Haukua na Mafanikio asilimia 100, ila Nchi hii inaendeshwa na huo Ubinafsishaji wa mkapa,
1. Makampuni Makubwa yote yanayoongoza Ulipaji kodi, TBL, Nmb, CRDB, Airtel, Geita Gold Mining etc ni zao la Ubinafsishaji.
2. Matajiri wa kubwa nchi hii utajiri wao umetokana na Ubinafsishaji
-Mo na Metl yake wana Viwanda vya Nguo, Mashamba ya mkonge ambayo yamebinafsishwa
-Bakhresa wengi wanasema humu viwanda vya ngano vilivyomtoa ni Ubinafsishaji
-Mengi pia alitoka wakati wa Ubinafsishaji.
Hivyo tunaishi Ubinafsishaji, kuna kipindi nchi hii watu walikua wakipanga foleni kupata mahitaji yao, kipindi Kifupi cha Mkapa na Kikwete tumetoka uchumi wa Dola 200 kwa mtu mmoja hadi Dola 1000, walioishia hawa wawili tunatakiwa tuendelee na momentum ile ile
Kama Kuna Vifungu vya kubadili vibadilishwe ila 100% Dp world waje, Bandari sio madini kwamba yatachimbwa yataisha.