Huu Msafara wa Rais Magufuli sijawahi uona

Huu Msafara wa Rais Magufuli sijawahi uona

Marais wote duniani ni kawaida sana hili,
Ni kawaida kwa rais kuwa na wanausalama,viongz wanaomsindikiza kwenda pengine kwenye tukio husika.

Marekani rais wao alipokuja mbona hamkwongea na walishuka hadi na ma gar yao?

Ukiachana tu na USA,
Yapo mataifa tu hapa Africa ambayo pia ni kawaida sana kwa vitu kama hivi...

So tusishangae sana.

Hata wewe ukiambiwa leo uwe rais lazima ufate Kitu kinaitwa PROTOCOL
Wanaitaga "Security detail" alafu wakati mwingine siyo kwamba raisi hutaka iwe hivyo ila wanaosimamia usalama wake ndio hupanga kulingana na hali waionavyo wao







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni lazima tuwaonyeshe Dunia kuwa nchi yetu hii ni tajiri, tumenyonywa, tumeonewa, tumeitwa masikini sasa ifike mahali tuseme basi.

Raisi ndiye kioo cha nchi, wakimuona yeye Mabeberu wanapata picha kuwa nchi ipo pazuri, yaani in the right track.
 
Yaani hapo ubungo tu ndo mpaka limsafara lote hilo!

Ati "security detail"! Doooh!

Sipati picha hilo foleni lake hapo!

Jamani watanganyika tupunguze ushamba! We can do better!
 
Tulia wewe mama ,wanaume wako kazini
Leo Msafara wa Rais wa wanyonge anayejali kodi za wananchi sijapata uona tangu nizaliwe na Nchi nilizowahi tembelea.

Nimehesabu Magari yamefika 53.
Zote ni V8.

Noma sana.
 
Ukiona magari mengi ujuwe kuna watu mbalimbali wanatakiwa wakajibu hoja huko aendako
Yeye anachokiona pekee ni msafara wa Rais uko kwenye ziara. Hajafanya makosa lakini, maana hata mimi mpaka majuzi tu nilikuwa na uwezo huo tu, wa kuona kama anvyoona yeye
 
Mnataka awe na msafara wa gari nne ,huyo sio mkuu wa wilaya,ni Amiry jeshi mkuu,pia genge lenu la walafi si mnamuwinda?
Alipokwenda Mbeya mwanzoni mwa 2019 kulikuwa magari kati ya 80- 100. Zote hizo zinakula mafuta na maofisa na madreva waliotoka nje ya mkoa wanakula posho ya kuwa nje ya kituo. Halafu bado anadai eti ana bana matumizi kwa ajili ya wanyonge.
 
Majibu ya swali hili yako kwenye maandiko matakatifu (Biblia) kwa sisi wakristo. Maana imeandikwa;

Mithali.28:1;

"....Waovu hukimbia japo hawafukuzwi na mtu; lakini waadilifu ni hodari kama simba...."


Tafsiri ya andiko hili ni hii;

Kwamba, mtu yeyote mwovu (anayetawaliwa na uasi (dhambi/uovu) dhidi ya Mungu muumba wake, huamwandamwa na ROHO WA MAUTI muda wote kiasi ambacho huishi kwa mashaka, woga na wasiwasi siku zote za maisha yake hata roho apewapo kibali rasmi za kukamilisha kazi yake...

Mtu wa namna hii muda wote hudhania na kujishuku yeye mwenyewe kuwa anawindwa na nguvu isiyojulikana ili auwawe. Na kwa sababu hutumia njia zote kujaribu kujilinda na kujifariji....

Hii hutokea kwa kuwa Mungu, hachangamani na roho ya uasi/uovu na hivyo humwondolewa neema ya ulinzi wake mtu wa namna hii....

Mtu wa namna anaweza kukimbia ama kukifyatulia risasi hata kivuli chake mwenyewe....!!

Kinyume chake, watu watii na wanyenyekevu mbele za Mungu, wanaoepuka uovu na dhambi dhidi ya Mungu muumba, hawana wasiwasi, hawana woga, hawana mashaka na wameishinda roho ya mauti...

Hawategemei akili na uhodari wa kibinadamu kuwalinda, bali ulinzi wao uko mikononi mwa Mungu mwenyewe [Zaburi 23]

Hawa......ni hodari kama simba!!
 
Leo Msafara wa Rais wa wanyonge anayejali kodi za wananchi sijapata uona tangu nizaliwe na Nchi nilizowahi tembelea.

Nimehesabu Magari yamefika 53.
Zote ni V8.

Noma sana.
Sasa si ndio umeuona unasemaje hujawahi ona??
 
Amejaa wasiwasi utafikri ni rais wa Rwanda wakati Tanzania hata ndege wa porini wanaishi kwa amani.
 
Jinga wewe unaleta zama za mawe za Julius Nyerere na zama za kisasa za high technology?
Hivi haiwezekani akawa na msafara wa gari hata 2 tu?. Atakuja mwingine hapa atasema tahadhali,tahadhali gari 50?. Nyerere kwa nini aliweza kusafiri na gari moja tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo Msafara wa Rais wa wanyonge anayejali kodi za wananchi sijapata uona tangu nizaliwe na Nchi nilizowahi tembelea.

Nimehesabu Magari yamefika 53.
Zote ni V8.

Noma sana.
mfalme!
 
Back
Top Bottom