Huu mpango wa Dangote kujenga refinery East Africa umekaaje?

Huu mpango wa Dangote kujenga refinery East Africa umekaaje?

Unafikiri Luto ni mjinga mpaka amwombe Dangote kujenga refinery Tanga?

Kenya itanufaika kwa mafuta nafuu, usalama wa nishati, biashara, ajira, na ukuaji wa viwanda

Hiyo refinery itaruhusu crude kutoka mataifa mengine kusafishwa

Kenya wana mafuta Turkana wanaweza kusafirisha hadi Tanga wayasafishe kwa matumizi ya ndani na nje
Nafikiri haitakuwa kwa faida kubwa kutuzidi.
 
Wanadai crude nyingine itatoka DRC na South Sudan. Kitu ambacho sielewi ni Tanzania kutosikika kabisa kwenye hili suala. Yaani Ruto, Museveni na Dangote wajadiliane kujenga refinery Tanzania!!
Bado Tanzania ni ideal place ya kujenga refinery ya mafuta toka Uganda.

Hivyo hatujaondoka kwenya picha.

Mafuta hayawezi toka Uganda, pa kuyapakulia pale Tanga halafu ujenge refinery kwingine.
 
Hiyo iko vizuri kinachoumiza hilo ni wazo la Luto

Tanzania ilitakiwa iwe mstari wa mbele kuongea na Dangote kuhusu huo uwekezaji

Ina maana viongozi wenu hawaoni fursa?

Kuzaliwa Tanzania ni laana
Kuzaliwa Afrika ni laana, ila kuzaliwa Tanzania ni zaidi ya laana.!!
 
Kuna ujinga sana hapo Tanzania

Baada ya kuona mpango wa bomba umeshindikana kupitia Kenya

Luto akasema hapana acha tuje na wazo wa refinery ili nao wafaidike na mafuta ya Uganda

Tanzania imezidiwa na Kenya maarifa ya diplomasia ya uchumi

Tanzania itabaki kuwa na leverage ya ardhi tu

Ikumbukwe Kenya haipo kwenye mpango wa EACOP na wala haina hisa kwenye mradi huo

Hii ni baada ya Uganda kukataa bomba lisipitie Lamu bali bandari ya Tanga

Ila Kenya itakuja kufaidika na refinery kama ikijengwa
Jifunze zaidi kuhusu geopolitics na economic diplomacy.

Jipe muda wa kujisomea taarifa zaidi.


In short, ikijengwa hiyo refinery TZ inageuka kuwa ENERGY HUB na Kenya anapoteza mazima, ikiwemo project yao ya LAPSSET kufa.
 
Jifunze zaidi kuhusu geopolitics na economic diplomacy.

Jipe muda wa kujisomea taarifa zaidi.


In short, ikijengwa hiyo refinery TZ inageuka kuwa ENERGY na Kenya anapoteza mazima, ikiwemo project yao ya LAPSSET kufa.
Kwa hiyo Luto alivyotoa hilo wazo ni ili kuipoteza Kenya?

Kama ina faida kwa Tz viongozi wenu walikuwa wapi kuongea na Dangote?

Asiye na hisa kwenye mradi ndio amekuwa msemaji wenu?

Usenge mwingi sana Tz
 
Kwa hiyo Luto alivyotoa hilo wazo ni ili kuipoteza Kenya?

Kama ina faida kwa Tz viongozi wenu walikuwa wapi kuongea na Dangote?

Asiye na hisa kwenye mradi ndio amekuwa msemaji wenu?

Usenge mwingi sana Tz
Kenya imekumbwa sana na madeni kwasasa zaidi ya 70% ya makusanyo yao ya kodi wanalipa madeni ya nje.

Wanataka kuanza kuuza mafuta yao ya Turkana ili kugharamia shughuli za serikali.

Kwasasa, automatically mafuta ya Uganda yanapita TANGA.

Mafuta ya South Sudan yanapita Sudan.

LAPSSET ya Kenya imekufa.

Kenya inaona kukiwa na refinery Tanga, wao mafuta yao watauza Tanga ambayo ni karibu na watanunua mafuta kwa bei ndogo.

Kwa lugha rahisi Kenya awepo au asiwepo, hawezi kumzuia Dangote kujenga Refinery, Tanga au Uganda. Maana hawezi kujenga Kenya halafu aanze kusomba crude oil kwa maroli kutoka Uganda.

Mafuta ni ya Uganda na hana bandari. Tanzania ina bandari na ina hisa EACOP.

Kenya hana usemi zaodi ya kubembeleza na yeye awemo, aidha kwa kununua hisa hapo refinery au kivingine.

TZ kutokuwepo haina maana kuwa hawajashiriki. Ukisikiliza hiyo taarifa, utaona kabisa Kenya ndio wamemtafuta Dangote na Dangote alishafanya maamuzi kuwa refinery yake atajenga Tanga.
 
Back
Top Bottom