Antetokounmpo
JF-Expert Member
- Feb 5, 2020
- 1,239
- 2,023
Kwahyo mkuu raisi atoe walinzi alindwe na malaika [emoji3][emoji3][emoji3]Majibu ya swali hili yako kwenye maandiko matakatifu (Biblia) kwa sisi wakristo. Maana imeandikwa;
Mithali.28:1;
"....Waovu hukimbia japo hawafukuzwi na mtu; lakini waadilifu ni hodari kama simba...."
Tafsiri ya andiko hili ni hii;
Kwamba, mtu yeyote mwovu (anayetawaliwa na uasi (dhambi/uovu) dhidi ya Mungu muumba wake, huamwandamwa na ROHO WA MAUTI muda wote kiasi ambacho huishi kwa mashaka, woga na wasiwasi siku zote za maisha yake hata roho apewapo kibali rasmi za kukamilisha kazi yake...
Mtu wa namna hii muda wote hudhania na kujishuku yeye mwenyewe kuwa anawindwa na nguvu isiyojulikana ili auwawe. Na kwa sababu hutumia njia zote kujaribu kujilinda na kujifariji....
Hii hutokea kwa kuwa Mungu, hachangamani na roho ya uasi/uovu na hivyo humwondolewa neema ya ulinzi wake mtu wa namna hii....
Mtu wa namna anaweza kukimbia ama kukifyatulia risasi hata kivuli chake mwenyewe....!!
Kinyume chake, watu watii na wanyenyekevu mbele za Mungu, wanaoepuka uovu na dhambi dhidi ya Mungu muumba, hawana wasiwasi, hawana woga, hawana mashaka na wameishinda roho ya mauti...
Hawategemei akili na uhodari wa kibinadamu kuwalinda, bali ulinzi wao uko mikononi mwa Mungu mwenyewe [Zaburi 23]
Hawa......ni hodari kama simba!!
Sent using Jamii Forums mobile app