Huu mdahalo lengo ni nini? Mdahalo unaitwa “Jesus and Mohammed”

🤔🤔🤔! Aiseee bongo bhana sasa mdahalo wa kujadili iman za watu tulisikia wap hii n upuuzi wahali ya juu na serikal kwl wakruhusu ujinga huuu bs hapa hatuna serkali, Africa dah kwl n bdo atujui tumekuja dunian kufanya nn din tumeletewa lakn unalikuta jitu limekazana kujaza na kukarirshwa vtu ambayo amnaga
 
Huo mdahalo wa azam upigwe marufuku. TCRA chukueni hatua hayo si maudhui ya chombo hicho, labda kama tv imaan, maarifa radio na media zingine za kiislam ingeeleweka vema. pili, huyo sheikh anayekataza waislam wasisherekee na kuuza bidhaa za krismas ni mwehu na mwendawazimu.
 
Huo mdahalo wa kulinganisha ni wa kipuuzi haujengi bali huleta mashindano yasiyokuwa na tija, haujengi huleta jazba na hasira kwa anayeshindwa kujenga na kupangua hoja kwa maandiko ya biblia na quran. Wakristo hugeuzwa kituko
 
C
Anaweza kumfikia professor mazinge kwa umahiri wake?
 
Huo mdahalo wa kulinganisha ni wa kipuuzi haujengi bali huleta mashindano yasiyokuwa na tija, haujengi huleta jazba na hasira kwa anayeshindwa kujenga na kupangua hoja kwa maandiko ya biblia na quran. Wakristo hugeuzwa kituko
Acha kabisa
 
Kabisa tutafanyaje
 
Kwani unajua Jesus gani ataongelewa?
Kumbuka kuna akina Jesus kibao.
Sio kila Jesus ni JESUS CHRIST.
Usikuchukulie serious sana haya mambo, utajizeesha bure.
Sawa saww mkuu
 

26 December 2024
AZAM MEDIA LTD PAMOJA NA THE ISLAMIC FOUNDATION …

UJIO WA DR ZAKIR NAIK TANZANIA - RATIBA YAKE YOTE

View: https://m.youtube.com/watch?v=PLO0zcQm7ok
KWA MARA YA KWANZA TANZANIA WANAKULETEA MHADHIRI MASHUHURI WA KIMATAIFA , DKT ZAKIR NAIK AKIAMBATANA NA MWANAE SHEIKH FARIQ NAIK KATIKA MDAHALO WA MASWALI NA MAJIBU :

TAREHE 31/12/2024 MSIKITI ZINJIBAR, UNGUJA ZANZIBAR KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA


TAREHE 2/01/2025 DIAMOND JUBILEE DAM KUANZIA SAA 1 USIKU HADI SAA 6 USIKU

TAREHE 5/01/2025 BENJAMIN MKAPA STADIUM UWANJA WA TAIFA KUANZIA SAA 2 ASUBUHI HADI SAA 7 MCHANA


MATANGAZO HAYA YATAKUJIA LIVE - MUBASHARA KUPITIA CHANEL YA ZBC2 WEMA UNAOENDELEA


PIA TUTAKUWA MUBASHARA KATIKA DUA TV AOMBWAE NI MOLA PEKEE JESUS AND MUHAMMAD PEACE BE UPON THEM BROTHERS IN FAITH




 
26 December 2024
Nairobi, Kenya

Lecture : Prophet Muhammad in the Bible - Dr. Zakir Naik | Talk + Q&A | Kenya, East Africa

View: https://m.youtube.com/watch?v=C4jvfQRrXg8

Hata Sheikh wetu nchini Tanzania, mwanazuoni Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania aliwahi kuonya juu ya dhehebu moja kuanza fitna, misuguano, kutishiana n.k dhidi la dhehebu jingine, wakati wote ni dini moja ya ki-Islamu..

19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania

SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI KWA HAYA YANAYOENDELEA


Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha sawia na maktaba yake binafsi iliyosheni mabuku juu ya mabuku ya elimu duniya na ilm ya dini pia ktk utumishi ulitukuka kwa dini na jamii.

Pia sheikh Abuu Iddi ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni Saudia na Shia linaloegamia Iran, Pakistani, India yanayo shambuliana kupitia propaganda kutoka maeneo mbalimbali ya dunia ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao wenye ushawishi wa kisiasa wa ndani na nje ya nchi kuchochea misuguano
 
Mdahalo kama huu unalenga zaidi kutoa maarifa na kuelezea tofauti na mfanano kati ya Mitume hao wawili kwa mujibu wa maandiko ya kidini. Ni nafasi ya kujifunza na kuelewa mtazamo wa dini tofauti, si lazima iwe "kupambanisha" imani, bali kujenga maelewano na elimu.

Kuhusu maswali yako:

  1. Kwa nini Waislamu wanapenda kuongelea mambo wasiyoamini?
  • Uislamu unaona umuhimu wa kujadiliana kwa hekima na kuwafikishia watu ujumbe kwa njia nzuri (Qur'an 16:125). Pia, Waislamu wanamwamini Yesu (Isa, A.S.) kama mtume wa Mungu, hivyo kumjadili si jambo geni katika Uislamu.
  1. Kwa nini Wakristo hawaandai midahalo kama hiyo?
  • Kila dini ina mbinu yake ya kufikisha ujumbe. Uislamu unasisitiza mazungumzo ya kidini kama njia ya kuelimisha. Wakristo wana njia zao, kama mahubiri, ibada, na matamasha.
  1. Shekhe kukataza Waislamu kusherehekea Krismasi:
  • Shekhe huyo anatoa fatwa kulingana na misingi ya dini yake. Katika Uislamu, kushiriki sherehe za kidini zisizo za Kiislamu mara nyingi huonekana kama kwenda kinyume na mafunzo ya dini. Hii haimaanishi kuwa kuna chuki, bali ni kuheshimu mipaka ya kiimani.
Kwa kumalizia, ni muhimu kuheshimu maoni na imani za kila mmoja, bila kusambaza hisia za chuki au kutokuelewana. Midahalo kama huu inaweza kuwa fursa ya kujifunza zaidi ikiwa tutaenda kwa nia ya kujenga, si kupinga.
 
Hili sio lengo mahususi la mdahalo/midahalo. Lengo ni kuwasilimisha wakristo. Sababu mara zote waislam wamekuwa wakishindwa hoja na WAKRISTO, na kuanzisha vurugu. Hawana uvumilivu. Bahati nzuri kuna wakristo wanaijua Quran kuliko waislam maamuma wasiojua lolote.
Ninayo mifano hai. Na kama mtu anabisha iandaliwe midahalo ya wazi na polisi wawekwe kulinda amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…