Huu mvutano wa TEC, Bakwata na mamlaka, ndio utakaovunja ule mwiko tuliouzoea

Si aondoke tu kwa amani?
 
Sijawahi kujua kuwa Kuna mvutano kati ya TEC na BAKWATA!
Ebu nipashe nijue!
 
Ukiangalia utaona TEC hawavutani na BAKWATA bali wanaiambia serikali itende hali. BAKWATA ndo wanadandia mambo ya TEC na kutafuta mialage za ubishi. By the way hapo ni mbingu na ardhi kwa uwezo wa kufikiri
Kweli kabisa, mi mwenyewe nashangaa bakwata wanatafuta nini hapo kwenye huo mpambano 😇.
Anyway kwatulipo fikia hii nchi inahitaji uamsho mkubwa sana kila mahali.
Nchi hii imechoka kuongozwa kwa Remote yaani watu fulani wajifungie mahali waendelee kupanga cha kufanyika nchini its a big NO.
Tumechoka kuongozwa na watu wa Dini (uislam /ukristo) tunamuhitaji KRISTO MWENYEWE.
 
Yaani kuamini Rais wa Nchi hajui kinachoendelea ni kuiundermine sana taasisi ya Urais.

Mnauchukulia Urais poa sana wazee.
 
Ndiyo maana ninasema kusema Rais anahujumiwa ni kumu-underestimate sana. And that is a huge mistake.

Yeye ndiyo ataamua nini kiwe na kitakuwa. Mfano wahafidhina walikuwa hawataki awakumbatue wapinzani kipindi cha maridhiano lakini aliamua na akafanya hivyo na baadaye alilisema hili hadharani.

The only issue ameona ni kiwa wapinzani wa CDM hawabebeki, baada ya kuwapa platform hiyo. so ameamua kama mbwai iwe mbwai... kwa maoni yangu.
 

Umesahahu akawaita Makhurukutaabhu
 
The only issue ameona ni kiwa wapinzani wa CDM hawabebeki, baada ya kuwapa platform hiyo. so ameamua kama mbwai iwe mbwai... kwa maoni yangu.
"Kwa gharama yoyote ile", sijui kama hili amelipa fikra ya kutosha katika maamuzi yake hayo.
 
"Kwa gharama yoyote ile", sijui kama hili amelipa fikra ya kutosha katika maamuzi yake hayo.
Hicho ni mimi nimeandika, lakini tumeona hii kwa gharama yeyote ikitumika. Mfano JPM aliwahi kusema tuko vitani na mtu anaturudisha nyuma, nakumbuka siku ile ile mtu akamiminiwa mvua ya moto, in the name ya gharama yeyote kuhusu issue za madini na sheria ya madini ikapita. Kelele zilikuwepo lakini ziliisha

Wapinzani wanamchukulia poa sana Rais, lakini yeye anacheza chess yake. Ana mwezi mmoja na nusu tu avunje bunge na nchi iwe kwenye election mode; saiz yuko kwenye Bunge la bajeti, so far wizara nane au Tisa zishasoma bajeti zake na kupitishwa. Kimsingi wizara key zimebaki labda mbili tatu tuuu. Kimsingi hakuna kilicholala, mwezi huu au mwanzoni mwa June anawazindulia kanda ya ziwa lile Daraja, huku huduma za SGR zikienda poa sana...

Ninachohifunza ni kuwa, wafanye watu wakuchukulie poa halafu wewe stick to your plan. Play with time the best way you can. Hii ni siasa tu
 
Umesahahu akawaita Makhurukutaabhu
Sahihi kabisa; nadhani ndicho atakachokifanya kwenye kampeni zake... ni kuwasema tu "nikiwapa kila aina ya platform ila hawa jamaa ni wasaliti hawabebeki" hata hizi purukushani wanazofabya TEC, mara Bunge la EU zitampa sida zaidi Maza in the long run... itaqnza kuonekana wana back up ya wazungu kwa hiyo hawafai kabisa kwa kuwa ni vibaraka... siasa ni timing.

Ushiriki wa ACT pia ni kete ngumu sana, ZZK anajiandaa kuwa KUB... hesabu za siasa ni ngumu mnooo
 
Sijui. May be. Huenda!

Hiyo 'script' ya Magufuli uliyoielezea hapo; kama ndiyo inayofuatwa, si sahihi kusema matokeo tarajiwa yatakuwa ni yale yale kama ya wakati ule. Sijui tutafikia vipi hitimisho la aina hiyo.

Hiyo miradi na uzinduzi wake, ifute fikra za watu juu ya matendo maovu..., this is asking too much!. !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…