Mwinyi hakujipigia kura?
 
Kapigeni kura acheni kulalamika mitandaoni wazanzibari, maana utashangaa anashinda kwa kishindo uko, na kuliko maalimu
 
Back
Top Bottom