Huu mdahalo lengo ni nini? Mdahalo unaitwa “Jesus and Mohammed”

Huu mdahalo lengo ni nini? Mdahalo unaitwa “Jesus and Mohammed”

Unapambanaga sana na faiza mkuu, jukwaa la zakir naik ni kubwa sana litakufaa. Usiingie mitini mkuu,
Liko wapi hilojukwaa 😁..kuna yule shekh mazinge na prof ndacha wanashindanaga kuhusu dini hoja zao ni zakitoto sana japo watu wanawaona wana hoja nzito awajawai kukutana na mimi wote watakimbia na kupigwa mawe na waumini wao ....
 
Mohammed Salah vs Gabriel Jesus
1000017848.jpg
 
Liko wapi hilojukwaa 😁..kuna yule shekh mazinge na prof ndacha wanashindanaga kuhusu dini hoja zao ni zakitoto sana japo watu wanawaona wana hoja nzito awajawai kukutana na mimi wote watakimbia na kupigwa mawe na waumini wao ....
Zakir Naik anatembeleaga nchi nyingi sana mkuu hata ukiwa unascroll youtube one time moja lazima ukutane nae, wewe achana na kina mazinge mkuu fika kwenye tarehe hizo. Unasemaga fulani hajakutana na wewe. Sasa huyu sheikh katoka huko kaja bongo kaka. Mambo yasiwe mengi fika na maswali yako, mimi ntafatilia kwa makini sana nisikie majibu


View: https://x.com/jaliluzaid/status/1871401246114115996


Kila la kheri
 
Nafikiri ameeleweka! Aliongelee na hili kwenye huo mjadala! Huwa namkubali sana huyu mwanazuoni(Naik) coz hana jazba,hasira,mhemko wala papara!
Haya maswali mepesi sana
 
Tangazo umeona wapi mkuu...?
Ngoja nifanyie hili suala kazi hapa
Azam TV wameweka hilo Tangazo na Azam Media ndio wamemuwezesha huyo Shekhe kufika Tanzania (Wadhamini wa huo mdahalo wa upande mmoja)

Cha ajabu ni kuwa mdahalo wa mtu moja. Yaani sheikh against yeye mwenyewe huku anaongela swala la muddy VS Yesu.

Wanaogopa nini kuita Mkristo ili iwe Sheikh VS Mchungaji. Wanialike nije kumtoa knock out huyo shehe.
 
Midaharo mbona inafanyika mingi tu, au unajizima data kwamba wakristo hawafanyi?
Wanafanya against nani? Wanafanya sana akian Jeff Massawe na akina Ndacha ila kunakuwa na Sulle au Shekhe yule mzee msema hovyo.

Hiyo ni sawa, sasa huu ni wa nani against nani? Shekhe Sijui Zikhir atadebate na nani mkuu? Kwamba Yeye against yeye na anajadili kuhusu Muhammad na Yesu.

Wangesema amekuja kutoa darasa au mawaidha kwa waislamu ni sawa ila kosa ni hilo la kuwa mdahalo lakini anafanya mwenyewe.
 
Umesikia tangazo vizuri wamesema njoo na maswali yako yote utajibiwa means kutakuwa na majadiliano? Pia unaposema ivyo ni wazi kabisa kutakuwa na maswali ya kichokozi
Kama una imani yako, na umeishika sawasawa, haijalishi hata uchokozwe vipi. Dunia nzima watu wanahoji imani za wenzao lakini bado dini zinaendelea tu kuwepo.

Ukiamua kubadili imani bila shuruti, ina maana roho na akili yako itakuwa imeshawishika.
 
Wanialike nije kumtoa knock out huyo shehe
Sifahamu uelewa wako kuhusu dini, ila jamaa ni level nyingine coz ana ufahamu,uelewa,uzoefu,maarifa,elimu,ujuzi kuhusu dini zote za hapa duniani.

Hili haliji mara moja linachukua muda kidogo na hata miaka kadhaa.Jamaa huwa hapendi kubishana (sifa ya watu werevu).

Ni mwanazuoni nguli kwa waislamu na kwa mambo ya dini.Ameizunguka karibu dunia nzima, kwa level yake naona huna jipya la kumwambia.

Kwanza unaonekana una papara na mhemko najua hukosi jazba na hasira!
 
Back
Top Bottom