Huu mpango wa Dangote kujenga refinery East Africa umekaaje?

Nyerere alijenga TIPER(Tanzanian and Italian Petroleum Refining) baada ya uhuru ,kikaja kufa mwaka 1999 kwasasa wanatumia Oryx kuhifadhi Petrol ,tumekwama wapi mpaka DANGOTE anakuja kutakeOVER?
 
Hapo watakuwa wamecheza kama Pele, mafuta yatoke Hoima Uganda kisha wajenge refinery Tanga tusihangaike kununua mafuta kwa madalali wanaosababisha bei ya mafuta ipande hovyo.
Kwani Mafuta ya Hoima ni ya waganda au TOTAL na kama Dangote anajenga wenye mali wameridhia
 
Narudia ni Tanzania tu ndio kutajengwa Refinery ikiwa wenye nguvu za pesa wataona inafaa kujengwa.

Wapembuzi ndio wenye kuamua sio Wanasiasa na Wapembuzi na makampuni ya kujenga iyo Refinery pesa vyote vinatoka nje wkt mwengine tena kwa Udhamin wa Ma banking ya Kimataifa

Wanasiasa kama Ruto uwezo wao ni kuvutia tu pande yake!!

lkn wenye kuamua sio wao✍️
 
Ni Upumbavu tu yeye Mseveni amekosa kupata dola bilion 5 au 14 kujenga tatizo umasikini wa akili kwa viongozi wa africa
Kutotengeneza kiwanda Wako sahihi.

Reserve ya Uganda sio kubwa Yakusema uweke Dola Billion 5 au zaidi kirahisi hivyo.

Na ubaya ni kuwa Uganda Haina Bandari ya baharini (kwamba anaweza kuagiza cruid oil) nchi za nje.

Bado nchi jirani nyingi hazina mafuta labda sudan kusin na ubaya ni nchi ya machafuko

Hivyo kutengeneza kiwanda Ni hasara kutokana na reserve iliyopo .
 
Wanadai crude nyingine itatoka DRC na South Sudan. Kitu ambacho sielewi ni Tanzania kutosikika kabisa kwenye hili suala. Yaani Ruto, Museveni na Dangote wajadiliane kujenga refinery Tanzania!!
 
Nyerere alijenga TIPER(Tanzanian and Italian Petroleum Refining) baada ya uhuru ,kikaja kufa mwaka 1999 kwasasa wanatumia Oryx kuhifadhi Petrol ,tumekwama wapi mpaka DANGOTE anakuja kutakeOVER?
Wizi wa Kijinga wa watu weusi. Hata Kenya na Nigeria refineries zao zimekufa.
 
Tanzania ni watu wa hovyo ni hakuna mfano, miaka ya nyuma wakati wa utawala wa Nyerere tulikuwa na mtambo wa kusafisha mafuta ghafi pale Kigamboni Tipper lkn kwenye tawala zilizofuata zikaiua ili wapate cha juu kwenye uagizaji wa mafuta yaliyosafishwa leo eti wanaongelea tena mtambo wa kusafisha mafuta ghafi. Bure kabisa.
 
Watanufaikaje nje na ukaribu wa kupatikana kwa mafuta? Au watakuwa wanapewa 10% ya udalali?
Unafikiri Luto ni mjinga mpaka amwombe Dangote kujenga refinery Tanga?

Kenya itanufaika kwa mafuta nafuu, usalama wa nishati, biashara, ajira, na ukuaji wa viwanda

Hiyo refinery itaruhusu crude kutoka mataifa mengine kusafishwa

Kenya wana mafuta Turkana wanaweza kusafirisha hadi Tanga wayasafishe kwa matumizi ya ndani na nje
 
U
Hapo watakuwa wamecheza kama Pele, mafuta yatoke Hoima Uganda kisha wajenge refinery Tanga tusihangaike kununua mafuta kwa madalali wanaosababisha bei ya mafuta ipande hovyo.
Uko sahihi kabisa mkuu.

Lakini kwa serikali HII YA MADALALI! HUO MPANGO WA KUJENGA REFINERY TANZANIA NI NDOTO! Zitafanywa figisu hapo!, labda mpaka siku CCM IKIACHIA MADARAKA! Ndipo refinery itajengwa Tanzania
 
U

Uko sahihi kabisa mkuu.

Lakini kwa serikali HII YA MADALALI! HUO MPANGO WA KUJENGA REFINERY TANZANIA NI NDOTO! Zitafanywa figisu hapo!, labda mpaka siku CCM IKIACHIA MADARAKA! Ndipo refinery itajengwa Tanzania
Lazima watangulize kampuni uchwara, kujenga maeneo yatakayopata fidia na kuleta vuguvugu ili mradi waondoke na chochote kitu
 
Kwani Mafuta ya Hoima ni ya waganda au TOTAL na kama Dangote anajenga wenye mali wameridhia
Ndio lobbying inafanyika hapo, unadhani Dangote kujenga kiwanda cha saruji Mtwara alikuwa hajui kama atakuja kujenga refinery hapa TZ miaka ya baadae?
 
Hapo ndio utaelewa kwenye pesa ndefu lazima damu zimwagike, fitina ziwe nyingi na minyororo iwepo sana tu
 
Nisaidie kujua Kenya anafaidikaje na hii refinery kujengwa tanzania mbali na kusogezewa huduma ya mafuta mlangoni kwake? Maana inaonekana yeye ndio anayemtongoza Dangote ili mradi uje Bongo
 
Hiyo iko vizuri kinachoumiza hilo ni wazo la Luto

Tanzania ilitakiwa iwe mstari wa mbele kuongea na Dangote kuhusu huo uwekezaji

Ina maana viongozi wenu hawaoni fursa?

Kuzaliwa Tanzania ni laana
Watapiga wapi udalali ikifanyika hivyo,?
 
Muda mwingine tuache uzwazwa wa kujishusha thamani yetu,unavyodhani huyo ruto anapenda refinery ijengwe TZ,halafu kwa uzwazwa bado unaamini hata ikijengwa TZ mnufaika atakua ruto!,museveni na dangote wanaprefer refinery iwepo TZ kwani wanajua kabisa kenyan ni untrust,hata kama tofauti za kisiasa watanzania tuache kujishusha thamani yetu sisi wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…